Mkataba mwingine kama wa Dowans huu hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkataba mwingine kama wa Dowans huu hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wikolo, Jul 31, 2011.

 1. w

  wikolo JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na Gerald Kitabu
  31st July 2011

  [​IMG] Ni ule mwekezaji aliyepewa ardhi kwa miaka 99
  [​IMG] Kodi ya ardhi sh. 200, Halmashauri kupata sh.500

  Wananchi, watendaji wa vijiji na Madiwani wa kata za Litapunga na Mishamo Wilayani Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, wamepinga yaliyokuwa makazi ya wakimbizi ya Mishamo na Katumba, kukodishwa kwa mwekezaji ambaye ni kampuni ya Agriosol ya Marekani, kwa maelezo kwamba uwekezaji huo, hautakuwa na tija kwa taifa.
  Makubaliano ya awali (ambayo NIPASHE inayo nakala yake), kati ya mwekezaji huyo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, yanaonyesha kwamba kampuni ya Agrisol itakodisha kwa miaka 99, eneo la Katumba hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800.
  Mwekezaji pia atalipa Sh. 200 kama kodi ya ardhi kwa ekari na Halmashauri itapata Sh. 500 kwa ekari, hata hivyo haijulikani malipo hayo yatalipwa kwa muda gani yaani kwa mwezi au kwa mwaka.
  Makubaliano hayo yanaonyesha pia kwamba iwapo kutatokea mgogoro, serikali itatumia busara kuutatua lakini ikishindikana, shauri hilo litasikilizwa jijini London, Uingereza na msuluhishi ambaye atakuwa Chemba ya Biashara ya Kimataifa (International Chamber of Commerce).
  Kadhalika, inaelezwa kwamba mwekezaji huyo ataajiri mameneja wa mashamba kutoka nje hususan Afrika Kusini na ataendesha kilimo cha mbegu za kimaabara.
  Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo Mawaziri na wale wa Halmashauri ya Mpanda, wamekuwa 'wakipigia debe' uwekezaji huo, kwa madai kwamba utaongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza ajira kwa Watanzania.

  WANANCHI
  Watendaji wa vijiji na Kata zinazozunguka maeneo hayo, wamepinga uwekezaji huo kwa maelezo kwamba hawajashirikishwa kikamilifu na hati hiyo haina maslahi kwa taifa.
  Wakizungumza na waandishi wa habari walioongozana na timu ya watafiti kutoka shirika la HakiArdhi kuhusiana na uwekezaji huo, viongozi hao na wananchi wameitaka serikali ijifunze kwa yaliyotokea kwa kampuni tata ya Dowans kwa kujifunga na mikataba mibovu, ya muda mrefu kwa bei chee.
  Mwekezaji pia anaitaka serikali ibadili sheria ili kuruhusu kilimo cha vinasaba (Genetically Modified Crops), ambacho kimsingi kinaua mbegu za asili na kudhoofisha ardhi.
  Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo, alisema madiwani wa kata zinazozunguka eneo hilo, hawakuwahi hakualikwa kwenye mikutano iliyopitisha makubaliano hayo tata wala kwenda kwenye ziara nchini Marekani.
  “Viongozi wa wilaya wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Wenyeviti wa kamati na Madiwani wa kutoka mbali na hapa kama vile Mpimbwe na Ulwila ndio waliokwenda Iowa- Marekani na waliporudi tu sisi tukawa tunaletewa maagizo bila kujua undani wake,” alisema.
  Msafara wa wajumbe kumi waliokwenda Iowa-Marekani uliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Salum Chima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Rajabu Rutenge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda, Philip Kalyalya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Silvester Nswima, Mkurugenzi wa Wilaya Eng. Emmanuel Kalobelo, Mjumbe wa kamati ya fedha Rose Mayaya, na Mjumbe wa Kamati ya maadili Teddy Nyambo.
  Wengine ni Mwanasheria wa Halmashauri Patrick Mwakyusa, Afisa Kilimo na Mifugo Fabian Kashindye, na Haruna Mwakitanile (cheo hakikuweza kupatikana mara moja).
  Alisema wajumbe hao waliporudi kutoka Marekani, wananchi walishangazwa na kitendo cha Serikali kutenga mipaka kwa ajili ya mwekezaji wakati vijiji hivyo havijawahi kupimwa.
  Ofisa Mtendaji wa kata ya Mishamo, Agustino wanga, alisema hawajawahi kuiona kampuni ya AgriSol wala wawakilishi wao ambao ni Agrisol Tanzania Limited, na kwamba wamekuwa wakiwasikia viongozi wakieleza kuwa makazi hayo ya wakimbizi yatakodishwa kwa Wamarekani kwa miaka 99.
  “Mimi binafsi nina mpango wa kuhama kabisa maana wakiondoka wakimbizi tu, huduma muhimu nazo zitakoma, hatuwezi kuwezana na mwekezaji ambaye hatumjui,” alisema.
  Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya ya wafugaji mkoani Rukwa, Masanja Katambi, alisema inashangaza kuona serikali inaingia mkataba usio na maslahi kwa taifa badala ya kuwapatia wafugaji maeneo hayo ambao wamekuwa wakigombea malisho na wakulima.
  “Kila siku wafugaji wanagombana na wakulima na mara nyingine kuuana, kwa sababu ardhi haitoshi katika mkoa wetu. Wafugaji hudiriki hata kuwahonga askari wa wanyamapori katika mbuga ya Katavi ili kuingiza mifugo yao kwa malipo maalumu, hili Serikali hailioni?” alisema.
  Mkuu wa Makazi ya Katumba na Mishamo, Athuman Igwe, alisema anachosubiri ni kutekeleza amri ya serikali pindi taratibu za uwekezaji zitakapokamilika.
  Hata hivyo, alisema wakimbizi walipaswa kuwa wameondoka kupisha uwekezaji lakini anashangaa kuona kuwa bado zoezi hilo halijakamilika mpaka hivi sasa.
  “Hili Zoezi la kuwahamisha wakimbizi linaratibiwa na Tamisemi, sisi tunasubiri utekelezaji tu,” alisema mkuu huyo ambae pia ni mratibu wa makazi ya Ulyahulu yaliyopo Kigoma.
  Alifafanua kwamba kikwazo ni wakimbizi ambao wanataka walipwe Sh. 19 milioni kila mmoja kama fedha za uhamisho badala ya Sh. 300,000 walizopangiwa.
  Mmoja wa wakimbizi, Andrea Helmashi, alisema Sh. 300,000 ni ndogo kwa kuwa wengine wanafamilia ya watu zaidi ya 10 na kupendekeza kwamba wangelipwa Sh. 13 milioni.
  SERIKALI INASEMAJE
  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Rajab Rutenge, alitetea uwekezaji huo akieleza kwamba ni wa faida kubwa kwa taifa na wakazi wa maeneo yanayozunguka makazi hayo kwani utaboresha upatikanaji wa chakula nchini.
  “Mimi ni mtalaamu wa masuala ya chakula na nchi yetu inakabiliwa na janga la njaa, ni lazima tushirikiane na kampuni ya Agrisol kumaliza tatizo hilo,” alisema.
  Kwa upande wake, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambaye ni mmoja wa waliotia saini makubaliano hayo, Patrick Mwakuysa, alisema kampuni hiyo ina lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula, masoko na kutengeneza ajira kwa Watanzania.
  CHANZO: GUARDIAN ON SUNDAY
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tutaishia kumalizana kama Rage alivyosema jana.
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ninachoona kwenye hii habari ni kuwa muandishi amekurupuka na kuweke upenzi (bias) badala ya kuijadili au kuiripoti kwa kuangalia pande 2 za coin. I suggest the writter to go back for clear reporting the issue.
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna siku mtaamka na kukuta ardhi yote wamekabidhiwa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji. Pamoja na kwamba tunahitaji mashamba makubwa, ni lazima kuwe na utaratibu wa partnership na wenyeji ili kunufaisha watazania na matumizi ya ardhi yao. Hakuna maana yoyote mmarekani kuja kulima mbegu za utafiti hapa hekari laki kadhaa na anondoka bila kodi kama wanavyovuna madini sasa hivi.

  Zimbabwe ilianza hivyo hivyo sasa wanatafuta uhuru upya. Kama wananchi wanaozunguka eneo hilo wako tayari kulitumia kwa nini wasipewe hata heka mbilimbili na wakazalisha kwa wingi wao? Hii engesaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na uhalifu wa vijana.
   
 5. T

  TAKELOVE Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  me hii hali nimeichoka sijui nyinyi wana jf wenzangu naanza ku mmiss sana mugabe
   
 6. s

  said kamwana Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaman haya mambo yapo na ndo kwanza mikataba kama hiyo inaendelea..mwekezaj anapewa miaka 10free..halip kod ukiuliza kwa nn kenya wanafanya hivyo tusipofanya cc wawekezaj watakwenda kenya duh!ndugu zangu wahenga walisema ukimuona mwenzako ananyolewa wewe tia maji..tumeona zimbabwe.
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mbona mapori yako mengi tu watu mmengangania mjini kulima hamtaki mkiona wazungu wamechukua mnaanza makelele mkiachiwa hata hamuendelezi acha wachukue
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  wewe unalima? ardhi ipo nyingi tu kulima hamtaki mmengangania mjini mapori yako kila mahali akichukua mzungu aendeleze ndo mnaona ni ardhi,acha walime watuokoe na baa la njaa mwe?
   
 9. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  nchi inanuka rushwa sana hii.
   
Loading...