Mke mpumbavu hutoka nje na kueleza mapungufu ya mume wake, ndiyo mwanzo wa ndoa kubomoka


tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
5,173
Likes
4,002
Points
280
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
5,173 4,002 280
Matofali 10 ya ndoa bora!

1.Lazima ujue kwamba wewe ni mke na ni wajibu wako kushuka na kumtii mumeo “enyi wake watiini waume zenu kama kutaniko linavyomti Mungu

2.Lazima ujue kwamba mumeo ni kiongozi wako, haijalishi uko smart kiasi gani, mume anabaki kuwa mume hata ukiwa rais wa nchi, ukirudi nyumbani unakuwa mke wa mtu; hapo elimu, nafasi, cheo, umaarufu havifanyi kazi.
“mume ni kichwa cha mkewe hata kama kichwa hakina akili bado ni kichwa, na unadhirisha usivyo na akili zaidi kwa kukubali kuolewa na mjinga umeshaolewa, umegundua ni mjinga, ishi naye kwa akili na msaidie kujua nafasi yake na muache akae kwenye nafasi yake”

3.Usiwe mjinga kiasi cha kutoka nje kwenda kueleza mapungufu ya mumeo; midomo ya wanawake wengi imevunja ndoa zao hao mashoga, marafiki, ndugu zako watakusikiliza ila hawatatatua shida zako bali watachangia kuibomoa.
“mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe”

4.Simama kidete na umlinde mumeo anaposhambuliwa… chako ni chako hata kama kina mapungufu… mtetee mumeo mbele za watu na mkosoe mnapokuwa wawili chumbani.
“naye abigaili akamwangukia daudi akamfichia mumewe aibu na kumlinda asiuawe”

5.Mumeo akitoka nje ya ndoa kutafuta nyumba ndogo, kabla ya kutafuta pepo aliyemwingia, tafuta mlango ambao huyo pepo ameutumia… inawezekana ulipokuwa single ulikuwa unajipenda, unapiga pamba mpaka basi, umeolewa unajivalia kivyovyote [shauri yako]; inawezekana ulipokuwa hujampata lugha yako ilikuwa super, lakini sasa unajibu unavyojisikia [shauri yako]; inawezekana ulipokuwa hujavaa pete ulikuwa unawapenda na kuwathamini ndugu na wazazi wake, lakini ulipoingia tu, ndio umeona karaha ya mawifi na ndugu wa mume [shauri yako]… inawezekana ni kitandani [biblia inasema mke hana umiliki juu ya mwili wake isipokuwa mumewe] usisahau hii ni ya muhimu sana, ukisema anakuchosha “kwa kukujia mara kwa mara” [shauri yako]!
“mungu amefanya jambo jipya duniani ya kwamba mwanamke atamlinda mwanaume”

6.Usisahau kwamba ni wajibu wa mke kuamka kabla usiku haujaisha na kupiga kazi zote za muhimu ndani… biblia imesema hili, mithali 31 [biblia haisemi ni kazi ya house girl; ukimpa house girl azipige umempa nafasi ya kuwa mke badala yake, maana ni kazi za mke mwema hizi]
“mke mwema huamka kabla usiku haujaisha ili kuweka sawa mambo ya nyumbani mwake kwa siku inayoanza baada ya usiku huo”

7.Ni lazima mke awe na kitu cha kufanya… ukiwa tu golikipa, hakuna viungo wala mabeki kukulinda utafungwa magoli.
Mke ambaye ana akili nzuri lazima awe na kitu cha kuingiza kipato…afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kutunza watu wa nyumbani kwake, mithali 31 iko wazi kama unataka ndoa yako isimame, ukikwepa imekula kwako!
“mke mwema hufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kuwapa chakula watu wa nyumbani kwake”

8.Mke mwenye hekima anaulinda uhusiano na mama mkwe [hii ni zawadi ya pekee kwa mumeo], moyo wa mtoto wa kiume humpenda na kumjali mama, usisahau hii itakusaidia, ni silaha muhimu ya vita!
Soma kitabu cha ruthu utaona ruthu alivyocheza kete zake vizuri na kuuteka moyo wa mama mkwe.
“mke mwenye busara huhakikisha anauteka moyo wa mumewe kwa kuwa kipenzi cha mama mkwe”

9.Mke mwenye busara anajua ya kwamba ni jambo moja kuwa mzazi [mwanamke aliyezaa] na ni jambo jingine kuwa mama.
Kuzaa ni kuporomosha kiumbe baada ya miezi 9 aliyoweka mungu lakini kuwa mama kunategemea malezi sahihi na bora yatakayoweka msingi mwema na bora usiofutika kwa mwanao.
“mke mwema humlea mtoto wake katika njia impasayo ambayo hataiacha hata atakapokuwa mzee”

10.Mke mwenye hekima huuweka moyo wake kwa mungu: huku ndiko anakoeleza mapungufu yake, mapungufu ya mume wake, na kukabidhi ndoa yao kwenye mikono salama na makini ya mungu. Mungu anaweza kubadili chochote ambacho wazazi, washenga au washauri wa ndoa hawawezi kugeuza au kutatua.
“mke mwema hufunga na kuomba kwa ajili ya mumewe, ndoa na familia yake… ni rafiki wa uwepo wa mungu”
 
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Messages
949
Likes
671
Points
180
Age
45
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2016
949 671 180
mnatumia muda mwingi kuwafunda wanawake wakati kizazi cha kiume kinapotea kwa kasi
Umefikiri kweli mamdogo kabla hujajibu? Wanaosababisha ndoa zivunjike mostly in wanawake. Mfano mke was mtu unakubali kutembea na mme wa mwenzio, au kijana au Bo's wako kazini. Mwanamke angekuwa na akili anapotongozwa akatae hata yasingekuwepo. Mkitongozwa tu mmekubali bila kujali huyo anaekutongoza ni nani. Wengine hata chupi zenu wanafua housegirls. Nguo za mmeo anafua yeye, unalala hadi hadi uamshwe eti kwa kuwa wewe ni bosi kazini kwenu. MNA vituko vingi kuliko kizazi cha kiume. Sasa kuwa mbishi ule jeuri yako. Samahani kwa kusema ukweli.
 
agata edward

agata edward

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2014
Messages
4,423
Likes
5,712
Points
280
Age
28
agata edward

agata edward

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2014
4,423 5,712 280
Umefikiri kweli mamdogo kabla hujajibu? Wanaosababisha ndoa zivunjike mostly in wanawake. Mfano mke was mtu unakubali kutembea na mme wa mwenzio, au kijana au Bo's wako kazini. Mwanamke angekuwa na akili anapotongozwa akatae hata yasingekuwepo. Mkitongozwa tu mmekubali bila kujali huyo anaekutongoza ni nani. Wengine hata chupi zenu wanafua housegirls. Nguo za mmeo anafua yeye, unalala hadi hadi uamshwe eti kwa kuwa wewe ni bosi kazini kwenu. MNA vituko vingi kuliko kizazi cha kiume. Sasa kuwa mbishi ule jeuri yako. Samahani kwa kusema ukweli.
ungejipa muda wakuchunguza usingehaha hivi pole
 
masai dada

masai dada

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Messages
13,240
Likes
635
Points
280
masai dada

masai dada

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2013
13,240 635 280
Ndoa ni watu wawili..si mwanamke tu..na mume wake pia
 
T

to yeye

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Messages
2,634
Likes
2,123
Points
280
Age
30
T

to yeye

JF-Expert Member
Joined May 30, 2016
2,634 2,123 280
Enyi wanaume watiini wake zenu,kupewa mamlaka ya kuongoza isiwe chambo cha kutudharau
 
H

hii sasa kali

Senior Member
Joined
Jun 12, 2017
Messages
166
Likes
189
Points
60
H

hii sasa kali

Senior Member
Joined Jun 12, 2017
166 189 60
Mwanaume asie na Mungu hawezi kua kichwa bali mkia wa familia
Wewe unataka mwanamke akutunzie udhaifu wako wkt ww unatangaza wake pia unataka akutii wakati ww hujaonesha upendo


Mtii Mungu wako kwanza ewe mwanaume uone kama Mungu hatamfanya huyo mwanamke akutii wewe
 
Hajar

Hajar

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
25,498
Likes
66,022
Points
280
Hajar

Hajar

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
25,498 66,022 280
Shida inapokuja ni pale mke anapokuwa navyo vyote hivyo halafu mume hamna kitu.

Kwa hili wote kwa pamoja inatakiwa tujue kuheshimiana, kuvumiliana, kufichiana siri, kuoneana huruma na vingine vingi na sio kuelemea upande mmoja pekee.
 
D

Dorrlyn

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2017
Messages
543
Likes
599
Points
180
D

Dorrlyn

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2017
543 599 180
Ndoa ni ya watu wawili na ni jukumu LA kila MTU kulibeba, hakuna Yesu na usitegemee mwanamke are replace Yesu ati alikuja kubeba mizigo ya wana dhambi na binadamu, hiyo Yesu original alishamaliza msabalani. Tuliobaki ni kila MTU ajue jukumu lake. Kuhusu kufunga mdomo mbona tu naona wanaume wakiongelea vibaya wake zao tena sana tu akitaka apate mwingine ni lazima akandie aliye naye na hii mbinh hata wake zenu wanatumia ili apate mpango wa kando lazima akandie Mme wake. Cha muhimu jua kwa nini unaoa au kuolewa hakikisha uko na perfect match. Mshikirishe Mungu ktk kila jambo.
 
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
5,173
Likes
4,002
Points
280
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
5,173 4,002 280
Shida inapokuja ni pale mke anapokuwa navyo vyote hivyo halafu mume hamna kitu.

Kwa hili wote kwa pamoja inatakiwa tujue kuheshimiana, kuvumiliana, kufichiana siri, kuoneana huruma na vingine vingi na sio kuelemea upande mmoja pekee.
Ni kweli kabisa
 
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
5,173
Likes
4,002
Points
280
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
5,173 4,002 280
Mwanaume asie na Mungu hawezi kua kichwa bali mkia wa familia
Wewe unataka mwanamke akutunzie udhaifu wako wkt ww unatangaza wake pia unataka akutii wakati ww hujaonesha upendo


Mtii Mungu wako kwanza ewe mwanaume uone kama Mungu hatamfanya huyo mwanamke akutii wewe
Kabisa Kumjua Mungu ni muhimu sana
 
M

mkweli sister

Member
Joined
Nov 6, 2017
Messages
82
Likes
123
Points
40
M

mkweli sister

Member
Joined Nov 6, 2017
82 123 40
ahaaaa kuna mdada aliniambia mume wake akiingiza tu anakojoa .hajui kugegeda kabisa.huwa nikimcheki yule baba nacheeka .akaja na picha ya kibamia chake akatuonesha saluni yaani ni shida
 

Forum statistics

Threads 1,235,705
Members 474,712
Posts 29,231,179