MKE MWEMA NI YUPI

Nyanda lunduma

Senior Member
Apr 10, 2015
187
68
1. Anayejali watu wa nyumbani mwake, hutunza siri siyo kutapanya nje maneno ya ndani na kila mtu anajua, huomba ushauri kwa wazee na si kwa vijana ambao wao siku zote hufikiri kuharibu
2. Humpa heshima zote mme wake, na haigi mabaya kutoka kwa wanawake wengine
3. Humzalia mmewe watoto, siyo anatumia madawa ili kuzuia asizae au kutoa mimba, hii yote huonesha kutokuwa tayari kwa mwanamke huyu kuishi maisha ya ndoa
4. Hupenda watu wote, na wa familia ya mme wake, hana ubaguzi wala uchoyo, hajivunii kati ya aliyo nayo bali hujivunia mmewe
5. Haendeshwi na maneno ya watu, kwani wengi wa wanawake wa dunia hii hupenda kusikiliza maneno yatokayo nje, akiambiwa neno hulitafakari kwa kina kabla ya kumnenea mmewe
6. Hashindani na mmewe, na wala kumfanyia makusudu ya kutopika kwa wakati, (hamjali pindi anapoumwa, hupenda kukashfu mmewe, na kila alisemalo mme wake yeye daima ni wakupinga) hayo mabaya yeye hatendi
7. Ni pambo la nyumba, awapo nyumbani nyumba hung'aa na kupendeza sana, watu huwa na furaha daima na kukosekana kwake ni huzuni ndani ya nyumba.
8. Hulinda ndoa yake, hakimbilii kuachana, hufanya suluhu katika kila mikwaruzano ndani ya familia
9. Moyo wake kaelekeza kwa mmewe na humuenzi na kumuona mfalme wa nyumba kwa ulinzi na utulivu nyumbani
10. Hata akimzidi mmewe cheo, elimu au mshahara bado anakuwa na nidhamu ya hali ya juu na kumpenda mme wake daima bila kuwa na dharau au kiburi chochote
11. Anakuwa na mawazo chanya, hatapanyi pesa, ni mwaminifu kwa mmewe kwa kutobeba mimba nje ya ndoa, hufikiria namna kuwa na maendeleo katika familia yake,
12. Huwa kiongozi na kukumbusha mfalme ibada za nyumbani, anapenda kumtumikia Mungu zaidi na kumuomba kwa bidii, hawi na hali yoyote ile itakayofanya wasifanye ibada au kutokwenda kwenye ibada, huwafundisha watoto wake njia iliyonjema, hulinda ndoa yake.

WANAUME/WANAWAKE WALIOOA NA KUOLEWA, USIONE KUWA KWA FULANI WANAISHI VIZURI MPAKA UKATAMANI UNGEMUOA YULE AU UNGEOLEWA NA YULE, HUJUI YA NDANI NA HUENDA WANASHIDA KUBWA SANA NDANI AFADHALI YA KWENU, FURAHA YA MAISHA NI MNAPO AMUA KUWA MWILI MMOJA LAKINI MKIISHI KWA KILA MTU NA MWILI WAKE KAMWE AMANI HAITAKWEPO.

WANAUME TUISHI KWA AKILI NA WAKE ZETU, NI VIUMBE DHAIFU, HATA AWE NA ELIMU KUBWA KIASI GANI BADO NI MDHAIFU, TUTUMIE AKILI MUNGU ALIYOZOTUJALI, USIPOTUMIA AKILI UTAOA KILA SIKU NA HUTAMPATA MKE MWEMA, KUWA MAKINI NA UJUE WEWE NDIWE BABA NA KICHWA CHA FAMILIA.
 
Back
Top Bottom