Mke wa Dk Slaa apata dhamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa Dk Slaa apata dhamana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prodigal Son, Feb 15, 2010.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Mussa Juma, Arusha

  MKE wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Rose Kamili, ambaye Diwani wa CCM wa Kata ya Bassotu, wilayani Hanang, amelituhumu jeshi la polisi wilayani Hanang kutumika kisiasa kutokana na kutekeleza maagizo ya kigogo mmoja kutaka yeye akamatwe pamoja na viongozi wa wafugaji.

  Diwani huyo, ambaye ametangaza kugombea ubunge jimbo hilo la Hanang katika uchaguzi mkuu ujao kupitia CCM, alisema kukamatwa kwake juzi pamoja na wananchi wengine 13 ni shinikizo la kigogo huyo.

  "Polisi wamenikata na kunipa dhamana mimi na Ally Kaoga jana na wamegoma kutoa dhamana kwa wananchi wengine 12 hili ni shinikizo la kigogo huyo tumepata taarifa amewaahidi baadhi ya wakulima kuwapa mashamba na wanataka kuzuwia dhamana ili walazimishe ugawaji wa mashamba," alisema Rose Kamili.

  Kamili ambaye ni Diwani wa CCM tangu mwaka 1994 na amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya CCM ikiwepo ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, alisema mgogoro wa mashamba ya Hanang hivi sasa umefanywa wa kisiasa ili kuficha ukweli.

  "Mimi nasema ugawaji wa mashamba Hanang uwe wa haki na wafugaji wapewe haki yao kwani kihistoria wao ndio walipokonywa na serikali maeneo yao na kuwafanya watawanyike karibu nchi nzima ili kuanzisha shirika la chakula la NAFCO," alisema Kamili.

  Diwani huyo alisema kitendo cha kigogo huyo, kutembelea eneo la mgogoro kufanya mkutano wa hadhara juzi na kuahidi kuwashughulikia watu aliowaita wachochezi ni ishara kuwa suala hilo limekuwa la kisiasa.

  "Mimi wanasema ni mchochezi nawachochea wafugaji wasikubali mgawanyo wa shamba eti nafanya mikutano usiku....huu ni uongo kwani wafugaji kama watanzania wengine lazima haki yao ijulikane na ndicho nimekuwa nikitetea,"alisema Kamili.

  Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Permena Sumari alikanusha tuhuma kuwa polisi inatumika kisiasa katika kutatua mgogoro wa ugawaji wa mashamba ya Hanang.

  "Sisi hatufuati siasa tunaowakamata tutawafikisha mahakamani kwa tuhuma za kufanya uvamizi kwa viongozi wasigawe ardhi na kuwashambulia wananchi wengine kwa silaha,"alisema Sumari.

  Kamanda huyo alifafanua kuwa,operesheni ya kuwakamata wananchi wote waliohusika na vurugu itaendelea hadi wote wawe wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

  "Ambao tumewakamata tumewanyima dhamana kwa sababu za kiusalama na sio kisiasa kwani hakuna shaka kuwa vurugu zilitokea na watu kujeruhiwa,"alisema Sumari.

  Februari 11 mwaka huu, viongozi wa serikali ya kijiji cha Mulbadaw pamoja na wananchi wengine walishambuliwa na kundi la wafugaji ambao walikuwa wanapinga eneo lao kugawanywa kwa wakulima.

  Katika vurugu hizo watu zaidi ya 10 walijeruhiwa vibaya kwa silaha za jadi na hadi jana watu wanne walikuwa bado wamelazwa katika hospitali ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) ya Haydom.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  serekali hii kila kukicha inawaonea wafugaji, na kwa sasa wamekuwa kama wakimbizi katika nchi yao, kati ya viongozi ambao walikuwa mstari wa mbele kuwatetea wafugaji alikuwa Sokoine peke yake
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 180
  kigogo fulani?...taja hilo jina unaogopa nini!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,259
  Trophy Points: 280
  2010-02-15

  [​IMG]
  Opposition parliamentarian Willibrod Slaa with his wife, CCM councillor Rose Kamili, who was arrested on Saturday for allegedly inciting violence.

  The wife of opposition leader Willibrod Slaa yesterday accused powerful forces of being behind her arrest and overnight detention in a police cell in Hanang District.

  Ms Rose Kamili told journalists after her release that police were being used to undermine her politically, adding that she was arrested on Saturday on the orders of a "big shot".

  But the Hanang District police boss, Mr Permena Sumari, swiftly denied the claims, saying the police were only performing their duties as custodians of the law.

  Ms Kamili said police had become partisan, adding that this was unacceptable. "The police are being used to undermine me 'they are being used to further the political interests of a big shot' they were ordered by the big shot to arrest me."

  Ms Kamili, who is the Councillor for Bassotu Ward in Hanang District, has declared her intention to vie for the Hanang parliamentary seat currently held by Dr Mary Nagu, who is also the Industry, Trade and Marketing minister.

  She was arrested along with 13 other people on suspicion of incitement, but said yesterday that only two of them were released on police bond.
   
 5. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  B.A.K

  Naona kama hapo umeweka taarifa mbili vile zenye content tofauti
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,624
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Imeshaelezwa baadhi ya wanasiasa hawana kazi kama wataanguka ktk siasa. wanaweza hata kuua kabisa!
   
 7. bht

  bht JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  yep hiyo para ya mwisho sijui imekaaje..........ni taarifa tofauti
   
 8. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwamba wife wa mh. slaa ni ccm?! sasa kama ameshindwa kum-influence wife wake kwa sera za chama chake watz wengine inakuwaje? au sioni vizuri miye?
   
 9. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45

  Amtaje hajipendi??? sasa hivi wanapambana kufa na kupona
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,810
  Likes Received: 4,385
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani ukiwa na mke hamruhusiwi kutofautiana kimawazo na kimsimamo? Rose Kamili anaweza kuwa mke wa Dr. Slaa. LAKINI anabaki yeye kama yeye na uhuru wa kujiamlia what she thinks is good for her and her country. Ni wanasiasa wengi sana ulimwenguni wana spouses ambao wanatofautiana kimtizamo. Mfano Gavana wa Carlifornia ni Republican damu na mke wake ni Democrat damu. Anyway, kwa hili la Slaa nadhani ni jambo jema kuona couple yote iko active kwenye politics. Inaonyesha kwenye hiyo familia kuna "democracy". Maana mume hajamlazimisha mke akubaliane naye kimawazo.

  Big up Dr. Slaa, big up mama Kamili.
   
 11. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,633
  Likes Received: 4,142
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli kwa Great Thinkers,kumbe ni makosa kwa mke na mume kutofautiana kisiasa?Sikujua kama hilo ni kosa hadi mwenzetu Great Thinker Outlier alipotueleza hivyo!

  Na labda sijakuelewa vyema Outliner,sasa kama mme akawa unamueleza sera za chama chako mkewe lkn mke hajavutiwa nazo na kukataa kujiunga na chama cha mme, ungekuwa wewe unamuacha kwa kumpa talaka huyo mkeo au?

  Soma habari hii mkuu Outlier;Kule CALIFORNIA-USA; wakati Anorld Sch ni Gavana wa jimbo hilo kupitia chama cha Republican lkn mke wake ni mwanachama maarufu wa Democratic na hata alimsadia waziwazi Obama kwa fedha kwenye uchaguzi wa mwaka 2008!Kwa maana hiyo Gavana amuache mkewe au?

  Si kweli kuwa mkiwa Mke/mme basi ni lzm muwe mnafuatana kwa sera na eti hamna kupingana,kumbuka no matter what kila mtu ana haki ya kuamini akiaminicho!
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nagu
   
 13. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 531
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  There is only one part in the bedroom( CALLED FAMILY), how was in when anorld showzneger ;s wife and girl was with obama while the dad is with McCain?? Only Kenyan women where able to boycott their man on their conjugal rights
   
 14. M

  Mikefe Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ms Rose , kumbuka wewe kiongozi wa serikali ya mtaa(local government).Wewe umevunja sheria kwa sababu serikali kuu ilikuwa ikiwagawia ardhi wananchi. Uliwezaje kukiuka maamudhi ya serikali kuu wakati wewe ni diwani.Ulitakiwa kujiuzulu kabla ya kuwatetea hao unaosema kwamba wanaonewa.Ulitakiwa kutetea serikali kuu kwa sababu it's ur boss.Uwemwangalifu sana. Usije ukaishia pabaya.

  I know you and I love u
   
 15. M

  Mikefe Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jame is Democrat and his wife is Repulican , nothing wrong with that
   
 16. M

  Mikefe Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  James Carvel is Democrat and Mary is Republican,Mary is Jame's wife.It's democracy.Zip ur mouth dude
   
 17. M

  Mikefe Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kinyabis who is nagu to foolish. b careful
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,375
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280
  wewe vipi? wengine wakigombea kwa tiketi ya ccm wanaaandamwa wanakuwa gumzo na wanaonekana kioja.

  Lakini mke wa kigogo wa chadema kugombea ccm, utasikia wakisema mwacheni atumie uhuru wake, eti hapo ndo inaonekana jinsi gani Slaa kakomaa kisiasa.

  kwa kweli falsafa hii binafsi siilewi wana i-apply vipi?
   
 19. b

  bigilankana Senior Member

  #19
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani hakuna ubaya wowote kwa mke wa Katibu wa CHADEMA kuwa Diwani wa CCM na hata kuwa Mbunge wa CCM.

  Marehemu Chacha Wangwe alipokasirishwa na CHADEMA walipomwambia anatoa siri za chama chao, akawauliza kati ya yeye na Slaa nani anatoa siri. kwani yeye makamu Mwenyekiti akimpigia simu Katibu Mkuu, anapokea mwana CCM anasema Mzee anaoga..... Chacha alikuwa na vituko kweli.

  Kwa demokrasia kukomaa nadhani masuala ya watu binafsi yawe binafsi tu la muhimu ni kutekeleza wajibu tu wa kila mmoja.

  Wasiwasi mkubwa ni huyu mwanamke kutumiwa kama alipotumiwa wakati ule wa Sumaye kwa kutengeneza fumanizi bandia pale Dodoma dhidi ya Dokta Slaa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...