Winnie Byanyima: Hali ya Kizza Besigye ni mbaya, hawezi kuongea

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,603
Reaction score
22,717
Akizungumza nje ya hospitali ya Mulago jijini Kampala alikolazwa mumewe, Byanyima ambaye ni Mkuruzengi Mkuu wa shirika la UNAIDS, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mumewe hawezi kuzungumza wala kuandika kwa sababu mikono yake haina nguvu.

Besigye, mwenye umri wa miaka 70, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, amekuwa gerezani tangu mwishoni mwa mwaka 2024 alipotekwa nyara nchini Kenya na kurudishwa Uganda kwa njia ya kisiri.

Besigye alilazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, baada ya kuzimia wakati wa kikao cha mahakama mnamo Julai 30. Alianguka muda mfupi baada ya kukemea uamuzi wa mahakama wa kuteua mawakili wa kumwakilisha.

Wakili wake mkuu wa utetezi, Erik Lukwago, alikamatwa, huku waziri wa zamani wa sheria wa Kenya Martha Karua, mwanachama mwingine wa timu yake ya mawakili, akizuiliwa kuingia Uganda. Alisema haki za Besigye za kuishi, kupata huduma sahihi za matibabu na kesi yake kuendeshwa kwa njia ya haki lazima ziheshimiwe, akisema kuwa "zinapuuzwa".

Soma Kiongozi wa upinzani Uganda ni dhaifu sana hospitalini
 
Mke wa Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, Winnie Byanyima ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini, amesema hali ya afya ya mume wake ni mbaya, ni dhaifu na hawezi kuzungumza.

Besigye mwenye umri wa miaka 70, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) jijini Kampala baada ya kuanguka wakati wa kikao cha mahakama Julai 30.

Kuanguka kwake kulitokea muda mfupi baada ya kupinga uamuzi wa mahakama wa kumteua mawakili wa kumwakilisha. Wakili wake mkuu wa utetezi, Erik Lukwago, alikamatwa huku Martha Karua akizuiwa kuingia Uganda.

Byanyima amesema mume wake anaonekana dhaifu sana, amekuwa akilala kwa muda mrefu na bado hawezi kuzungumza wala kuandika kutokana na hali ya mikono yake kutokuwa imara.

Amesema awali Besigye alikuwa akipewa chakula kupitia mshipa wa damu, lakini baada ya hali yake kuimarika kidogo, mirija hiyo imeondolewa na ameanza kunywa supu.
 
Akizungumza nje ya hospitali ya Mulago jijini Kampala alikolazwa mumewe, Byanyima ambaye ni Mkuruzengi Mkuu wa shirika la UNAIDS, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mumewe hawezi kuzungumza wala kuandika kwa sababu mikono yake haina nguvu.

Besigye, mwenye umri wa miaka 70, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, amekuwa gerezani tangu mwishoni mwa mwaka 2024 alipotekwa nyara nchini Kenya na kurudishwa Uganda kwa njia ya kisiri.

Besigye alilazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, baada ya kuzimia wakati wa kikao cha mahakama mnamo Julai 30. Alianguka muda mfupi baada ya kukemea uamuzi wa mahakama wa kuteua mawakili wa kumwakilisha.

Wakili wake mkuu wa utetezi, Erik Lukwago, alikamatwa, huku waziri wa zamani wa sheria wa Kenya Martha Karua, mwanachama mwingine wa timu yake ya mawakili, akizuiliwa kuingia Uganda. Alisema haki za Besigye za kuishi, kupata huduma sahihi za matibabu na kesi yake kuendeshwa kwa njia ya haki lazima ziheshimiwe, akisema kuwa "zinapuuzwa".

Soma Kiongozi wa upinzani Uganda ni dhaifu sana hospitalini
Umri umeenda Yule Mzee, ameitumikia Uganda kwa uaminifu mkubwa
 
Back
Top Bottom