Mkataba wa Halotel/Vietel

selemala

JF-Expert Member
Feb 14, 2007
370
253
"Prof. Mbarawa alisema kuwa Tanzania imekuwa na ushirikiano na Vietnam kupitia Kampuni ya Viettel kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya kufikisha huduma za mawasiliano vijiini kwa kutiliana saini Mkataba. Mkataba huo ni wa miaka mitatu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2014 hadi Novemba, 2017 ikijumuisha ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wenye urefu wa kilomita 20,000 kwenye wilaya zote nchini; kujenga miundombinu ya mawasiliano kwenye vijiji 4,000; kuunganisha Ofisi za Wakuu wa Wilaya; hospitali za Wilaya; Ofisi zote za Posta za Wilaya; na kupeleka na kutoa huduma za intaneti bila malipo kwenye shule 3 za Sekondari za Serikali katika kila Wilaya nchini kwa kipindi cha miaka mitatu."

Source: MATUKIO-MICHUZI: VIETNAM KUPANUA WIGO WA UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA MAWASILIANO TANZANIA

Kwa wenye kujua vizuri huu mkataba, tusadidiane majibu ya haya maswali.
- serikali ina mpango gani kuhusu kuendelea kupatikana kwa huduma ambazo katika huu mkataba zinatolewa bure mpaka 2017?
- kwenye huu mkataba serikali imepata: huduma za mawasiliano za bure kwa miaka mitatu, upatikaji wa huduma za mawasiliano vijijini. Je serikali imewapa halotel nini?

Suala la mkataba linaweza likawa lipo sawa kabisa kwa makubaliano kwamba watoe huduma bure kwenye hizo asasi za serikali huku wakitoza gharama nafuu kwa watumiaji wengine kufidia gharama za ujenzi na huduma.

Lakini kuna kitukimoja ambacho sisi tunazidiwa hawa wawekezaji nikwamba kuna rasilimali wanazichukua kisiri sana kama madini hasa hasa ukizingatia kazi zao ni zakupitisha mikongo ardhini alafu utakuta katika miradi yao hii kuna camp zao wanaziweka porini ambapo sidhani kama kuna wadhibiti wanawafuatilia wanachofanya huko.

Ndio maana hata wanaposemea wanatoa huduma bure gharama zao wanakuwa wamezifidia. Katika dunia ya sasa hakuna bure. Wanatuibia sana hawa kwa kigezo cha uwekezaji.

Na pia ukiona mpaka raisi wao anakuja sio bure.
 
kumbe wanatulisha mbele,na kutula nyuma!
 
hilo la kuibiwa madini huko porini wanakoweka camp zao haliingii akilini kabisa.
ok chukulia wameiba hayo madini watayatoroshaje ikiwa airport kuna ulinzi wa kutosha ama wataweka mifukoni mwao...? halafu hiyo dhamira ya kuiba ni sera ya wavetnam na serikali yao nzima inapanga kuiba kama ndio sehemu ya faida ya kutusaidia na fidia ya gharama ya usaidizi wao kwetu..? mpaka Rais wao anakuja rasmi huku..
No hiyo sio kweli ingawa Bure ghali wao wanatafuta biashara kwetu kwa njia ya kutusaidia kwanza lakini mwishowe watafaidika kwa mahusiano mengine ya kibiashara kwa vile tutawapa upendeleo maalum kwa fursa zitakazojitokeza hapo baadaye..
huo msaada ni rushwa baridi kwa malengo ya kupewa upendeleo maalum
 
huo msaada ni rushwa baridi kwa malengo ya kupewa upendeleo maalum....
 
Naombeni mnieleweshe kama halotel wanatakiwa kufanya yote hayo TTCL kazi yao ni nn? Serikali haioni kama ni wakati muafaka wa ku-liquidate TTCl maana inaonekana haina umuhimu wowote tena.
 
Hii kitu haijaeleweka kabisa kwa wadau wa kitanzania. Ni kweli wanajitahidi kuingia ndani vijijini lkn kwenye hizo shule 3 @wilaya mbn halionekani? Na hata hivyo kuna vimaneno vingi vingi kwamba ni mtandao na kuna share za wakubwa tu.

Je, kweli IPO wapi?
 
Ukiw
hilo la kuibiwa madini huko porini wanakoweka camp zao haliingii akilini kabisa.
ok chukulia wameiba hayo madini watayatoroshaje ikiwa airport kuna ulinzi wa kutosha ama wataweka mifukoni mwao...? halafu hiyo dhamira ya kuiba ni sera ya wavetnam na serikali yao nzima inapanga kuiba kama ndio sehemu ya faida ya kutusaidia na fidia ya gharama ya usaidizi wao kwetu..? mpaka Rais wao anakuja rasmi huku..
No hiyo sio kweli ingawa Bure ghali wao wanatafuta biashara kwetu kwa njia ya kutusaidia kwanza lakini mwishowe watafaidika kwa mahusiano mengine ya kibiashara kwa vile tutawapa upendeleo maalum kwa fursa zitakazojitokeza hapo baadaye..
huo msaada ni rushwa baridi kwa malengo ya kupewa upendeleo maalum
Nashauri ukae kimya kuhusu kutorosha madini maana tangiapo yanayoroshwa pamoja na huo unaoitwa ulinzi. Sioni kwanini washindwe
 
Kikwete alituambia hao Viettel watagawa smartphone bure,kwa sisi waelewa tukajua hiyo ni mbinu ya muwekezaji kupata kibali hakuna kitu
 
Ukiw
Nashauri ukae kimya kuhusu kutorosha madini maana tangiapo yanayoroshwa pamoja na huo unaoitwa ulinzi. Sioni kwanini washindwe
Sio kama nakataa madini yanatoroshwa. ,uwezekano upo wa mtu mmoja mmoja kutorosha zikiwa mali zake mwenyewe njia anayoitumia si halali kisheria akikamatwa ina kula kwake na hasara ni yake mwenyewe.

Lakini sio kampuni au Nchi ipange kuiba madini baada ya kupewa kazi fulani hapa nchini halafu makampuni hayo yapange kuchimba madini kiwizi kisha wayatoroshe nje ya nchi. kama mchangiaji alivyochangaia maoni yake hapo juu

mtu binafsi anaweza kutumia njia zozote kutorosha madini hilo halina ubishi
 
Unapoongelea ulinzi wa upitishaji mizigo airport, naona umesahau kuwa mizigo ya vip haikaguliwi, na pia kumbuka tetezi zilizovuma juu ya meno ya tembo kwenye ndege ya rais wa china alipotembelea tanzania.
 
Nchi na Nchi kamwe haziingizani mkenge kwa sababu taratibu zote za kisheria hufuatwa katika kila jambo linalozikutanisha Nchi hizo na kila Nchi ina wataalam waliobobea katika kila nyanja.
Mathalan ujio wa Rais wa Vetnam haujazuka tu ghafla bali ni hitajio la msingi kwa Nchi zetu kuna faida nyingi kwa sasa na kwa vizazi vijavyo. mahusiano mazuri huzalisha fursa za ajira na kubadilishana ujuzi.

Kwa mfano wenzetu hulima mpunga mara tatu kwa mwaka na wamejitosheleza kwa mchele mpaka wanauza nje ziada
Mahusiano mazuri na wao yatatusaidia kupata ujuzi na sisi tuweze kujitosheleza kwa mchele mpaka kilo ya mchele iwe rahisi karibu na bure...
 
Suala la mkataba linaweza likawa lipo sawa kabisa kwa makubaliano kwamba watoe huduma bure kwenye hizo asasi za serikali huku wakitoza gharama nafuu kwa watumiaji wengine kufidia gharama za ujenzi na huduma.

Lakini kuna kitukimoja ambacho sisi tunazidiwa hawa wawekezaji nikwamba kuna rasilimali wanazichukua kisiri sana kama madini hasa hasa ukizingatia kazi zao ni zakupitisha mikongo ardhini alafu utakuta katika miradi yao hii kuna camp zao wanaziweka porini ambapo sidhani kama kuna wadhibiti wanawafuatilia wanachofanya huko.

Ndio maana hata wanaposemea wanatoa huduma bure gharama zao wanakuwa wamezifidia. Katika dunia ya sasa hakuna bure. Wanatuibia sana hawa kwa kigezo cha uwekezaji.

Na pia ukiona mpaka raisi wao anakuja sio bure.
Vietnam ni third world inayokua haraka kuliko Tanzania hata nchi nyingi za Afrika. Ina tumia fursa hii kupitia Tanzania kutangaza biashara yake ya mawasiliano kupitia Tanania na mengine yatafuata. Hakuna bure ya kweli bali huwa na ndoano
 
Back
Top Bottom