Nenda youtube, mikasi zote ziko kule!
By the way, nilikiangalia kipindi, nimemkubali sana Masoud Masoud japo kuna maeneo natofautiana nae kwenye baadhi ya maeneo. Amebonda sana watangazaji wa kisasa, huku amesahau kuna watangazaji wapya pia ni vipaji!.
Amebonda sana vipindi vipya ikiwamo vile vipindi vya mipasho!.
Hata mimi kama mtangazaji wa zamani, Clouds Radio ilivyoanza, ilianza kwa kuokoteza vipaji mitaani, wasio na ujuzi wowote kitaaluma, mwanzo sikuliunga mkono hili, kwa sababu enzi hizo kuwa mtangazaji ilikuwa ni lazima upite RTD huko kwanza upikwe ndipo utangaze.
Clouds radio wanachofanya ni kuwapatia wasikilizaji kile wanachotaka!. Kati ya saa 4-7 mchana, wengi wa wasikilizaji ni wamama walioko nyumbani, hivyo wanamambo yao ndio kama kwenye kipindi cha Leo Tena!.
Kitu ambacho nimemkubali sana Masoud Masoud ni ule uwezo wake kuujua muziki, kwa undani, chimbuko na lengo la nyimbo mbalimbali!.
Pia simuungi mkono alipowalaumu wanawake wote kuwa "sio!" na kusema ameoa mara tatu, ana watoto nane, lakini sasa anaishi "alone" kwa vile wanawake wote "sio!". Yes ni kweli baadhi ya wanawake ni "sio" ila sio wote!, kuna wanawake wengi tuu "ndio!", ila ikitokea mtu ukakutana na bahati mbaya ya kila chaguo lako likatokea kuwa "sio!", haina maana wanawake wooote ni sio!.
Pasco.