Mke wa mtu sumu

mende 2014

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2014
Posts
763
Reaction score
131
Ama kweli mke wa mtu ni sumu kali sana. Jamaa mmoja alikuwa anatembea na mke wa mtu kwa mda mrefu kabla mme wa mke hajagundua. Sasa baada ya mda kupita, alipata taarifa kuwa kuna jamaa anamla mke wake lakini hakuamini ila alichokifanya ni uchunguzi. Siku zikaenda, wiki zikapita lakini hatimaye siku za mwizi ziliwadia. Jamaa siku hiyo alimuona mke wake akielekea sehemu na mke hakujua kama mmewe anamuona. Mme akafuatilia taratbu na hatimaye kumuona mkewe anakutana na jamaa na kuelekea eneo la shamba la migomba. Mme aliendea kunyatia taratibu hadi wahusika walipofika ndani ya shamba hilo na kuanza manjonjo yao. Mme alinyatia na kukuta mkewe kalaliwa na huyo jamaa. Kilichotokea ni kuwa mme akateka panga alilokuwa nalo jamaa na mme kuanza kumdunda jamaa vibao. Mme alikuwa na RUNGU na akawa tena na panga la adui wake. Kilichoendelea ni kwamba jamaa alipigwa kipigo cha kufa mtu kama vile jambazi sugu. Huyo jamaa alipigwa vibaya sana hadi akawa kiwete hadi leo hii. Haya ni ya kweli maana nilishuhudia live bila kusimuliwa na mtu. Jamani, mke wa mtu ni sumu.
 
Ulishuhudia hata picha basi hukupiga au kuchua video tuone wenzio.....
Tyta vipi weye unayo picha?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ulishuhudia hata picha basi hukupiga au kuchua video tuone wenzio.....
Tyta vipi weye unayo picha?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Natumia simu lakini kuweka picha nimeishajaribu nikashindwa.
 
Last edited by a moderator:
Yasikukute haya
 

Attachments

  • 1397909716089.jpg
    7.5 KB · Views: 1,183
Vitu vinavoleta majanga hapa duniani ni Pesa na Papuchi....
 
Kuna jamaa yeye alifanywa kitu mbaya kukawa na mjusi mkubwa anatoka sehemu ya haja ndogo...akawa akitaka kujoa akienda chooni mjusi anatoka jamaa anakojoa, kabla ya kufunga suruali mjusi anaingia tena kupitia sehemu ya kutolea haja ndogo..
Hayo maumivu aliokuwa anayapata wakati mjusi anaingia yalikuwa ni makali saaana.!
Akaenda kuomba msamaha kwa mume ndo kupata salama
 
Kwa kawaida mke wa mtu ni sumu. Lkn wao wanajibadili kutoka sumu wanakuwa sweet honey. Sasa mtu akilamba nani wa kulaumiwa
 
ogopa sana mke wa mtu km unapenda usalama wa maisha yako,na kwann uchukue mke wa mtu???
 
Ila pamoja ya kuwa sumu hao wake za watu,ila mijianaume haikomii!
 
Kuna sababu ya mwanamke kutoka nje. Kama unagawa au kutoa dozi ndogo ataacha kutoka nje? Waume wapeni wake zenu dozi ya maana. Hujakata kiu yake ataacha kutoka?
 
bold:
1. ulikwa ukimfuatia mwenye mke au wezi? huwezi kuwepo sehemu zote mbili
2. Chabo inakuhusu.
3. kwa nini hukuamulia kabla jamaa kuumizwa kiasi hicho? au nawe ulishiriki kumpiga jamaa?
 
bold:
1. ulikwa ukimfuatia mwenye mke au wezi? huwezi kuwepo sehemu zote mbili
2. Chabo inakuhusu.
3. kwa nini hukuamulia kabla jamaa kuumizwa kiasi hicho? au nawe ulishiriki kumpiga jamaa?

Nilichokishuhudia ni kipigo alichokuwa anapewa jamaa ila kule kwenye mgomba mwenye mke ndo alitusimulia. Mwenye mke hakuweza kumruhusu mtu yeyote kumzigelea maana alikuwa na panga na rungu ambapo hata rafiki yake wa karibu sana hakuweza kumsikiliza alipojaribu kumzua. Sio siri sie wenye ndoa zetu tuchunge sana.
 

"Haya ni ya kweli maana nilishuhudia live bila kusimuliwa na mtu".

"kule kwenye mgomba mwenye mke ndo alitusimulia"


Mind your tongue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…