Mke wa mtu karaha

Starwars91

Member
Joined
Jul 12, 2020
Posts
52
Reaction score
47
Mimi ni kijana ambaye bado sijawa na familia. Ila nafanya kazi na naishi mwenyewe kwa kujitegemea.

Kuna dada nilikutana naye kabla hajaolewa. Nikawa nimempenda nikamuomba tuwe pamoja. Kwa bahati mbaya aliolewa na sikuweza kupata nafasi ya kuwa naye.

Alimpata mume akaenda kwake. Nikamsahau. Baada ya miezi kadhaa, nikakutana naye barabarani. Akanisalimia kwa bashasha kweli ananiambia kanimiss. Mimi sawa tu. Kumbe hakufuta namba yangu. Kesho yake akanipigia. Nikapiga naye story kidogo.

Akawa kama anazoea. Siku moja nikamjaribu nikamwambia aje nyumban. Akaniambia atakuja jioni. Kweli akaja na nikafanya naye mapenzi. Sasa kumbe alikuwa na mimba ya miezi miwili. Nikashangaa sana. Yaani ana mume ana mimba lakin kaja. Mpaka Leo simuelewi. Aliniomba elfu kumi na nilimpa. Ila nataka niblock kabisaaa. Haiwezekan. Target yake ni nini?
 
uliposema wewe ni kijana na bado haujaanzisha familia, nmekuelewa hvyo sina cha kuchangia zaidi
 
Uhawala huwa haufi! Hapo uamuzi wa busara ni wako! Kama tayari ulishajua ni mke wa mtu basi hakukua na haja hata ya kumuita gheto! Ukionja penzi la mke wa mtu huwa ni shida sana kumuacha, Huku sauti nyingine inakwambia achana nae, Huku sauti nyingine itakwambia kula mzigo wa mwisho then ndipo ukate! Basi inakuwa hivohivo mpaka jamaa anakuja kukufuma tena akiwa na jambia, hapo ndipo utajuta kuzaliwa! Trust me, huo uamuzi wako wa kutaka kumblock ndio uamuzi sahihi na usifikiri tofauti na hapo!
 
We hauwajui wanawake wa siku hizi walivyo na akili mbovu especially wake za watu wa siku hizi.

Achana na wake za watu. Usijebeba laana ya kugongewa mke bure. Unavyotembea na huyo na wewe ipo siku utajapata mwanamke atakae kuwa na yeye anatoka nje ya ndoa hivyo hivyo.
 
mfate mme wake umwambie kila kitu ila usisahau kubeba vilainishi nakusihi tena usisahau kubeba vilainishi utakuja kunishukuru
 
Tukusaidieje?,nyie ndo mnaoshinda kwenye vijiweni vya kahawa kuichafua CCM kuwa haitoi ajira ilikhali mnatembea na wake za watu
 
Achana naye haraka iwezekanavyo vinginevyo jiandae kushikishwa ukuta. Mke wa mtu ni sumu kali
 
Ulikuwa unajua ni mke wa mtu then ukatembea nae na bado hujui target yake....achana na mke wa mtu.
 
Kijana chunga sana usije kuja jutia badae huko achana nae uyoo
 
Target yake itakua ni wewe utolewe bikra ya ndukum
 
...apa sometime ndo ile akili ya kuoa mke bikra inakuja....daaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…