Mke mmoja hatoshi kwa mwanaume aliyekamilika

Mke mmoja hatoshi kwa mwanaume aliyekamilika

aliyetegwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
320
Reaction score
525
Wadau nimekutana na hii sijajua malijali wenzangu mko na maoni gani, kavipi tupia machache hapa.

*MKE MMOJA HATOSHI*

Mke Mmoja Si
Mke,
waume Nawaambia.
Mke Apendae
Peke,
mahaba Hajayajua,
anaogopa
Wenzake,
wasije Kumpindua.
Mke Mmoja hatoshi,
kwa Mume Alotimia..

Ndoa Yataka Makeke,
mke Kujifaragua..
Huba Mshike Mshike,
mizungu Kuipindua..
Sasa Yuko PekeYake,
vipi Atajitambua..
Mke Mmoja Hatoshi,
kwa Mume Alotimia..

Akisema kasirike,
kichura tajilalia..
Siku kisemaAchoke,
mto Utakumbatia..
Ikifika Ada Yake,
wiki Yote Utalia..
Mke Mmoja Hatoshi,
kwa Mume Alotimia.

Pia akijifungua,
Au kwa maradhi pia.
Mume hapo utajua,
Hekima yake jalia.
Wanne walotimia,
Uadilifu kujua.
Mke Mmoja Hatoshi,
kwa Mume Alotimia.

Allah na hekima zake,
Amri hio kutoa.
Idadi ya wanawake,
Mara nne yapitia.
Kila mmoja na wake,
Wengine wapi takua.
Sitara kwa wote wake,
Kuliko kuchepukia.
Haiwi kwa waja wake,
Allah kuwadhulumia.
Ety kuongeza mke,
Ni dosari kweny ndoa.
Mke Mmoja Hatoshi,
kwa Mume Alotimia;
 
Hakika MUME mmoja HATOSHI Kwa MWANAMKE wa sasa aliyekamilika SEKTA zote tatu muhimu yaani
UCHUKUZI, UTALII na MALI ASILI.
 
Kuna wanawake wana appetite ni hatari, huyo huyo mmoja anaweza kukutoa kamasi labda uamue kumfanyia makusudi na kumnyima au awe mjamzito ndipo utafute mchepuko.
 
mke mmoja hatoshi🙄🙄🙄 labda ni kuongea kwaajili ya kujifurahisha tu. Maana wengi wenu ht huyo mke mmoja hamuwezi kumtosheleza mahitaji yake yote ya msingi, sembuse kuwa na wanawake wengi. Labda km mnataka tuwe tunazika kila siku maana hakika wengi mtakuwa mnakutwa mmekufa.
 
Back
Top Bottom