Mkasa Wa Kweli: Damu Ya Mwanamwali Kitandani

Mkasa Wa Kweli: Damu Ya Mwanamwali Kitandani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,639
52602654_2323247914393236_200852371775946752_n.jpg


DAMU YA MWANAMWALI KITANDANI
MTUNZI: ALLY KATALAMBULA

UTANGULIZI

“MWANAUME kutokwa na machozi, iwe kwasababu ya maumivu au majonzi, si kitu kinachokubalika katika ukoo na kabila letu.
Ukiona mwanaume analia, ujue ana roho ya kike. Ukilia, huna sababu ya kuvaa kaptula ama suruali. Machozi ya mwanaume yanatakiwa kuwa adimu sana. Mwanaume kutokwa machozi ni udhaifu wa kiwango cha mwisho.”
Ni maneno ya marehemu baba yangu. Niliyakumbuka nikiwa katika madhila makubwa. Donge kavu lilikuwa limenikaba kooni. Uso wangu ulikuwa umesawijika kwa hasira iliyochanganyikana na simanzi kubwa.
Nilikuwa nimejiinamia mkono ukiwa shavuni. Maungo ya mwili wangu yalikuwa yakivuja jasho kama mgonjwa wa homa kali. Macho yalikuwa mekundu kama yaliyoingiliwa na pilipili. Kila wakati nilikuwa nikitoa msonyo mdogo, huku nafsi yangu ikijilaumu ndani kwa ndani.
Kwa mara nyingine, nilinyakua simu yangu ya mkononi iliyokuwa kando na kupiga namba fulani.
Namba niliyokuwa naipiga, nilikwishaipiga kabla zaidi ya mara kumi na moja bila mafanikio. Simu ilipokuwa sikioni, mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakinienda kasi kuliko kawaida. Japokuwa haikuwa mara yakwanza kuipiga simu ile, ila safari hii nilikuwa na presha kubwa.
Baada ya muda fulani kupita, majibu kupitia sipka za simu hiyo nikayapata:
“…namba ya simu ya mteja unayempigia haipatikani kwa sasa...”
Nilikata simu bila kusikiliza maneno yote punde baada ya kupokea ujumbe ule.
Donge kavu likaendelea kunikaba kooni, wivu na hasira vikaendelea kutanda moyoni mwangu, kwa mara nyingine nilijikuta nikisaliti ujasiri niliofundwa na baba yangu. Machozi yakanibubujika tena!
“Kwa nini unanifanyia hivi Nasra? Kwanini? Iweje jambo hili lifanywe na wewe? Haya ndiyo malipo ya pendo langu? Kosa langu ni kukupenda si ndivyo? Nini maana yake hii sasa? Eeh!!..” nilinong’ona kwa sauti iliyojaa mfadhaiko huku machozi yakijikusanya machoni.
Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi, ilikuwa ni saa sita na nusu usiku, nilichukua pakiti ya sigara na kutoa mche mmoja na kuupachika mdomoni, nikawasha kwa kiberiti cha gesi ambacho kilitoa mlipuko mdogo wa moto, nikaunguza ile sehemu mbele ya sigara.
Nikavuta kwa mkupuo mmoja na kutoa moshi mwingi kupitia tundu za pua na mdomo.
Nafsi yangu ilikiri wazi kuwa mke wangu Nasra hakuwa mtu sahihi kwangu, hakuwa na sifa hata moja ya kuwa mke nimtakaye, mke niliyekuwa nikimwota usiku na mchana, lakini moyo wangu ulinionya kutofanya kitendo chochote kitakachopelekea kuwa mbali na kiumbe yule.
Haja ya moyo wangu ikazidi nguvu mtazamo wa utashi wangu. hali hiyo ikanifanya nizidi kuangamia nafsini.Nikawa mtu wa kujilaumu.
Ndiyo. pamoja na mgogoro wa ndani kwa ndani uliokuwa ukinivuruga hata afya ya mwili wangu bado nafsi yangu ilijiapiza kufa Kijerumani na tai shingoni!!!!.

SURA YA KWANZA

Jina langu halisi naitwa Faraji Hussein Mpangalala, ni mzaliwa wa Kigoma katika Kijiji cha Nguruka, japo kwa sasa naishi katika Jiji la Dar Es Salam. Ni mtoto mwisho kati ya watatu kutoka kwa mzee Mpangalala, mbele yangu wakiwa ni dada zangu wawili Halima na Shadia.
Dada zangu hao, wote walikwishaolewa miaka mingi iliyopita, baada tu ya kumaliza kidato cha nne na kupata matokeo ambayo hayakuwawezesha kuendelea na masomo.
Naweza nikasema, katika familia yetu, ni mimi pekee ambaye wazazi wangu walikuwa na matumaini makubwa ya kuja kuwa kiongozi wa familia siku za usoni. Hii ni kutokana na kwamba, kwanza nilikuwa mtoto wa kiume lakini pia nilikuwa ndiye mtu msomi kuliko mwingine yeyote.
Nikiwa na umri wa miaka 27 baada ya kumaliza shahada yangu ya kwanza ya ualimu pale Mlimani, niliajiriwa ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Jiji Dar, kama mratibu wa elimu wa manispaa hiyo.
Mwaka 2004 rasmi niliyaanza maisha ya kujitegemea, nikiwa kijana mwenye ndoto kubwa za mafanikio mbele yangu, mshahara mzuri pamoja na malupulupu ya hapa na pale yaliniweka katika daraja la juu sana kimaisha, kimsingi nilishi maisha ambayo kijana yeyote anayaota na angapenda awe nayo.
Ni katika kipindi hicho, ndipo nilipoanza kupata shinikizo kubwa kutoka kwa wazazi wangu, ni kuhusu ndoa. Kuoa.
Ni kweli, kwangu mimi wakati huo, ulikuwa ni wakati sahihi kabisa kuoa, hasa ukizingatia nilikuwa na kipato kikubwa, tena cha uhakika. Hata hivyo, tatizo lilikuwa ni moja tu. Sikumwona mwanamke sahihi wa kuwa mke wangu.
Siyo kwamba katika Jiji la Dar nilikuwa sikutani na warembo. Laa!!. Warembo niliwaona utitiri ila wengi wao walikuwa viruka njia. Ndiyo. Baadhi ya wanawake wengi wa mjini wanahitaji mwanaume wa kariba yangu.
Si labda kwakuwa nilikuwa mwanaume mwenye mvuto, Laa! Isipokuwa nilikuwa kijana mwenye fedha na mafanikio makubwa maishani.
Baadhi ya wanawake wa Dar Es Salam kwao fedha ni zaidi ya upendo, hivyo sikupenda kabisa kuoa mwanamke ndani ya jiji hilo ambaye nitamweka ndani huku nikijua mwanamke huyo kapenda fedha na mali zangu.
Kwangu mimi, urembo ilikuwa ni sifa ya pili baada ya uchamungu, heshima, upendo na uvumilivu.
“Mwanangu kama tatizo ni hilo, tupe ruksa sisi tukutafutie mwanamke wa kuoa huku kijijini,” siku moja mama yangu alinieleza, ilikuwa ni baada ya kumpa sababu za kwanini nachelewa kuoa.
“Siyo jambo baya na wala siyo jambo zuri.”
“Kwa nini unasema hivyo baba?”mama aliniuliza.
“Ni jambo zuri kama mwanamke mtakayenichagulia ndiye wife material nimtakaye, na ni jambo baya kama mkinichagulia mwanamke ambaye hatokuwa na sifa nizitakazo.”
“Naamini mimi na baba yako hatuwezi kukuangusha mwanangu Faraji. Chombo nitakachokutafutia utakipenda,” mama aliniambia.
Nawaamini mno wazazi wangu, Sikuwa na pingamizi juu ya ombi hilo, niliwakubalia kwa roho moja wanitafutie mke.
Hazikuzidi wiki mbili, nilipigiwa simu na baba yangu akanieleza kuwa wamekwishampata mchumba na kilichokuwa kimebakia ni kumposa, kulipa mahari, kisha ndoa.
“Jina lake?” niliuliza kwa kiherehere
“Anaitwa Nasra Mfaume.”
“Kabila gani?”
“Unauliza kabila, unataka kutambika mwanangu?” baba yangu alinitania.
“Napenda kujua tu.”
“Hana kabila lakini nadhani ni sahihi kukwambia ni Africast, mchanganyiko wa Kiajemi na Kibantu, mababu zake ambao asili yao walitokea nchini Yemen na kuishi kisiwani Pemba, lakini baada ya kulowea huku na kuzaliana na Waswahili wamekuwa ni hukuhuku kwetu,” baba alinieleza.
Nilishusha pumzi fupi huku taswira ya machotara wa Kipemba ikijengeka kichwani mwangu.
“Atakuwa bomba huyo mchumba. Niliwaza kimoyomoyo simu ikiwa bado sikioni.
“Kwa hiyo mipango iliyobakia ni kulipa mahali kisha ndoa tu mwanangu,” baba akaendelea kuongea zaidi kwenye simu.
“Unaweza kunitumia picha yake huyo mrembo?”
“Nakutumiaje?”
“Kwa njia ya mtandao?”
“Bila shaka mwanangu.”
“Basi nitumie picha yake huyo mchumba sasa hivi,”nilisema nikiwa na wahaka wa kumwona huyo mwanamke wa Kipemba.

Je, nini kitaendelea?

KITABU KIPO MTAANI NICHEKI KWA 0687750295
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya Lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij @addenbwii ONTARIO Kobe The Vein mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny @Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi @Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA
 
DAMU YA MWANAMWALI KITANDANI

NA: ALLY KATALAMBULA

SEHEMU YA 2

ILIPOISHIA…
“Unaweza kunitumia picha yake huyo mrembo?”
“Nakutumiaje?”
“Kwa njia ya mtandao?”
“Bila shaka mwanangu.”
“Basi nitumie picha yake huyo mchumba sasa hivi,”nilisema nikiwa na wahaka wa kumwona huyo mwanamke wa Kipemba.

SONGA NAYO…

Nilitumiwa picha ya huyo mchumba kwa njia ya mtandao. Haraka nilifungua e-mail nikaipakua picha huku shauku ikiwa kubwa.
Muda mfupi badaye, nilikuwa nikitizama picha ya mwanamwali mrembo. Tabasamu pana lilinitoka huku nikiendelea kusaili mwonekano wa kiumbe yule.
Alikuwa ni msichana wa kati ya miaka 20 ama 22. Alikuwa kigori, chotara aliyeumbwa akaumbika, katika ile picha, alikuwa kwenye mavazi ya heshima huku uso wake ukionesha kama mtu asiye na hatia yoyote maishani.
Nafsi yangu ilikiri nilikuwa natarajia kuwa na mke mrembo sana siku za usoni. Kwa mara nyingine, nilijisikia furaha kwa kuwa mvulana mwenye mika 27 tu, ambaye nilikuwa nakaribia kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha yangu.
Siku chache baadaye, posa ililipwa, kisha mahari ikafuata, haraka sana mipango ya ndoa ikaanza kufanyika, kwa kuwa nilikuwa bize sana na masuala ya kazi, niliwachia wazazi wangu pamoja na ndugu kuendelea na mchakato wote wa ndoa huku mimi nikingojea tu kuletewa mke.
Hatimaye siku iliwadia. Ndoa ikafungwa Kigoma huku mimi nikiwakilishwa na binamu yangu aitwaye Mrisho.
“Unatakiwa kumpokea mkeo stesheni,” nilijulishwa baada ya mambo yote kukamilika.
“Wanakuja kwa treni?”
“Ndiyo.”
“Wanakuja wangapi?”
“Wapo watatu. Mkeo Nasra, mjomba wako Majeed na mdogo wake na mkeo aitwaye Aisha.”
“Kwanini msingesema niwatumie tiketi za ndege, usafiri wa treni ni tabu sana siku hizi…”
“Unahamu na mkeo baba. Eeeh!” mama akaniuliza kwa utani.
“Sana mama, ninahamu na mke wangu.”
“Basi usijali, keshokutwa nenda ukampokee stesheni,” mama alisema kisha akanipa usia mfupi wa namna nzuri ya kuishi na mke wangu.

Siku ya Ijumaa saa saa kumi na mbili jioni, nilikuwa Posta eneo la stesheni nikingoja ugeni kutoka Kigoma. Moyo wangu ulikuwa ukinidunda huku viganja vya mikono vikilowa jasho, sikujua kama hali hiyo ilitokana na hamu ya kuhitaji kumwona msichana yule Chotara ama laa!.
Nusu saa baadaye, treni iliwasili, nikajiondoa katika gari langu nililokuwa nimelipaki katika Kituo cha Daladala cha Stesheni na kusogea eneo la kutokea abiria katika jengo la stesheni, macho yangu yalipepesa kwa kila abiria aliyetoka.
Nilisimama pale getini kwa muda mrefu hadi abiria wakaanza kupungua lakini sikuwaona wageni wangu.
“Watakuwa wapi?” nilijiuliza mkono mmoja ukiwa mfukoni huku mwingine nikiwa nimekamata lundo la funguo nililokuwa nikilitingishatigisha.
“Faraji,” mara sauti moja iliniita nyuma yangu.
Niligeuka haraka.
Macho yangu yakakutana na watu watatu wakinitazama huku vinywa vyo vikiwa katika tabasamu pana.
“Wooh jamani ni ninyi!” nilisema kwa uchangamfu huku nikiwapokea mizigo wageni wale niliokuwa nikiwangojea.
“Karibuni sana jamani.”
“Ahsante Faraji za hapa?” mjomba Majeed, aliitikia kwa uchangamfu sana.
“Hapa ni kwema, poleni na safari.”
“Tumekwishapoa shemeji,” msichana mdogo aliyekuwa karibu na msichana mrembo na mtulivu alidakia kwa kiherehere huku uso wake ukiwa umesawijika kwa furaha kubwa.
“Lo! We naye kwa umbeyahumo!Umejuaje kama huyu ndiye shemejio?”
Mjomba Majeed akamuliza kwa sauti yenye kusuta, ila katika hali ya maskhara.
“Mke ataachaje kujua chake,” binti yule mdogo akajibu kwa utani. Wote tukacheka.
“Huyu ndiye mkeo anaitwa Nasra Mfaume, na huyu chaumbea ni mdogo wake, anaitwa Aisha…” mjomba Majeed alianza kutoa utambulisho. Kule kumuita msichana mdogo chakaramu kuwa ni chaumbea, sote tukacheka.
“Nasra,” mjomba aliita baada ya kicheko.
“Abee mjomba,” binti mrembo, mtulivu akaitika kwa heshima.
“Huyu ndiye mumeo, Faraji Hussein Mpangalala.”
Mrembo yule alinikata jicho la wiziwizi kisha akanisalimia huku akinipa mkono.
“Asalam aleykum,” sauti laini kama iliyochujwa kwenye kifaa maalumu cha kuchujia sauti ikasikika, ikapenya kwenye ubongo na kuvuruga kabisa mwenendo ufanyaji kazi wa moyo wangu. Sekunde tatunne zikapita tangu salamu itoke, hatimaye nikaitikia.
“Waleykum salama bibie, hujambo?”
Nilimjibu huku nikiupokea ule mkono wake.
Picha ambayo nilitumiwa na baba yangu, haikuongopa hata kidogo. Urembo wa mke wangu ulikuwa vilevile kama wa kwenye picha.
Hata hivyo, baada ya kumtazama kwa makini zaidi nilibaini kuwa alikuwa na ziada moja juu ya urembo wake. Si kwa ile ngozi yake nyeupe, maana ile Ilikuwa ni ngozi ya kawaida ingawa ilimfanya imeremete na kushawishi kuigusa.
Wala si lile tabasamu lake la mara kwa mara. Maana hilo pia ni jambo la kawaida katika nyuso za wasichana wa kisasa na lingeweza kununuliwa kwa fedha tu iwapo mwenyewe angejali kujiunga na chuo kimojawapo cha usanii na kuhitimu.
Hali kadhalika, ziada hii haikutokana na macho yake maangavu, pua yake iliyochongoka, wala meno yake meupe yaliyojipanga kikamilifu kinywani mwake kama mistari miwili ya punje za mahindi kwenye kibunzi.
Alikuwa na ziada!
Lakini ziada hii ilikuwa ipi? nilijiuliza nikimtazama kwa hila Nasra Mfaume huku mkono nikiwa bado nimeukamata.
Nilimtekenya kwa siri kwenye kiganja chake nilichokuwa bado nimeking’anga’nia, tendo lile likamfanya anitazame, macho yetu yakagongana. Alishindwa kabisa kuhimili walau kwa sekunde mbili, alitazama chini lile tabasamu lake likigeuka kuwa katika sura nyingine.
Ni hapo nilipobaini ile ziada iliyonivuta katika sura na umbile la msichana huyu.
Aibu!
Alikuwa msichana mwenye aibu! Mmoja kati ya wasichana wachache kabisa duniani waliobakia na aibu. Wengi wao, toka waliposombwa na jinamizi llitwalo ‘utandawazi,mdudu wa ‘aibu ’ alitoroka zama za kale katika maumbile yao na hivyo kuwaacha wakavu kama wanaume.
Sifa zake hizo zikiwa zimepambwa kwa mavazi yenye heshima, sketi ndefu iliyovuka magoti na blauzi nyepesi iliyokifanya kifua chake kilichotoa picha ya uhai wa matiti yake.
“Si…si..sija..sijambo,” alinijibu kwa kubabaika huku aibu yake ikiongezeka maradufu.
“Karibuni sana,” nilisema huku nikiachia tabasamu. Nikajilamba midomo, nikameza funda la mate, kisha nikawataka tuelekee kwenye gari langu na safari ya kuelekea Kinondoni Studio ikaanza.
Lisaa limoja badaye, tuliwasili nyumbani kwangu, katika nyumba yangu kubwa ya kifahari, wageni wangu niliwapatia chumba kila mmoja na chake, ambapo niliwataka waoge na kubadilisha nguo ili kuchangamsha miili yao kabla ya kurudi mezani na kupata chakula cha usiku.
Mke wangu Nasra nilimwongoza hadi chumbani mwetu ambako pia nilimtaka aoge kabla ya kuungana na mjomba Majeed pamoja na shemeji Asha katika meza ya chakula.
“Faraji...” aliniita kwa sauti ya chini, uso wake ukionekana kuwa na jambo analotaka kunieleza.

TUKUTANE
 
DAMU YA MWANAMWALI:
MWANDISHI: ALLY .A. KATALAMBULA
SIMU: 0687 750295
SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA…

“Faraji...” aliniita kwa sauti ya chini, uso wake ukionekana kuwa na jambo analotaka kunieleza.

SONGA NAYO…

“Unasemaje mke wangu?”
Akanitazama kisha akasema:
“Nataka kuvua nguo.”
“Eeh, sawa vua tu.”
“Unaweza kunipisha kidogo?” mke wangu aliniambia huku uso wake ukionekana kujawa na haya.
Nilibaki nimeduwaa huku nikiwa sina jibu la kumpa, kwa mara nyingine nikabaini nilikuwa na mwanamke mwenye aibu nyingi.
Ingawa awali nilivutiwa mno na hilo, lakini sikutaka tabia ya aibu kwa mke wangu ipite kiasi, kama ilivyokuwa wasaa ule.
“Unanionea aibu?”nikamuuliza kwa sauti ya upole ilihali nikitambua hilo halikuwa swali bali jibu.
Alitikisa kichwa kukubali kwamba alikuwa akijisikia haya kuvua nguo mbele yangu.
“Utanionea aibu hadi lini mke wangu….”nilisema huku nikimsogelea karibu.
“Huna sababu ya kuwa na aibu tena, hasa unapokuwa mbele yangu, mimi ni mumeo sasa. Upo kwenye maisha mapya, maisha ya kuwa kama ulivyozaliwa ukiwa ndani ya chumba hiki. Maisha ya kuchezewa mwili wako vile nitakavyojisikia. Maisha yako yote. Tegemea hayo kuanzia sasa,” nilizungumza nikiwa nimesimama sentimita chache mbele yake. Wazungu wanasema ‘ziro distance’
Nasra alibaki ameinamisha kichwa chini, mikono akiwa ameikusanya pamoja na kusuguasugua viganja vyake.
Nilimtizama kiumbe yule kwa chati, nikaona uso wa mtu mshamba katika ulingo wa mapenzi, nikaendelea kujiuliza, Je? mrembo yule alikuwa bado mwanamwali, ambaye hajawahi kuguswa na mwanaume yeyote tangu azaliwe?
Kama ndivyo, basi nitakuwa nimelamba dume. Nitakuwa nimepewa zawadi nzuri mno na wazee wangu. Nilijiwazia kimoyomoyo.
Nilipenyeza mikono kwa hila na kushika kiuno chake, akashituka kwa woga, hata hivyo hakuondoa mikono yangu! nikakipapasa kiuno chake chembamba, kiuno kilichoning’iniza makalio makubwa na mapaja yaliyonona, nikawa namwangalia chotara yule usoni huku nkitembeza viganja vyangu kwenye mzunguko wa kiuno chake.
Nasra alifumba macho yake, midomo yake akiwa ameiuma, aibu ilikuwa imemtawala.
“Ngoja nikakoge,” akasema kwa kunong’ona.
“Kuoga na nguo?”
“Nitavua.”
“Acha nikuvue.”
“Nitavua mwenyewe.”
Alikwishachelewa. Tayari nilikuwa nimekwishafungua zipu ya sketi yake na kuivuta chini kwa nguvu.
“Ayaaaa!!!” alibweka kwa fadhaa baada ya kubaki na kinguo cha ndani peke yake. Nacho nikakishika kwa hila na kukiondoa mara moja..
“Aaagh!...Aagh!!! Oooii!!... Jamani Faraji…”alinung’unika.
Alikuwa amepandisha mguu mmoja kwa mwingine huku mkono wake mmoja ukiwa umeziba nyeti zake wakati ule wa pili akiwa amejiziba usoni kutoana na haya. Akawa kama samaki aliyetolewa kwenye maji.
Ile blauzi nyepesi aliyokuwa amevaa na kufanya kifua chake kitoe picha ya uhai wa matiti yake nayo nikaichojoa mauongoni. Hatimaye nilikuwa nikimtizama mwanamke mrembo akiwa kama alivyozaliwa! Ndani ya chumba changu mwenyewe.
Nilianza kuhisi hali isiyo ya kawaida mwillini mwangu, mapigo ya moyo yakawa yanaenda kasi, kitendo cha kuona maumbile ya mke wangu kwa kweli ilisababisha nipatwe na msukumo wa fulani usioelezeka.
Nikawaza: Nimvuruge humu ndani ama nimweke kiporo?
Hata hivyo, nikajionya kutokuwa na pupa yeyote kwa kuwa tayari samaki yule yupo ndani ya bwawa langu, hivyo nikaona ni vema nimalizane na wageni wangu ambao hadi wasaa ule niliamini wangekuwa mezani wakitungoja ili tujumuike pamoja katika chakula cha usiku. Kabla ya kumrudia mwanamwali yule na kumchakaza kwa mapigo ya ki-Jack chan
Nilifyatua taulo langu na kumfunika.
“Nenda basi ukaoge mpenzi,” nilimnong’oneza huku nikimsindikiza na mabusu motomoto.
Muda mfupi badaye watu wote tulikuwa mezani tukipata chakula cha usiku. Mazungumzo ya hapa na pale yaliendelea pale mezani.
Baada ya chakula, mke wangu pamoja na mdogo wake waliondoa vyombo mezani huku mimi na mjomba Majeed tukiendelea na mazungumzo
“Uliwasiliana na mama yako?” mjomba Majeed aliniuliza.
“Nilisahau kabisa, ila nitampigia kabla sijalala.”
“Alinipigia kujua kama tumefika na amelalamika kwa nini hujamjulisha kama wageni wako wamefika.”
“Mama naye anamaindi’ mambo madogo, nitamcheki,”nilisema. Nikatoa simu na kumpigia.
Nilimtaka radhi mama kwa kutokumwalifu juu ya kuwasili salama kwa wageni wangu, nikamhakikishia kuwa wote walifika salama na wanakaribia kuwa wenyeji.
“Usijali mwanangu Faraji, najua ni kutokana na shauku ya mke ndiyo maana ulisahau,” mama alizungumza kwenye simu.
“Ni kweli kabisa mama, na nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunichagulia kifaa,” nilimwambia, nikasikia anaguna, mguno ambao ndani yake ulibeba kitu fulani kilichojificha. Akasema:
“Pongezi zote anastahili baba yako, maana yeye ndiye aliyempendekeza.”
“Kwani wewe hakuwa pendekezo lako?”
Tayari simu ilikuwa imekwishakatwa.

Toba.

SURA YA PILI

KAULI ya mama yangu ilinifikirisha kidogo, hata hivyo, nikaipuuza.
Tukaendelea na maongezi na mjomba Majeed.
Muda wote wakati tunaendelea na maongezi, mke wangu Nasra na nduguye Asha walikuwa wakiendelea na shughuli za hapa na pale.
Lisaa limoja badaye, shemeji yangu Asha alikuja kutuaga kuwa anajisikia usingizi hivyo anakwenda kupumzika.
Mimi na mjomba tukaendelea na mazungumzo, nusu saa baadaye mjomba naye akahitaji kupumzika.
Tuliagana kisha naye akaelekea chumbani mwake, sikuwa na cha kusubiri pale sebuleni, nikajinyanyua na kwenda bwawani kwangu ili kumvua samaki wangu.
Nilipoingia tu chumbani, macho yangu yalitua kwa kiumbe aliyekuwa amejilaza kitandani huku akiwa amevalia ‘night dress’ nyepesi iliyoacha maungo yake yaharibu kabisa mfumo thabiti wa upumuaji wangu.
Alikuwa amezikusanya nywele zake ndefu na kuzifunga pamoja kwa kijibanio kidogo huku akiacha kamkia kadogo kuning’inia.
Sura nzuri ya kuvutia, iliniita. Kifua kilichobeba matiti mazuri, kilinisisimua na umbo lake la kuchora, lilinihamasisha.
Nilimsogelea pale kitandani huku nikiwa na nia moja tu. Kufanya mapenzi na mke wangu. Lilikuwa ni hitaji langu kubwa wasaa ule. Alikuwa amejilaza kifudifudi ile ‘night dress’ aliyokuwa ameivaa ilikuwa ikitoa picha ya makalio yake yaliyokuwa yameumuka kama kichuguu.

Alipobaini kwamba nipo mbele yake, alijigeuza na kujikunyata kiubavu. Aibu ya kisichana ikawa inajitengeneza usoni mwake.
“Hujalala?” nilimsemesha.
“Bado. umeingia humu ndani saa ngapi?” akaniuliza huku akiuma vidole.
“Muda tu.”
“Safari ya treni ilinichochosha sana.”
“Pole.”
“Ahsante, usingizi ulikuwa umenichukua.”
“Pole mpenzi.” nilimwambia.
Nikawa nasaula nguo hadi nikawa mtupu, nikapanda kitandani, kisha nikajilaza kando yake.
“Huzimi taa?” Nasra aliniuliza kwa sauti ya chini.
“Unataka tufanye gizani?”na mimi nikamuuliza.
“Sina maana hiyo Faraji?”
“Kumbe?”
“Siwezi kulala taa ikiwa inawaka,”mke wangu alisema, nikaendelea kumuona kama mgonjwa anayesumbuliwa na kirusi kiitwacho aibu.
“Mke wangu.”
“Abee.”
“Usiniogope,” nilimwambia.
Hakunijibu.
Nilishika waya wa swichi uliokuwa uking’inia kutokea darini, nikazima balbu yenye mwanga mkali na kuwasha ile yenye mwanga hafifu wa rangi ya njano.
Nilipoyarejesha macho kwa mke wangu, nilimwona mithili ya malaika, kwa namna alivyokuwa akimeremeta katika mwanga wa rangi ya njano.
Mapigo ya moyo yalinienda kasi, nilishika kiuno chake nikawa natembeza kiganja changu polepole kwenye mzunguko wa kiuno..
Nikamvutia kwangu kidogo, hapo vifua vyetu vikagusana, ncha ya chuchu za matiti yake zilipochoma kufuani mwangu, ilikuwa ni kama vile nimepigwa na shoti ya umeme. Nilipatwa na misisimko isiyoandikika humu.
Joto la mwili wake likaongeza hisia za ajabu, wakati vidole vyangu vikihamia katikati ya mfereji wa uti wa mgongo na kutambaa kutokea juu hadi kwenye makalio ya chotara yule. Alishindwa kabisa kuizuia sauti isimtoke. Aliweweseka kama anataka kufa.
Sikukoma.
Vidole vyangu vikiwa vinafanya ziara pande zote za mwili wake, mdomo wangu niliusogeza kwenye matiti yake. Kisha nikawa nazimung’unya zile chuchu kama pipi kijiti.
Lilizuka balaa!.
Nasra alikuwa akipiga kelele za ajabu sana. Ukubwa wa mayowe yale ya mahaba, niliona yangeweza kumshitua mjomba Majeed na shemeji Aisha ambao muda ule kila mmoja alikuwa chumbani mwake anakoroma.
Nilichofanya ni kufungulia redio sauti ya juu, ili sauti ya redio angalau ilimeza ukelele wa mke wangu, Nasra Mfaume.
“ Ngoja…Ngoja…Ngoja kidogo,” Nasra alinisihi baada ya kuwa nimerudi kuendelea pale nilipoishia.
“Kuna siri ningependa nikueleze,” aliniambia
 
DAMU YA MWANAMWALI KITANDANI
MWANDISHI: ALLY KATALAMBULA
SEHEMU YA NNE
Simu: 0687750295

ILIPOISHIA

Nilichofanya ni kufungulia redio sauti ya juu, ili sauti ya redio angalau ilimeza ukelele wa mke wangu, Nasra Mfaume.
“ Ngoja…Ngoja…Ngoja kidogo,” Nasra alinisihi baada ya kuwa nimerudi kuendelea pale nilipoishia.
“Kuna siri moja ningependa kukueleza,”aliniambia

SEREREKA NAYO.

“Siri gani bibie?”
“Mwenzio sijawahi kufanya huu mchezo.”
“Acha maskhara.”
“Haki ya Mungu.”
“Tangu uzaliwe?”
“Ndiyo.”
“Kwa hiyo wewe ni mwanamwali…Bikira?”
“Kabisa.”
“Kama ni kweli nitakupenda maradufu,” nilimwambia huku nikimwangalia kama vile ndiyo kwanza namtia machoni. Uso wake ulikuwa kwenye woga. Ndita zilikuwa zimejitengeza usoni mwake kama mkeka wa kizaramo.
“Kwahiyo unasemaje?” nikamuuliza.
“Naogopa…Utaniumiza!!!”
“Huwezi kuumia.”
“Kivipi?’
“Kwani unamiaka mingapi?”
“Ishirini na mbili tu.”
“Basi huwezi kuumia. Ushakuwa mkubwa, siwezi kukuumiza.”
“Na ukiniumiza Je?”
“Ning’ate meno.”
Alitabasamu na mimi nikatabasamu. Nikamsogeza karibu yangu, nikampelekea kinywa changu kisha tukaanza kunyonyana. Mchuano ukaanza upya. Nilimwandaa kiasi cha haja. Sikupenda kabisa kumwachia maumivu hasa ukizingatia siku ile ilikuwa ni mara ya kwanza kufanya tendo la ndoa maishani mwake.
Kwa kweli ndugu msomaji, usiku huo ni siku ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu, penzi nililolipata kwa mke wangu ambaye mimi nilikuwa ndiye mwanaume wake wa kwanza, lilikuwa ni penzi tamu lenye msisimko pengine kuliko penzi nililowahi kupewa na mpumbavu yeyote maishani mwangu.
***
Asubuhi kulipokucha, mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuamka, nilishitushwa na mionzi hafifu ya jua la asubuhi ambalo huwa mara nyingi linapenya chumbani kwangu kupitia dirishani.
Pembeni yangu, mke wangu alikuwa bado akikoroma, saa ya ukutani ilionyesha ilikuwa saa mbili asubuhi, nilipiga miayo ya kivivu, nikajiondoa kitandani.
Nilikuwa mtupu, taswira ya penzi la mwanamwali lilikuwa likijitengeneza upya akilini mwangu. Nilitabasamu na kujiona kidume mwenye bahati kubwa maishani.
Kuwa na mke ambaye hajawahi kuguswa na mwanaume ni ushindi mkubwa kwenye dunia ya leo.
Nilisogea kwenye kioo cha kujiangalizia na kusimama wima, nikaona ukoko wa damu ya Mwanamwali iliyogandana kwenye nyeti zangu, nikatabasamu tena huku moyo wangu ukiwa wenye faraja.
Nilipoyarudisha macho kitandani, Mwanamwali alikuwa bado akiuchapa usingizi, uso wake uliendelea kuyaburudisha macho yangu.
Niliyatembeza macho pale kitandani lakini sikuwa nimeona kitu kingine nilichotarajia kukiona, nikasogea karibu zaidi. Naam! Hapo nikaona nilichokuwa nimekusudia kukiangalia.
Damu ilikuwa imetapakaa kwenye mashuka meupe, nikajipongeza kimoyomoyo kwa kazi nzuri niliyoifanya usiku wa kuamkia siku hiyo.
Kazi ya kufungua bikira ya mwanamwali.

****

Maisha yangu na mke wangu, yalikuwa ni ya furaha, tulipendana na nilimwamini mno. Kama walivyo wanawake wengine wa Kipemba, Nasra alikuwa ni mwanamke mpole, msikivu zaidi alikuwa mchamungu.
Kwa miezi kadhaa angalau hata ile aibu ilipungua. Kwa kweli alikuwa na kila kitu ambacho mwanaume yeyote angetaka mkewe awenacho. Wazungu wanasema ‘Wife material’
Mjomba Majeed alikwisharejea kijijini. Katika mji wangu tulikuwa tumebakia watatu, yaani mimi mwenyewe, mke wangu, pamoja shemeji yangu Aisha, yule binti chakaramu, ndugu wa mke wangu.
Hatimaye mwaka ulikatika, nikiwa naishi na mke wangu kwa upendo na furaha kubwa. Pale mtaani sikuwahi kusikia jambo lolote baya kumuhusu.

Jioni moja, baada ya kurudi kutoka kazini, kama kawaida yangu huwa napenda kujituliza nyumbani kwa ajili ya kufuatilia taarifa ya habari katika vituo mbalimbali vya runinga.
Siku hiyo mke wangu na nduguye walikuwa wakiendelea na matayarisho ya chakula cha usiku.
Nikiwa pale sebuleni na rimoti mkononi, nikiwa nahamisha stesheni moja hadi nyingine, mara simu ya mke wangu ilianza kuita. Iliita muda mrefu hadi ikakatika.
Sikuijali.
Ikaita tena hadi ikakatika.
Sikuijali tena.
Simu ikaita na kuita. Mke wangu alikuwa mbali nayo, sikuthubutu kuipokea. Ikaendelea kuita hadi ikawa kero.
“Kwa nini asikae na simu yake huko,” nilinong’ona.
Sikuwa na mazoea ya kupokea simu zake, niliweka utaratibu huo ili kila mmoja awe huru, asijione kubanwa. Na kwa kuwa nilikuwa nina imani kubwa dhidi yake, sikuona haja ya kumchunga chunga. Hakushika simu yangu sikugusa yake.
Ila siku hiyo kwa kuwa mke wangu alikuwa mbali nayo na muito wa simu ulikuwa ukioniondolea utulivu wa kutazima taarifa ya habari, niliichukua ile simu ili niiweke ‘silence’
Wakati nafanya zoezi lile punde ujumbe wa maneno ukaingia, na katika kubofyabofya nikajikuta nimefungua ujumbe huo kwa bahati mbaya.

Ujumbe ulikuwa umetumwa na namba ileile ambayo ilikuwa ikipimgia mke wangu muda mfupi uliopita.
Meseji ulikuwa umeambatana na meseji ya muamala wa fedha uliotumwa katika akaunti ya benki ya mke wangu. Ujumbe Ulisomeka hivi:
“Mbona hupokei simu mrembo? Nimekuingizia milioni tatu kwenye account yako ya bank, nimekutumia na ujumbe wa muamala nilioufanya. Nitafute.”
“Nani huyu!!!!.” nilinong’ona.
Nikafikiria mtu ambaye anaweza kumpa mke wangu kiasi kile cha fedha, bado sikuona ndugu yake yeyote mwenye uwezo huo.
Huyu mtu sasa atakuwa ni nani, kwa nini amtumie mke wangu fedha zote hizi, na mke wangu naye pesa hii ya nini?
Maswali yalikuwa mengi kichwani kuliko majibu, mwisho nikaona njia nzuri ya kupata majibu ni kuinakiri ile namba katika simu yangu, kisha nimpigie mfadhili yule na nimuulize yeye ni nani na alikuwa na biashara gani na mke wangu.
Nilinakiri haraka kisha nikaipiga, lakini kabla simu haijanza kuita nikaikata simu. Wazo jipya likanijia. Niliona njia ile sio njia nzuri sana ambayo ingeweza kunipa ukweli wa jambo lile.
Kama kulikuwa na biashara isiyo ya kawaida kati ya mke wangu na mtu aliyemtumia fedha, kwa kutumia njia niliyotaka kuitumia, kamwe nisingeweza kubaini ukweli. Niliwaza kimoyomoyo.

Na wakati mawazo hayo yananijia kichwani, wivu wa mapenzi ukaanza kujitengeneza moyoni, fikra mbaya zikaanza kuniteka. Hisia za mke wangu kuhongwa kiasi kile cha fedha na mwanaume mwingine mwenye uwezo mkubwa zaidi yangu zikavuruga kabisa mwenendo wa utashi wangu.

Waswahili wanasema: Subira yavuta heri. Nilichofanya ni kui-save’ namba ya mtu yule, halafu nikafuta simu zote zilizoingia kwenye simu ya mke wangu ikiwa ni pamoja na ule ujumbe unaomtaarifu kuwa amekwishamwingizia milioni tisa kwenye akaunti yake.
Nilifanya vile makusudi ili mke wangu asibaini chochote kama kuna mambo yasiyo ya kawaida nimeanza kuyashtukia.
Jambo la mwisho nililofanya katika simu ile nilifungua faili lililoandikwa ‘Play store’, nikafungua, kisha nikapakua ‘program’ iitwayo ‘Voice recoder, nikaiseti simu ile iwe inajirekodi yenyewe simu yoyote itakayokuwa inaingia na kutoka.

Baada ya hapo, nilitulia tuli. Moyoni nikiweka nadhiri ya kulifuatilia jambo lile kimyakimya. Muda mfupi badaye, mke wangu na nduguye walimaliza kupika. Aliniandalia chakula, tukala wote pamoja. Wakati wote nilimwonesha tabasamu, sikumwonesha kama kuna kitu kisicho cha kawaida nimekibaini dhidi yake.
Baada ya mlo wa usiku, tulielekea chumbani mwetu kulala huku mdogo wake Aisha, naye akielekea chumbani mwake.
Tukiwa chumbani, kama kawaida tulipeana mapenzi motomoto na kama nilivyokwishaeleza awali,katika kipindi cha miezi mwaka mmoja, tangu nifungue usichana wake, mke wangu alikuwa mjuzi mno kitandani. Tulipeana mapenzi mazito hadi miili yetu iliporidhika.
“Ahsante mume wangu.”
“Kwa?”
“Penzi tamu, unajua sana kunikuna,” mke wangu aliniambia baada ya kumaliza mmenyano.
“Kweli?”
“Sikudanganyi mume wangu.”
“Lakini hata wewe siku hizi umekuwa fundi sana kitandani.”
“Muongo.”
“Kweli mke wangu, sijui nani amekufundisha.”
“Nimefundishwa na wewe mwenyewe au umesahau?”
“Nikumbushe.”
“Umesahau ‘ningali’ mwanamwali ulichonieleza?”
“Nilikueleza vingi, kipi unachokusudia?”
“Kuhusu aibu.”
“Alaa! Kumbe somo hilo.”
“Ndiyo, siku hizi ninalifaulu kwa kiwango kikubwa, ndio maana unaona nimekuwa fundi kitandani.”
Tulizungumza na kufanyiana utani wa hapa na pale kisha usingizi mzito ukatuchukua.

****
Ilikuwa ni asubuhi ya siku mpya, wingu la mvua lilikuwa limetanda, ngurumo za radi zilidhirisha uwepo wa mvua kubwa ambayo ingenyesha asubuhi hiyo.
Magari yalikuwa mengi barabarani, watu walikuwa wakihaha huku na kule kuhakikisha wanakuwa sehemu salama ili kujiepusha na kadhia ya matone ya mvua.
Ngurumo za radi zilizokwenda sambamba na miale mikali, ilifanya asubuhi ya siku hiyo kuwa nzito kwa wakazi wengi wa jiji la Dar Es Salam.
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo ilianza kunyesha, upepo ulikuwa ukizoa takataka zilizotapakaa hovyo barabani na kuzisukuma hovyo.
Mimi nilikuwa katika gari langu, nilikuwa nimenasa kwenye foleni katika Barabara ya Karume, ambapo askari wa usalama barabara alikuwa akiita magari ya upande mmoja huku akiacha ya upande wetu magari yakizidi kujilundika kama uyoga.
Nikiwa ndani ya gari, mawazo yangu yalikuwa ni juu ya mtu aliyemtumia mke wangu milioni tatu kwenye akaunti yake.
Bado swali kubwa lilikuwa ni mtu yule ni nani? Na alikuwa na ajenda gani na mke wangu? Kwa kweli jambo lile lilinikoroga mno.
Au alikosea namba?
Hawezi kukosea namba ya simu hadi namba za akaunti ya benki.Nilijiambia kwa sauti ndogo.
Katika kufikiria, nikawa nimepata wazo moja la kumjua mtu huyo.
Kuangalia jina lake kupitia namba aliyosajilia laini yake ya simu.
Nilinyakua simu yangu iliyokuwa kando, kisha nikaifungua namba yake, bahati nzuri namba zile zilikuwa za mtandao mmoja na ule niliokuwa nikitumia mimi.
Nikanza mchakato wa kufanya kama namtumia pesa ili nilione jina lake, ilipofika sehemu ya kuweka pesa nikaweka, na kabla ya kuweka namba ya siri ndipo nilipoliona jina lake.
Moyo wangu ulilipuka baada ya kuona jina la mtumiaji wa namba ile.
“Mungu wangu ni huyuuu!!!” nilipayuka. Taharuki kubwa ikanivaa, sikuamini kabisa kuona jina la mtu ambaye sikumtegemea.

JE MTU HUYO NI NANI?
ANAJENDA GANI NA MKE WA MTU?
NI KITU GANI KITATOKEA?
 
DAMU YA MWANAMWALI

SEHEMU YA 5

MTUNZI: Ally Katalambula

0687 750295

ILIPOISHIA ...
Nikanza mchakato wa kufanya kama namtumia pesa ili nilione jina lake, ilipofika sehemu ya kuweka pesa nikaweka, na kabla ya kuweka namba ya siri ndipo nilipoliona jina lake.
Moyo wangu ulilipuka baada ya kuona jina la mtumiaji wa namba ile.
“Mungu wangu ni huyuuu!!!” nilipayuka. Taharuki kubwa ikanivaa, sikuamini kabisa kuona jina la mtu ambaye sikumtegemea.

ENDELEA NAYO...

SURA YA TATU

“Piii piiii!!” wakati huohuo nilisikia honi za magari zikitokea nyuma yangu.
Nilistuka. Askari wa usalama barabarani alikuwa ameita magari ya upande wetu, niliweka simu kando na kuliondoa gari kwa kasi.
Baada ya kumvuka mataa ambapo yule askari alikuwa amesimama katikati ya zile njia panda nne huku akiiendelea kuita magari ya upande niliotokea, nilipunguza mwendo, nikaangalia kama kuna mtembea kwa miguu yeyote ambaye alikuwa akivuka barabara, nilipoona ni shwari, nikanyooka na Barabara ya Chang’ombe.
Dakika ishirini baadaye niliwasili ofisini, akili yangu bado ilikuwa kwenye jina la mtumiaji wa namba iliyomtumia mke wangu pesa.
“Bosi naona leo uko mbali sana,” katibu muhtasi wangu aitwaye Debora aliniambia akiwa anamimina kahawa katika kikombe baada ya kuwa nimekwishaingia ndani ya ofisi yangu.
“Kivipi?” nikamuuliza.
“Umeingia ofisini ukionekana kuchanganyikiwa sana, hata salamu za baadhi ya staf hujajibu.”
“Kweli?”
“Tangu lini nimekufanyia masikhara bosi?”
“Kuna mambo fulani yananichanganya Debora,” nilimwambia.
“Unaweza kunishirikisha, pengine naweza kuwa na msaada.”
“Laaa! Si kitu, ni mambo binafsi,”nilimjibu, sikupenda mambo yangu nimshirikishe Debora ingawa tulikuwa tumeshibana mno na msichana yule.
Mimi na Debora ukiachilia mbali mimi kuwa bosi wake, lakini binti huyo mwenye umbo zuri na sura ya kushawishi tulikuwa ni maswahiba wa karibu sana, urafiki wetu ulitokana na kuendana tabia fulani fulani. Nitaelezea wakati mwingine ni tabia gani tuliendana mimi na Debora, kwa sasa itoshe tu kufahamu kwamba mimi na binti yule, tulikuwa ni marafiki wa karibu.
Baada ya kuniandalia kahawa na kuondoka, nikawa na wakati mwingine wa kutafakari juu ya uhusiano ulipo kati ya mke wangu na mtu yule aliyemtumia pesa.
Baada ya kutafakari kwa kina nikawa nimepata majibu ni kitu gani natakiwa kufanya kama mwanaume ili niweze kutatua tatizo lile ambalo lilikuwa limekwishaanza kutia doa katika ndoa yangu.
Nilifanya kazi zangu zote pale ofisini, saaa kumi jioni, nilikuwa ndani ya gari langu nikirejea nyumbani.
Baada ya kufika, kama ilivyo ada, mke wangu alinikaribisha kwa mapenzi na mahaba yote, nilikwenda kuoga, baada ya kutoka bafuni, nikakuta juisi nzito ya parachichi ipo mezani, akanikaribisha kinywaji kile.
Wakati napata kiburudisho ndipo nikaanzisha mazungumzo:
“Mke wangu Nasra,” nilimwita kwa sauti tulivu.
“Rabeka mume wangu,” akaitika.
“Nina mazungumzo na wewe leo.”
“Naona fikra zetu zilikuwa sambamba,” mke wangu naye akasema.
“Kwa nini?”
“Hata mimi nilikuwa nahitaji kufanya mazungumzo na wewe, tena leo hii.”
“Kweli fikra zetu zilikuwa zikisafiri katika ngalawa moja,” nikamjibu, akatabasamu. Tabasamu la mke wangu huwa ni sumu mbaya sana nafsini mwangu.
Tabasamu lile likaamsha maruhani yaliyokuwa yamelala kwa wakati huo.
“Vipi tena?” akahoji, alipoona mikono yangu inazunguka kiunoni mwake.
“Majini yamepanda.”
“Yatulize kwanza tuzungumze.”
“We’ ndiye mganga wangu, tuliza tu haya mapepo,” nilimjibu kwa utani nikiwa napenyeza mkono wangu kwenye ikulu yake.
“Weweeee!” mguno wa ajabu ukamtoka wakati kidole changu kikifanya ziara ya kushitukiza kwenye ofisi nyeti.
“Si…si…ta…taa..ki,” akaendelea kuweweseka huku akinivutia kitandani.
Nikamchojoa nguo zake, kisha nikaanza kumfanyia ujuvi. Wakati namfanyia utundu huo, mke wangu aliweweseka kama mgonjwa wa degedege, hazikuzidi dakika 20 tukajikuta tupo kwenye gumzo la pamoja kitandani.
Mchezo ule ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja. Tulirudi bafuni, tukaoga huku tukifanyiana michezo ya kitoto, kwa kweli ulikuwa ni wakati mzuri mno maishani japokuwa kulikuwa na jambo zito lililonifukuta.
Tuliporejea mezani ambapo kulikuwa na kile kinywaji laini cha juisi, mke wangu ndiye alikuwa wa kwanza kuanzisha mjadala kuhusu yale mazungumzo yetu.
“Unaonaje ukianza kuzungumza kile ulichodhamiria kunieleza kisha na mimi niseme kitu gani nataka kuzungumza na wewe” nilimwambia mke wangu. Wazungu wanasema ‘Lady is first’
“Sawa mume wangu.”
“Nakusikiliza sasa,” nilimwambia
“Jambo lenyewe ni hivi…” alianza kunieleza.
“Nimepata dili moja kwenye kampuni ya sky production ambayo ipo chini ya yule mwanamuziki maarufu aitwaye Abdul Ally.” alisema, akanyanyua glasi ya juisi na kupiga funda moja, kisha akaendelea.
“Kwa kweli nimekuwa njia panda kama natakiwa kukubaliana na ombi la hawa jamaa ama laa! Hii ni kutokana na aina ya kazi ambayo natakiwa kufanya. Ndiyo maana kabla ya yote nikaona nikushirikishe wewe mume wangu,” alisema.
Jambo alilonieleza mke wangu, ni jambo hilohilo ambalo nilitaka kulijadili na yeye, katika maelezo yake bado nilikuwa na mambo mengi ambayo ningependa kujua, hivyo kwa kuwa mjadala wa jambo lile ulikuwa mezani nikaona hiyo ni njia pekee ya kufahamu chungu na tamu.
“Umemaliza?” nilimuuliza
“Ndiyo mume wangu.”
“ Jambo ulilonieleza, ndilo na mimi nilitaka kulizungumzia, kwa kuwa nilianza kulifahamu kabla hujanieleza…” nilisema. Mke wangu akashtuka, niliendelea kuzungumza.
“Maadam jambo hilo ni moja basi hebu tulizungumze…” nilipiga funda moja la juisi, nikaendelea:
“Kwanza kabisa ningependa kujua wewe na mwanamuziki, Abdul Ally umefahamiana naye vipi hadi ukafikia kupewa hilo unaloliita dili?”
“Ilikuwa ni kama ajali,” alijibu.
“Sijakuelewa”
“Nilikutana naye supermarket.”
“Eeh!”
“Ndiyo mume wangu.”
“Endelea kueleza.”
“Nilipokuwa naemea mahitaji ndani ya ile supermarket, alinifuata na kunieleza kwamba amevutiwa na mwonekano wangu, hivyo ingekuwa ni vema kama ningeshiriki kwenye video yake mpya anayotarajia kutoa hivi karibuni.
“Awali nilichukulia kama masikhara. Na nilidhani ni janja tu ya wanaume wa mjini ili aweze kunilaghai kimapenzi, lakini nilipokutana naye siku zile nilipokwenda kufuatilia ATM kadi yangu pale CRDB ndipo akakamilisha hili dili palepale benki aliniwekea milioni moja kwenye akaunti yangu.
Akaniambia hiyo ni fedha ya awali, angenilipa zaidi kama ningekuwa tayari kufanya naye kazi, ndipo nilipoona kaka huyu anamaanisha kile anachotaka.”
“Hiyo milioni moja ilikuwa ya nini?” niliunguruma
“Alinipa kama motisha ya kukubali ofa yake.”
“Ofa!!!” nilimaka.
“Ndiyo.”
“Ya nini?” nikauliza kwa ukali
“ Faraji nimekwambia, eti kama motisha ya kutakafari jambo lake”.
“Eeh” nilizidi kumaka. Mke wangu akaendelea kueleza:
“Baada ya hapo amekuwa akinipigia mara kwa mara akitaka kujua nimefikia wapi,”
“Kwa nini ulimpa namba yako bila idhini yangu?” nilibweka hadi cheche za mate zikanitoka.
Mke wangu alikaa kimya kidogo, kisha kwa upole akaniambia:
“Mume wangu, niliona hii ni fursa nzuri ya biashara.”
“Biashara au umalaya tu…Endelea kueleza.” nilisema kwa ukali
“Mara ya mwisho nilimwambia lazima nimshirikishe mume wangu juu ya jambo hilo, lakini leo ameniambia amenitumia milioni tatu kama sehemu ya malipo ya awali ya mkataba wangu, amefanya hivyo bila kujali kama jambo hili litawezekana ama laa,” mke wangu alimaliza.
Nilishusha pumzi ndefu, kisha nikamuuliza:
“Kazi unayotakiwa kufanya kwenye hiyo kampuni ni ipi?”
“Kushiriki kwenye video zake kama video vixen ama imean video Queen…” alinijibu.
“Nini!!...” niliuliza kwa jazba nikiwa nimetoa macho.
“Sitaki, nasema sitaki kabisa kusikia huo upuuzi….” nilipayuka kwa ukali hadi cheche za mate zikanitoka tena.
“Umenielewa wewe?”
“Ndiyo mume wangu nimekuelewa,” mke wangu akaitikia kwa utii.
“Eti uwe video queen, khaa! yule mpuuzi amekuchukuliaje? Anadhani wewe ni kiruka njia kama hao wanawake wengine wanaoacha miili yao uchi huku wakishikwashika hovyo,” niliendelea kuunguruma.
“Kwanza Tangu lini hao ‘video vixen ’ wanalipwa milioni tatu, kama hana nia ya kukulaghai.”
Kwa kweli nilikuwa na wivu mkubwa mno dhidi ya mke wangu, sikuwa tayari kuona mwanamke yule anajihusisha na mambo ya kidunia, hususani masuala ya muziki.
Niliamini wanawake wote wanaojihusisha na sanaa za muziki na unenguaji walikuwa ni viumbe waliokubuhu kwa umalaya.
“Hivi mke wangu, unajua kama muziki ni haramu kwa mujibu wa dini yetu?”nikamuuliza huku nikiwa nimemkazia macho
“Najua mume wangu.”
“Sasa kwa nini unataka kujihusisha na huo uovu?”
“Nisamehe mume wangu.”
“Nisikilize…”nilisema macho yakiwa yamenitoka pima.
“Pesa alizokupa huyo baradhuli mrudishie zote, sitaki kabisa kuona upo karibu na huyo mtu…Sawa”
“Nimekusikia mume wangu.”
“Siyo unisikie tu na unielewe wewe.”
“Nimekuelewa Faraji,” mke wangu aliendelea kunijibu kwa utii.
Baada ya hapo tukakubaliana ampigie mwanamuziki yule na amweleze juu ya kujiweka mbali naye na kuacha mazoea ya karibu.
Alichukua simu yake na kumpigia Abdul Ally mwanamuziki wa kizazi kipya. Simu iliita bila kupokelewa, akapiga tena, iliita muda mfupi baadaye ikapokelewa na mwanamuziki yule
“Mume wangu amekataa na hataki kabisa uwe na mazoea na mimi, kwa hiyo naomba usitishe mazoea…Nipe akaunti yako nirejeshe fedha zako,”mke wangu alimpasha simuni Abdul Ally.
“Kuna nini tena baby, kwa nini mumeo anakuwa na swaga za kishamba namna hii, anakukoseshaje dili kubwa kama hivi?”Abdul Ally aliongea kwa lafudhi za vijana wa kileo.
Nilijisikia vibaya sana mtu yule kuniita mshamba mbele ya mke wangu, kwa kuwa simu ilikuwa imewekwa ‘loud speker’ niliichukua kisha tukaanza kutupiana maneno na mwanamuziki yule maarufu.
Tulitukanana matusi ya nguoni hadi simu ilipokatika kwa kuishiwa salio, kwa kweli siku hiyo iligeuka na kuwa siku mbaya mno.
***
Masiku yalikatika, angalau amani na furaha ikaendelea kudumu kwenye ndoa yangu, mawasiliano kati ya mke wangu na Abdul Ally yalikufa.
Mke wangu akazidi kuwa mwaminifu, akawa mchamungu, upendo na heshima dhidi yangu ilikuwa haina mfano, urembo wake ukabakia kuwa mali yangu, nilinenepa, dunia yote ikawa yangu.
Miezi michache badaye, mke wangu alinasa ujauzito, jambo hilo lilizidisha furaha kubwa katika ndoa yangu.
Nilifuarahi kuona siku moja ningeitwa baba, sikujali ni mtoto gani angezaliwa, kwangu mtoto wa jinsia yoyote nilikuwa tayari kumpokea kwa mikono miwili.
Niliona siku zinakwenda taratibu, shauku ya kupata mtoto ilikuwa kubwa, mapenzi kwa mke wangu yalizidi maradufu.
Sikupenda hata mara moja kuona mwanamke yule anaingia kwenye mkanganyiko wowote katika nyakati zile za kulea mimba.
Siku zilienda, waswahili wanasema ‘ndondo si chururu’ Baada ya kusubiri hatimaye miezi tisa ilitimia. Usiku mmoja mke wangu alipatwa na uchungu, upesi mimi na mdogo wake Aisha tukamwingiza kwenye gari langu na kumwahisha Hospitali ya Regency.
Baada ya kuwasili, manesi walitupokea mbiombio, kwa kuwa hali yake ilikuwa mbaya, alipelekwa moja kwa moja leba.
Mimi na Aisha tuliibakia nje kwenye benchi, mbele ya mlango wa kuingilia katika chumba ambacho mke wangu Nasra aliingizwa.
Tulisubiri pale kwa muda mrefu sana, nakumbuka karibu masaa matatu tulikuwa nje ya wodi ile.
Daktari alishauri tuondoke na turudi kesho yake kwa kuwa uzalishaji wa mke wangu ilikuwa na mizengwe mingi.
Kauli ya daktari ilinitisha, hata hivyo nilipiga moyo konde na kuondoka kuerejea nyumbani. Usiku ule sikulala, moyo ulikuwa ukinidunda, presha ilikuwa juu.
Siku iliyofuatia. Asubuhi na mapema, niliamka nikajiandaa, kisha nikamuaga shemeji yangu Aisha, nikimtaka yeye aje Hospitalini baadaye mchana, baada ya kumaliza shughuli zake asubuhi ile.
Niliendesha gari hadi Posta, kwa kuwa magari yalikuwa machache, muda mfupi badaye nilikuwa Regency. Baada ya kufika manesi walinipokea kwa sura zisizokuwa na chembe ya ukarimu wowote.
Mapigo ya moyo yakaanza kunidunda, nikanza kuhisi heunda kuna jambo baya limetokea dhidi ya mke wangu na mtoto.
“Vipi hali ya mke wangu?’ nilimuuliza nesi mmoja.
“Daktari Charles Meleka amesema ukifika tu ukamuone ofisini kwake,” badala ya kujibu swali, nesi yule aliniambia kitu kingine kabisa.
“Mke wangu ni mzima?” niliuliza kwa wahaka mapigo ya moyo yakinIenda kasi
“Kaka hebu kuwa mwelewa,” nesi alizidi kuwa mkali.
Nikaona nisiendelee kulumbana na yule mwanamke, nilichofanya ni kwenda kwenye ofisi ya dokta Charles Meleka.
Baada ya kuingia ndani ya ofisi ile dokta Cherles alikuwa ameketi katika kiti cha kuzunguka huku mezani kwake kukiwa na mafaili kadhaa.
“Hongera Mr Faraji Hussein…” Dr Charles alianza kunipasha baada ya kuingia.
“Mkeo kajifungua mtoto wa kiume tena kajifungua salama kabisa….lakini…” Dr Charles Meleka alisema.
“Lakini nini?” nikauliza kwa kiherehere.
“Kwa nini unafanya mapenzi na mkeo kinyume na maumibile?” Dr Charles Meleka aliniuliza kwa ukali. Nikabaki nimepigwa na bumbuwazi.

ITAENDELEA
 
DAMU YA MWANAMWALI....

MTUNZI: ALLY KATALAMBULA

SEHEMU YA 6

SIMU: 0687750295

ILIPOISHIA...

“Kwa nini unafanya mapenzi na mkeo kinyume na maumibile?” Dr Charles Meleka aliniuliza kwa ukali. Nikabaki nimepigwa na bumbuwazi.

SEREREKA NAYO...

MWANZONI nilidhani labda swali lake lilikuwa na maana nyingine zaidi ya vile linavyoweza kueleweka. Lakini nilipoona uso wa daktari yule ukiwa katika hali ya kungoja jibu la swali lile nikatambua hakuwa na maana nyingine zaidi ya vilevile alivyohoji!

“Unamaana gani kusema hivyo?”
“Sina maana yoyote zaidi ya kukuonya tabia ya kumwingilia mkeo kinyume na maumbile,” dokta akaniambia, tena alisema huku akiwa amenikazia macho.
Niliendelea kuchanganyikiwa. Mambo niliyokuwa naelezwa na daktari yule yalikuwa yakiniikoroga akili yangu. Kila kitu kilikuwa ni michoro isiyoeleweka.
Sikuwahi kuwa na michezo ya kishenzi kwa mke wangu, kitendo cha kutuhumiwa kumwingilia mke wangu kinyume na maumbile, ilikuwa ni fedheha mbaya sana.
“Sijawahi kufanya huo mchezo mchafu…” nilimwambia kwa ukali kidogo.
“Una uhakika?”
“Kabisa dokta, sijawahi kujihusisha na tabia za namna hiyo.”
“Basi inawezekana kabla ya kukutana kwenu mkeo alipitia hii michezo,” dokta alinileza.
“Kujihususha na mapenzi kinyume na maumbile?”
“Ndiyo,” alitikia kwa kwa upole.
Mate mepesi yakanijaa kinywani. Jambo lile lingewezekanaje wakati mimi ndiyo nilikuwa mwanaume wake wa kwanza? Nilimkuta akiwa mwanamwali, tena bikira, mshamba kwenye ulimwengu wa mapenzi.
“Lakini inawezekanaje hilo dokta? Mimi ndiyo nilikuwa mwanaume wa kwanza. Nilimkuta akiwa mshamba kabisa kitandani.” nikauliza kwa fadhaa nikitaka ufafanuzi na uthibisho juu ya alichonieleza.
“Kweli?”
“Ndiyo.” niliitikia huku nikimwangalia usoni.
Alifikiria kitu kisha akasema:
“Nimekuwa daktari wa wanawake huu mwaka wa 17, mwanamke anapojifungua, hutokea mara kwa mara kutokwa na haja kubwa, lakini kwa mkeo ilikuwa ‘too much’ uzoefu unaonesha mtu wa aina hii amekubuhu kwenye tabia za kuingiliwa kinyume na maumbile,” dokta alinipasha.
Nilijisikia vibaya sana, maneno ya Dk. Charles yalinisuta, yakanifanya nijione bwege. Tafsiri rahisi ni kwamba, maisha ya nyuma ya mke wangu yalikuwa na siri kubwa iliyojificha.
“lakini usijali Faraji, siyo kesi sana, haya ni mambo ya kawaida tu maishani, ” daktari aliendelea kunitia moyo, kimuonekano ni kama yeye pia alibaini kwamba jambo lile lilikuwa ‘surprise’ kwangu, na alivyoonekana alitaka jambo lile nisilichukulie kwa uzito utakaopelekea ndoa yetu kutikisika.
“Ndiyo maana nilipoingia hapa manesi hawakunichangamkia, kumbe kulikuwa na kasheshe wakati mke wangu anajifungua!”
“Faraji nikwambie mara ngapi hayo ni mambo madogo, hebu achana nayo na jaribu kusahau.
“Siri kubwa ya kuwa na furaha maishani ni kutokukumbuka mambo mabaya ya nyuma…”alisema, kisha akabadili mada.
“Mkeo amejifungua mtoto wa kiume,” aliniambia huku akifunua funua makablasha yaliyokuwa mezani.
“Kweli?”
“Kwa nini nikudanganye?”
“Ahsante dokta, ahsante kwa kumsaidia mke wangu.”
“Karibu tena Faraji,” alisema huku akinipa mkono wa pongezi.
Alinipeleka kwenye kitanda alicholala mke wangu na mtoto
Nililimkumbatia mke wangu na kumpa pole na pongezi ya kunizalia dume la mbegu.
“Ahsante mume wangu, hongera na wewe pia kwa kunipa mimba,” mke wangu naye alinipa pongezi zilizonifanya nijione kidume.
Wakati wote nilimwonesha uso wa tabasamu, sikupenda kabisa malumbano juu ya jambo alilonieleza dokta katika kipindi hicho cha uzazi.
Hata Dk. Charles aliendelea kunisihi niachane kabisa na mambo yale ambayo kama ningeyaibua pengine yangepelekea ndoa yangu kuwa matatani.
Nilimuitikia na kumuhakikishia amani ya kudumu kati yangu na Nasra, mwanamke mrembo mwenye asili ya Kipemba, ambaye nilichaguliwa na wazazi wangu kama mke.
Tuliruhusiwa kurudi nyumbani, tukiwa na mtoto mzuri wa kiume, niliwataarifu ndugu na jamaa juu ya kupata mtoto, ilikuwa ni furaha kubwa.
Kwa kuwa mke wangu alikuwa akitakiwa kupata huduma za hapa na pale kama kukandwa maji na kuelekezwa mambo mengine juu ya malezi ya mtoto mchanga, ilibidi mama yangu afunge safari kutoka Nguruka aje Dar Es Salam kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Baada ya ujio wa mama, nyumba yangu ikazidi kuwa na furaha, mama alimsadia mke wangu katika kila kitu alichohitaji. Mtoto naye alizidi kukua, na miezi michache badaye tulimpa jina. Tukamwita Mwanda.
Siku zilikwenda, miezi ikayoyoma. Sakata la mke wangu kuingiliwa kinyume na maumbile niliendelea kuliweka kiporo. Kama nilivyosema awali sikupenda kuleta ukinzani wowote kati yangu na mke wangu hasa katika nyakati zile.
Furaha, vicheko na tabasamu viliendelea kushamiri katika familia yangu, kwa kweli nilikuwa ni moja ya vijana wachache wanaofaidi matunda ya elimu yangu.
Wazungu wana msemo mmoja unaosema:
“It is always the very good times of one’s life that normally turns into one’s very bad times in no time…”
Hii ina maana kwamba kama mtu akiwa katika maisha mabovu hakuna kibovu zaidi kitakachomkuta zaidi ya hicho, lakini akiwa kwenye maisha mazuri ndiyo ataona mabadiliko pale hali hiyo itakapotoweka. Na kwa kawaida maisha mazuri huwa hayadumu. Wakati nasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam msemo huu nilikuwa nauelewa sana.
Ajabu katika nyakati zile nilisahau kabisa juu ya ukweli huu. Wakati nikiwa nimesahau kabisa juu ya falsafa hii ghafla amani ndani ya nyumba yangu ikaanza kutoweka.
Mambo yalianza kama masikhara. Kukawa na mikwaruzano ya hapa na pale kati ya mke wangu na mama yangu mzazi, mama yangu alikuwa akimtuhumu mke wangu kwa tabia ya kupenda sana kuchati na simu kuliko mambo muhimu, wakati mke wangu naye alikuwa akimtuhumu mama kwa tabia ya kupenda kulalamika kwa mambo madogo madogo.
Madai yote hayo, yalipoletwa mbele yangu, niliyapuuza, kwakuwa sikuona kama yanamashiko. Sikujua kama nakosea. Na sikujua kama kwa kupuuza migogoro ile ilikuwa ni mwanzo wa kuingia kwenye historia mbaya sana maishani.

Je nini kilitokea kwenye maisha ya Faraji Hussein Mpangalala na ndoa yake...Majibu yanapatikana kesho saa nne, mahali hapa.

UKITAKA KITABU CHA SIMULIZI HII NICHEKI KWA 0687750295
 
KITABU: DAMU YA MWANAMWALI
MTUNZI:ALLY KATALAMBULA
SEHEMU YA 7
0687750295

SURA YA NNE

MAMA alinisihi nimkanye mke wangu kwa tabia ya kupenda kuwa bize katika mitandao ya kijamii kiasi cha kusahau majukumu yake muhimu.
Kama niliyosema awali, sikuchukulia kwa uzito mkubwa jambo hilo, nadhani ni kwakuwa muda mwingi nilikuwa nikishinda ofisini, hivyo sikuona athari za jambo alilonieleza mama yangu.
Mke wangu naye hakuisha kunishitakia mapungufu ya mama, alimtuhumu kwa tabia ya kumchunga kama mtoto mdogo, akamtuhumu kuwa alikuwa na hasira za karibu.
Mambo yaliendelea kuwa hivyo bila mimi kuchukua maamuzi yoyote.

Jioni moja mama aliniomba nimpe nauli ili siku inayofuatia arejee Kigoma.
“Kuna nini. Mbona ghafla?”
“Nilikuja kwa ajili ya kumsaidia mkeo.Nimemaliza”
“Sasa kwa nini uondoke kama unakimbizwa, si ukae tuiandae safari vizuri.”
“Nimekwishakaa sana hapa, kesho lazma niondoke.”
Uso wake ulionesha kama alikuwa na jambo zito lililomkwaza moyoni, nilihisi huenda kulitokea sintofahamu kubwa kati yake na mke wangu siku hiyo.
“Kwani mama una tatizo gani?”
“Kivipi?”
“Unaonekana hauko sawa.”
“Siku zote sipo sawa, we’ wagundua leo?”
“Ni nini hasa?”
“Hujui?”
“Ni yaleyale ya siku zote?”
“Ndiyo hayo hayo.”
“Mama unajua sivutiwi na namna mnavyoshindwa kuishi vizuri na mke wangu.”
“Ndiyo maana nataka kesho nijiondokee ili uwe na amani moyoni.”
“Kwani ni kipi hasa alichokufanyia mke wangu?”
“Sijafanyiwa mimi ila unafanyiwa wewe,” alisema.
“Nafanyiwa nini?”
Hakunijibu.
Alisisitiza nimpe nauli ili siku inayofuatia arejee Kigoma.
“Kwa kuwa mama aling’ang’ania sana kuondoka, nilichofanya ni kuindaa safari jioni hiyo hiyo. Nilimpigia simu jamaa yangu mmoja aitwaye Frank Majige, ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirikika la Ndege la FastJet nikamuomba aniafanyie mpango wa tiketi asubuhi ya kesho.
Kupata tiketi chini ya Frank Majige ilikuwa ni kazi rahisi. Sikutaka mama asafiri kwa basi au treni kutokana na kadhia ya usafiri huo. Siku iliyofuata, nilimsindikiza uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere, akapanda ndege ya saa mbili kamili na kurudi Kigoma.
Baada ya kuhakikisha mama ameondoka, nilirudi kwenye gari ili kuendelea na ratiba zangu nyingine. Nikiwa njiani narudi nyumbani, sikuwa na raha kabisa, uondokaji wa mama sikuupenda, zaidi ya dada wa kazi , aitwaye Doreen, si shemeji yangu Aisha wala mke wangu Nasra aliyemwambia mama neno kwaheri.
Niliazimia nitakaporejea nyumbani, lazima nimweke kitako mke wangu na nimkanye juu ya tabia hiyo. Sikupenda Nasra aendelee kuwa na uhasama na mama.
Nilipowasili nyumbani, mke wangu alikuwa sebuleni, alikuwa bize na simu yake. Nilimtaka aje chubani. Mimi nikatangulia ndani, nilipoingia tu, nikamkuta mtoto analia huku akiwa ametota kwa mkojo.
Mara mke wangu naye akaingia, alipoona mtoto analia huku akiwa amejikojolea ndiyo akajitia kushtuka na kwenda kumnyanyua.
“Wewe kwa nini unamwacha mtoto kwenye hali hii?” nilimuuliza kwa ukali.
“Sikujua kama angeamka sasa hivi.”
“Nilipoambiwa kwamba mitandao ya kijamii imekuteka akili, nilibisha, lakini leo nimejionea.”
“Sasa hayo yametokaea wapi mume wangu?”
“Unawezaje kuwa Facebook kiasi cha kumsahau mwanao?”
“Nikwambie mara ngapi sikujua kama angeamka sasa hivi.”
“Hebu nenda kamsafishe kisha urudi hapa tuzungumze,” nilimwambia. Aliondoka muda mfupi baadaye akarejea.
“Ulishindwa hata kumwambia mama kwaheri.”
Nilianza kumpasha.
“Mbona yeye hakuniaga?”
“Kwa hiyo unashindana na mzazi?”
“Wala.”
“Kumbe?”
“Mama yako anamatatizo mengi.”
“Sawa, ila wahenga wanasema, mzazi hakosei.”
“Mama yako anakosea na amezidi.”
“Sasa nisikilize…” nilimwambia.
“Unatakiwa kumwomba msamaha mama.”
“Kwa kosa gani?”
“Siyo kwa kosa gani Nasra, unachokifanya ni kutengeneza mahusiano mazuri na wazee.”
“Nitakuwa mnafiki kama nitafanya hilo unalolitaka, sitaweza,” mwanamke yule alinikatalia kwa ujasiri mkubwa.
Nikabaki kinywa wazi. Nilimsihi sana na kumweleza faida ya kufanya jambo hilo, lakini mke wangu alinikatalia katakata kumuomba mama msamaha.
Maisha yaliendelea, jambo lile nikalipuuza na kulitupilia mbali!. Na kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo hata songombingo la tuhuma za mke wangu kuwahi kuwa na tabia za mkushiriki mapenzi kinyume na maumbile nalo nikaliona la kawaida tu!!!.
Nikijibidiisha sana katika kazi zangu, miladi yangu ilizidi kukua siku hadi siku, miezi michache baadaye niliamua kuacha kazi serikalini na kuweka nguvu katika biashara zangu.
Muda wangu wa kutulia na familia yangu ukawa mdogo, nilikuwa nikitoka nyumbani asubuhi, kurudi kwangu ilikuwa ni saa nne usiku hadi saa sita.
Katika nyakati zile zile, nilipata pigo baya maishani. Nakumbuka ilikuwa ni asubuhi moja nilipata simu mbaya kutoka nyumbani, baba yangu mzee Hussein Mpangalala alinguka bafuni kutokana na presha iliyopanda, na alifariki njiani alipokuwa akiwahishwa hospitalini.
Ulikuwa ni msiba mzito maishani, mimi na mke wangu, tulisafiri hadi Kigoma kwenye mazishi ya baba.
Baada ya mazishi, watu walikaa matanga siku kadhaa huku tukisubiri 40 kwa ajili ya kisomo.
Tukiwa tunagoja 40, Mke wangu nilimtaka arudi Dar ili akasimamie maduka ambayo kwa wakati huo yalikuwa chini ya wafanyakazi.
Kwa kuwa mimi ndiyo nilibaki kuwa kiongozi wa familia, nikabakia na mama pale nyumbani kama sehemu ya kumtia nguvu na faraja katika kipindi kile kigumu.
Arobaini ilipopita, nilirudi Dar es salama kuendelea na maisha. Nilipofika nyumbani nilikutana hali iliyonishangaza.
Mtoto wangu Mwanda, ambaye kwa nyakati zile alikuwa kama ana mwaka mmoja na nusu kama sijakosea. Nilimkuta mtoto amekondeana sana, nywele zake zilikuwa zimenyonyoka, mwili wake akionekana kudhoofu.
“Anaumwa?” nilimuuliza mke wangu
“Aka.”
“Sasa kwa nini yupo hivi?”
“Mwenyewe nashangaa.”
“Ushawahi kumpeleka hospitali?”
“Bado.”
“Kwa nini?”
“Sijaona athari za moja kwa moja.”
Majibu ya mke wangu yalinifanya nitamani kumzaba kibao, lakini nilijizuia. Nilichofanya ni kumchukua mwanangu mimi mwenyewe na kumpeleka Hospitali ya Regecy.
Nilikutana na dokta Chale.
Baada ya dokta kumfanyia vipimo aliniita ofisini mwake ili anipe majibu.
“Faraji majibu nitakayokupa lazima ustahimili.” maneno ya dokta Chale yalinitisha.
Nikajiweka vizuri kitini kumsikiliza.
“Nieleze tu dokta haina shida”
“Iko hivi…”akaanza kunieleza.
“Mwanao amebemedwa.”
“Kubemendwa ndiyo nini?” nikauliza nikiwa makini sana.
“Kubemendwa ni hali ya mtoto kunyonya maziwa ya mama yake yaliyochanganyikana na mbegu za kiume, yanii manii.”
“Duu! Mbona hilo jambo geni inakuwaje mtoto anyonye maziwa yenye mbegu za kiume?” nikahoji.
“Ngoja nikufundishe kitu…” dokta Chale alisema, akajikohoza kidogo kisha akaanza kunieleza.
“Kitaalamu ndani ya manii au mbegu za kiume kuna vitu vikuu vinne. Protein, acid, chromosome na virus, nitakueleza kuhusu Acid kwa kuwa ndiyo kitu kilicholeta madhala kwa mwanao.
“Acid ni mfano wa tindikali, yaani kitu chenye ladha ya ukali mfano ndimu. Na kitu chenye tindikali kina kawaida ya kuunguza na pia kulegeza, ndiyo sababu kitaalam ukimlinganisha mwanamke aliyeolewa na asiyeolewa kisha akawa hafanyizinaa maumbile yao yanatofautiana,” alisema kisha akaendelea:
“Yulealiyeolewa mwili wake unakuwa laini zaidi sababu ya acid inayopatikana ndani ya manii.Nitakupa mifano mingi iliyo hai ili akili yakoikubali kwamba mwanao amenyonya maziwa ya mama yake yaliyochanganyikana na manii ya mwanaume asiye baba yake.
“Ukitaka kuthibitisha zaidi acid katika manii kuwa inaunguza nakulegeza, ukiwa na kidonda kibichi jaribu kutia manii, kidonda kitauma mara mbili zaidi kwa sababu ya acid.
“Mfano mwingine tazama kwa wale watoto wa kiume ambao wanaingiliwa kinyume na maumbile (mashoga) hata kama zamani alikuwa strong kiasi gani akiingiliwa tu, basi analegea kuanzia kutembea, kuzungumza na kila kitu,sababu ni Acid inayopatikana ndani ya manii.Ndiyo maana tunashauri kutomuingilia mwanamke anayenyonyesha sababu ukimuingilia ukamuingizia manii ambayo yana acid, acid ile itapanda katika matiti na kuyaharibu maziwa na hapo mtoto akinyonya atanyonya maziwa yenye acid. Hali hiyo, itasababisha mtoto kuwa katika hali kama aliyonayo sasa.
“Lakini kama atakula acid ya baba yake hatadhurika sana,sababu atakula acid ambayo kwa asili ndiyo iliyomtengeneza.
“Ilamwanamke akiziniwa na mtu mwingine mtoto ataathirika sana kama huyu wako na pengine itakuwa ni sababu ya kifo chake, kwa kuwa amekula acid ambayo siya asili kutoka kwa wazazi wake.
“Mungu wangu!....” nilihamaki.
“Kwa hiyo unataka kuniambia mke wangu anatoka na mwanaume mwingine?” niliuliza swali la kibwege.
“Sijasema hivyo.”
“Sasa?”
“Inawezekana wewe ndio ukawa tatizo.”
“Kivipi?”
“Labda mtoto huyu si wako ndio maana mbegu zako za kiume zinamuharibu,” kauli ile ya dokta ilizidi kunikata maini.
Sasa nikawa kwenye mkandamizo wa mambo mawili, aidha mke wangu anaye mwanaume mwingine ambaye anazini naye kiasi cha kumuharibu mtoto, au mimi nikawa si baba wa mtoto yule na ndiye ninaye muharibu.
Nilijikuta katika hali mbaya sana kifikra.
“Najua hali unayopitia Faraji,” dokta akanishitua baada ya ukimya mfupi kupita kati yetu.

“Nitachukua sample ya damu yako na ya mwanao ili niwapime DNA tuone kama damu zenu zina-match ili tujue kama wewe ni chanzo cha mtoto kuwa hivi ama kuna mpumbavu mwingine anayetuharibia mtoto,” aliniambia.

Sikuwa na sababu ya kukataa ushauri ule, Dk Chale alichukua damu zetu. Kisha akaenda kuzifanyia vipimo, masaa saba badaye akanipa majibu.

Majibu yalionyesha DNA yangu na ya mtoto ziliendana.Kwa hiyo jawabu lilikuwa ni moja. Mke wangu alikuwa akitoka kimapenzi na mwanaume mwingine kiasi cha kumuharibu mtoto wetu.



NJOO Kesho tuendelee kusoma kisa hiki.…

UKITAKA KITABU NICHEKI KWA 0687750295...
 
DAMU YA MWANAMWALI...
SEHEMU YA 8
MTUNZI: ALLY KATALAMBULA
SIMU: 0687750295
ILIPOISHIA..
Majibu yalionyesha DNA yangu na ya mtoto ziliendana.Kwa hiyo jawabu lilikuwa ni moja. Mke wangu alikuwa akitoka kimapenzi na mwanaume mwingine kiasi cha mbegu zake kumuharibu mwanangu.
SONGA NAYO...
JAMBO lile liliniumiza sana, kila nilivyokuwa nikimfikiria mke wangu, sikuamini kama kiumbe yule aliyekuwa mpole na msikivu kama njiwa angeweza kufanya ushenzi wa namna ile, kitendo cha kunisaliti na kumbemenda mtoto wangu kiliniuma sana.
Niliporejea nyumbani, nilimkuta akiwa sebuleni, muda wote alikuwa bize Facebook, Whatsapp, na Instagram. Aliponiona alikuja kunipokea mtoto.
“Vipi mmepata matibabu?” aliniuliza huku akimchukua mtoto.
“Njoo chumbani,” nilimwambia bila kujibu swali lake.
Tuliongozana hadi chumbani mtoto tukimwacha mikononi kwa dada wa kazi. Doreen.
“Mke wangu,” nilimwita tukiwa chumbani.
“Bee.”
“Ungependa kuona maisha ya mwanao yakishia kulelewa na baba au mama wa kambo?”
“Kivipi mume wangu?”
“Sikutoshelezi kimapenzi?”
“Mbona sikualewi?
“Tupo wanaume wangapi tunaokuvua nguo yako ya ndani?”
“Heeee!!!” alihamaki baada ya swali hilo.
“Nakuuliza tena, tupo wanaume wangapi tunaokuvua nguo yako ya ndani?”
“Faraji naomba unitake radhi,” akaniambia kwa ukali.
Nilinyamaza nikavuta pumzi, donge zito lilinikaba kooni, nilimsimulia mambo yote niliyoelezwa na daktari.
Habari ile ilimshitua sana mke wangu, lakini bado uso wake uliendelea kuonesha ni kiumbe asiyekuwa na hatia yoyote maishani.
“Faraji kama umenichoka niambie, lakini siyo kwa kunitafutia sababu namna hii” hatimaye akaniambia.
“Kukutafutia sababu?”
“Ndiyo, unanitafutia sababu.”
“Kwa taarifa yako, hili siyo jambo la kwanza kuelezwa juu ya uhuni ufanyao…” nikasema nikiwa nimemkazia macho.
“Wakati unajifungua ulijisaidia sana haja kubwa kitandani, na madaktari husema hali hiyo huwatokea wanawake wanaojihusisha na ngono kinyume na maumbile,” nilimpasualia.
“Faraji shika adabu yako,” aliniambia kwa ukali.
“Sasa niambie ni lini nilikuingia kinyume na maumbile?”
“Unikome!!” alisema
Nikamchapa kibao. Akabweka kama jibwa koko. Bila kutegemea akanivaa akiwa amechanua vidole vyake na kuniparua usoni kwa makucha.
Hasira zilinipanda nikamtandika kofi jingine usoni. Kilichofuata baada ya hapo ulikuwa ni ugomvi mkubwa sana.
Songombingo lile likawakusanya majirani ambao walikuja hadi chumbani kutuamulia, mke wangu alikuwa na hasira za mbogo akaanza kupasua vitu vya ndani hovyo.
Wakati huo mwanangu asiyejua lolote alikuwa akilia muda wote. Ghafla ndoa ikawa chungu kama shubiri.
Mtoto alikuwa akilia bila kujua chochote, mke wangu naye akaendelea kupiga kelele za kilio huku akipasua vioo vya magari. Vituko vile vilizidi kunitia ghadhabu, watu wakaendelea kunisihi niwe mtulivu.
Wanaume watatu akiwemo mwenyekiti wa mtaa, wakamkamata mke wangu na kumdhibiti. Wakati huo watu walikuwa wamefurika nyumbani kwangu wakijionea video ya bure. Kwakweli mambo yale yalinifedhehesha mno.
Baada ya mke wangu kutulizwa na kutulia, na kutokana na utitiri wa watu kufurika nyumbani kwangu, kilichofanyika ni kuwaondoa ili taratibu zingine ziendelee.
Kwa msaada wa mwenyekiti wa mtaa, watu waliondolewa wakabakia wachache, mtoto naye aliyekuwa mikononi mwa dada wa kazi alikwishanyamaza kulia.
“Ni nini hasa tatizo?” mwenyekiti wa mtaa aliuliuliza baada ya utulivu.
Nilimweleza kwa kifupi kiongozi yule wa mtaa chanzo cha songombingo lile, alinisikiliza kwa makini maelezo yangu kisha akamgukia mke wangu ili naye atoe maelezo yake.
“Sina chochote cha kuzungumza zaidi ya kutaka talaka yangu,” alisema
“Eeh!.” mwenyekiti akahamaki.
“Ndiyo nataka talaka yangu, sijaolewa ili nipigwe,” akasisitiza.
“Unadhani hiyo ndiyo suluhu ya changamoto za ndoa?”
“Nimesema nataka talaka yangu, sitaki siasa,” mke wangu akasisitiza kwa jeuri.
Ndani ya muda huohuo mara mageti ya nyumba yakagongwa kwa nguvu. Watu wote tukabaki tukishangaa.
Mwenyekiti akasimama kwenda kufuangua, mara askari polisi wakaingia wakiwa wameongozana na shemeji yangu Aisha.
“Tumeambiwa kuna vita hapa?” afande mmoja akauliza.
“Hakuna vita afande, ilitokea sintofahamu kidogo lakini tumeimaliza,” mwenyekiti wa mtaa alijibu.
“Amenipiga, ameniumiza na damu zimevilia kwa ndani,” mke wangu alidakia, halafu palepale akaangusha kilio.
Watu wote wakapigwa na butwaa, wale polisi wakamgeukia mwenyekiti:
“We unasema hakuna vita wakati watu wanatoana ngeu?”
“Aagh…unajua mambo ya familia…”
“Faraji ni nani?” askari akauliza kwa ukali, hakuta kumsikiliza yule mwenyekiti.
“Huyu hapa” mke wangu akawaonyesha wale polisi kwa kunisonta.
“Mkamateni,” amri ikatoka. Nikakamatwa na polisi.
Nilipotaka kujieleza kwa wale mabwana, sikupewa nafasi hiyo, waliniburuza kwa nguvu hadi nje. Mtoto wangu mdogo akaanza kulia tena kwa uchungu.
Niliingizwa kwenye gari la polisi kama gaidi, kisha safari ya kituo cha polisi cha Oystabay ikaanza, nilijisikia uchungu sana kwa kile kilichokuwa kikinitokea. Nilijikuta namchukia sana mke wangu. Hasira dhidi yake ikawa kubwa.
Baada ya kufikishwa kituoni, sikuchukuliwa maelezo yoyote zaidi ya kutakiwa kuvua mkanda na viatu, pamoja na kukabidhi vitu vyangu, kisha nikaingizwa selo.
Tangu nizaliwe sikuwahi kuingia ‘lockup’ na sikudhani kama siku moja ningeingia sehemu mbaya kama ile. Mule ndani kulikuwa kunanuka mkojo na hewa ilikuwa nzito sana. Chawa na kunguni lile lilikuwa ni zizi lao.
Nikiwa mule ndani, nikaamini muda si mrefu marafiki na jamaa wangekuja kuniwekea dhamana endapo wangepata taarifa juu ya maswahibu yale.
Nusu saa ilipita bila kuona dalili zozote za kuchomoka, nilimwita askari aliyekuwa kaunta nikamuomba anisaidie kufanya mawasiliano na moja ya marafiki zangu ili wajue nipo kwenye madhila.
“Hata kama akipatikana mtu wa kukuwekea dhamana, kwa muda huu siyo rahisi kutoka,” yule askari aliniambia.
“Kwa nini?”
“Ni utaratibu tu, usiku huwa hatutoi dhamana.”
“Kwa hiyo nitalala humu hadi asubuhi?”
“Ndiyo maana yake.”
“Mungu wangu,” nilimaka.
Hata hivyo kabla sijawasiliana na jamaa yangu kwa ajili ya kumpa taarifa za kukamatwa kwangu, mwenyekiti wa mtaa alifika. Aliomba kuzungumza na mimi, kisha akasogea katika geti.
“Kesho utaachiwa…” aliniambia.
“Kweli leo haiwezikani?”
“Ndiyo, dhamana mara nyingi zinatolewa mchana siyo usiku, vinginevyo labda tutumie njia za panya” alisema, nikamwelewa hapo lazima rushwa utumike.
“Haina shida we waulize wanataka kiasi gani.”
“Basi subiri kidogo,” aliniambia.
Akatoka na kwenda kuzungumza na polisi, sikujua alimkabili nani ila muda mfupi badaye akarudi.
“Jamaa wanasema wanataka laki moja.”
“Haina neno, pesa siyo tatizo, ninachotaka ni kutoka tu humu.”
“Sasa hiyo pesa tunaipataje?”
“Pesa ipo kwenye simu, kama inawezekana mwambie afande akupe simu kisha nikupe Password ukafanye muamala wa hiyo fedha.”
“Sawa, nipe password” aliniambia. Nikamtajia nywila, kisha akaondoka tena.
Haukupita muda mrefu, yule mwenyekiti akawa amemaliza machakato wote wa kuwahonga wale polisi, niliachiwa usiku ule ule na kesi ile ikafutwa.
Walinisihi nisafanye fujo yoyote, wakanishauri ni kheri niachane na mwanamke yule kuliko kuendelea kuishi naye katika migogoro.
Niliwaitikia na kuondoka, nilikiwa sambamba na mwenyekiti yule wa mtaa, nilimshukuru sana yule kiongozi kwa msaada alionipatia ingawa haukuwa uliozingatia misingi ya kisheria. Nikampa shilingi elfu 40 kama ahsante.
Naye aliniomba kwa usiku ule siyo vizuri kurudi nyumbani, kwakuwa bado mimi na mke wangu wote tulikuwa na hasira.
Ushauri wake niliuzingatia, na niliona unamashiko, nilichofanya ni kwenda katika hoteli moja na kupumzika usiku ule wote.
Asubuhi kulipokucha, nilikwenda kuoga na kupata supu nzuri kama kifuangua kinywa, nikajitahidi kusahau matukio yaliyotokea jana usiku ili kuweka kichwa change freshi. Lakini bado nafsi yangu ilikuwa nzito sana juu ya mke wangu.
Nilitamani sana nikae peke yangu hadi pale nafsi yangu itakapokuwa safi, lakini kwa kuwa nyaraka za dukani kwangu huwa zipo nyumbani na wasaa ule nilitakiwa kwenda ofisini kwangu, ilinibidi nirudi tu nyumbani.
Nilichukua tax hadi nyumbani, milango ilikuwa wazi hivyo nikapitiliza ndani, nyumba nzima ilikuwa kimya, niaendelea kuzipiga hatua, nilipokifa kwenye kijikorido cha kutokea sebuleni nikamsikia mke wangu akizungumza na simu, nikasita kuendelea kutembea baada ya kusikia maneno aliyokuwa akiyazungumza mke wangu simuni.
Nikatega sikio, jambo alilokuwa akiliongea na mtu wa upande wa pili, lilinitisha sana, mapigo yangu ya moyo yakanienda kasi hadi nikaogopa.
UKITAKA KITABU CHA SIMULIZI HII NICHEKI KWA NAMBA 0687750295
 
DAMU YA MWANAMWALI…
MTUNZI: ALLY KATALAMBULA
SEHEMU YA 9
SIMU: 0687750295
ILIPOISHIA…
Nikatega sikio, jambo alilokuwa akiliongea na mtu wa upande wa pili, lilinitisha sana, mapigo yangu ya moyo yakanienda kasi hadi nikaogopa.
SONGA NAYO..
SURA YA 5
NILIENDELEA kubana pale koridoni, mwili wote ukitetemeka. Mazungumzo kati ya mke wangu na mtu wa upande wa yalikuwa hivi:
“Mume wangu amegundua kama natoka nje ya ndoa,” alisema.
“Wacha wewe!” sauti ya mwanaume upande wa pili ikahamaki.
“Ndiyo, amekwishajua kila kitu.”
“Kajuaje. Ameona akaunti yako ya Facebook?”mtu yule akauliza.
“Hapana. Amejua kutokana na kuzorota kwa afya ya mwanangu. Kumbe ile michezo tuliyokuwa tukifanya ilikuwa sumu kwa mtoto”
“Kivipi?”
“Nilikuwa nikimbemenda…”
“Mimi si’ nilikwambia umwachishe ukabisha.”
“Sasa kama ningemwachisha, ningemwambiaje mume wangu?”
“Sababu ziko nyingi Nasra.” Jamaa alimwambia mke wangu, kimya kifupi kikapita, kisha wakaendelea na maongezi
“Sasa tunafanyaje?”
“Wallah Ally mie bado nakupenda,”maneno yale yalitoka kinywani mwa mke wangu.
“Najua, lakini hujapewa talaka bado.”
“Nitahakikisha wiki hii naipata hiyo talaka, nahitaji kushi na wewe Ally.”
Yalikuwa ni maneno mabaya sana kusikika masikioni mwangu, pale nilipokuwa nimesimama nilihisi kizunguzungu, nilijiona nipo angani naelea. Akili ilinizunguka.
Dunia kwangu ilikuwa kubwa mno. Nilijiona kiumbe mdogo mithili ya sisimizi. Nikiwa pale kiridoni, nikawaza, nimvae mke wangu na nimfanye kitu mbaya, ama nimpe talaka kisha niachane naye kiroho safi.
Wazo la kumwacha kwa amani, niliona nitakuwa siitendei haki nafsi yangu, nikaamini, hatua nzuri kabla ya kumwacha ni kumkomesha. Kadhalika. Nikaamini kumkomesha mke wangu peke yake ilihali yupo mjinga mwingine aliyenichoma kijiti jichoni, bila kumuadabisha nitakuwa nimeidhulumu nafsi yangu.
Kabla mke wangu hajashitukia uwepo wangu, nikanyata na kurudi nje, bahati nzuri hapakuwa na yeyote aliyeniona. Nilitembea kwa mguu hadi katika kituo cha madereva bodaboda, nikachukua usafiri huo, nikamtaka dereva anipelekea Mbezi Temboni.
Niliazimia kwenda Temboni kumwona jamaa yangu mmoja aitwaye Daniel Mwansasu, watu hupenda kufupisha jina lake na kumwita Dani, huyu alikuwa ni mtaalamu wa mambo ya ‘Information Technology’ (IT)ambaye alikuwa akifanya kazi ubalozi wa Urusi kama fundi.
Lengo la kumfuata huyu mtu nilitaka anisaidie kuingilia mawasiliano ya Facebook ya mke wangu (HACK), ili niweze kumtambua mtu niliyemjua kwa jina moja la Ally, niliamini ndiye kirusi kilicho iharibu ndoa yangu.
Baada ya kufika nyumbani kwa jamaa huyo, ambaye hadi wakati huo alikuwa akiishi nyumbani kwa wazazi wake, bahati nzuri nilimkuta, siku hiyo alikuwa ni ya mapumziko kazini kwake.
“Ooh! Faraji…” Dani alinilaki baada ya kuniona.
“Karibu, naona leo umenifanyia uvamizi wa kimyakimya”
“Ahsante sana Dani, nisamehe kwa kukuvamia.”
“Siyo kitu Faraji, karibu sana, pita ndani.”
Dani ni mtu mmoja mcheshi na makarimu sana, aliendelea kunikaribisha, usoni mwake akiwa katika tabasamu pana.
“Tangu uachane na ukapela umenitupa sana mwanao.”
“Hapana Dani, si kwa sababu nilioa, ni mihangaiko tu ya maisha.”
“Kweli, haya leta habari. Uso wako unaonesha unalo jambo tata sana,” Dani alisema.
“Ndiyo. Hujakosea Dani.”
“Kuna nini tena?”
Nilivuta pumzi, nikazitoa kwa nguvu, nikaanza kumuhadithia mkasa wote, nilimweleza kila kitu bila kumficha.
“Loh! Pole sana Faraji.”
“Ndiyo ukubwa, nimekwishapoa Dani.”
“Mimi naogopa sana ndoa, wanawake ni viumbe washenzi sana, hasa wanapozongwa na mihemko ya kiwendawazimu,” Dani alisema kwa kulalama, maswahibu yangu yalimgusa sana.
“Sana Dani,” nikashadadia.
“Ulikuwa kipofu Faraji, haya mambo ungekwishayatambua mapema tangu mama yako alipokuwa akikueleza.
“Ni kweli nilikuwa kipofu,” nilisema kwa huzuni.
“Kwa hiyo ulikuwa unataka msaada wa gani hasa?”
“Swali zuri…”nilimwambia, nikaendelea:
“Kwanza kabisa nataka niachane na huyu mwanamke, pili nataka niwakomeshe yeye na hawara wake.”
“Kuwakomeshaje?”
“Nataka niwadhalilishe.”
“Duh! Sasa mimi naingiaje hapo?”
“Kama nilivyokwambia, sijamtambua moja kwa moja mwanaume anayemzuzua mke wangu, lakini inavyoonyesha mawasiliano yao yapo zaidi facebook.”
“Kwa hiyo unataka ni-hack akaunti ya mkeo ili kumnasa huyu mtu?”
“Ndiyo. Hilo ndilo kubwa ninalolitaka kutoka kwako.”
“Usijali Faraji, hilo hesabu limekwisha, unajingine?”
“Hapana ni hilo hilo.”
Baada ya kuzungumza hayo, Dani alichukua laptop yake na kuanza kazi, aliingia kwenye ukurasa wa mke wangu, akachokonoa vile anavyojua yeye, dakika chache badaye, akaunti ile ikawa tunaweza kuiongoza tutakavyo.
“Kazi imekwisha, sasa unaweza kuona kila kitu unachotaka,” aliniambia huku akinisogezea laptop ile.
Upesi nikaingia sehemu ya jumbe katika akaunti ya facebook ya mke wangu, mke wangu alikuwa akipokea jumbe nyingi za wanaume wanaomtaka kimapenzi.
Wanaume waliokuwa wakimfutilia mtandaoni walikuwa ni wengi mno, mambo yale yalizidi kuniumiza sana. Bado niliendea kutafuta jina la mtu aitwaye Ally.
Nikiwa naendelea kutafuta jina hilo mara ujumbe ukaingia, ujumbe huo ulitumwa na mtu aitwaye Abdul Ally. Naam! Alikuwa ni mtu yule yule niliyekuwa nikimsaka, Ujumbe uliotumwa na mtu huyo, ulikuwa ni mapenzi. Ulisomeka hivi:
“Vipi mpenzi, unafanya nini sasa hivi? nitumie basi kapicha.”
Mate mepesi yalinijaa kinywani, ujumbe ule sikuujibu, nilichofanya ni kuingia kwenye ukurasa wa mtu huyo ili kumtambua vizuri.
“Mungu wangu!” nilipayuka baada ya kumwona mtu yule. Sikuamini macho yangu, nilihisi kutetemeka kwa hasira.
Mtu aliyekuwa akimzuzua mke wangu, alikuwa ni msanii wa muziki ambaye aliwahi kumtumia fedha miaka ya nyuma akitaka ashiriki kwenye video ya muziki.
Nikiwa bado katika taharuki ile. Mke wangu aliyekuwa ‘online’ nikaona anajibu ujumbe ule, akasema:
“Niko chumbani, nakuwaza tu wewe, nakutumia kapicha,” nikazidi kutetemeka. Sijakaa sawa, mara picha ikatumwa.
Picha iliyotumwa, ilikuwa ya kifua cha mke wangu, alikuwa mtupu, matiti nje, alijifotoa matiti yake, akamtumia picha hiyo kwa hawala wake.
Bila kutarajia, machozi yalinibubujika. nilihisi kifua kikiwaka moto kutokana na hasira, kitendo cha kusalitiwa na mwanamke yule, niliona ni uonevu mkubwa mno maishani.
Nikaendelea kufuatilia mawasiliano yao, nikaona namna mke wangu alivyokuwa amekolea kwenye penzi la jamaa yule.
Kila ambacho Ally alitaka kwa mke wangu, mwanamke huyo alitii. Walitumiana picha chafu kadiri walivyojisikia. Wakaambiana maneno yote ya kimapenzi vile walivyoweza. Mambo yote hayo niliyashuhudia kwa macho yangu mawili.
Kwa kweli niliumia mno, nakumbuka siku ile, nililia kama mtoto chumbani kwa rafiki yangu Dani. Uchungu nilioupata ulishinda hata ule msiba wa marehemu baba yangu.
“Pole sana Faraji,” Dani alisema huku akinishika bega.
“Waswahili husema, dunia tambara bovu. Mambo yote ambayo mkeo anakutendea ni matokeo ya ulimbukeni wa kutoutambua vema ulimwengu. Wajibu wako ni kumpuuza.”
“Kumpuuza!..” nilibweka kwa hasira.
“Nawezaje kupuuza tukio la kusalitiwa na mke wangu? Unajua uchungu wa mke wewe?”
“Mantiki ya kauli yangu sivyo hivyo Faraji bali….”
“Nisikilize Dani,”nilimkatisha. Uso uliniiva
“Nashukuru kwa msaada wako ndugu, nasikitika siwezi kusikiliza falsafa na siasa zozote juu ya hili, najua nitakachofanya,” nilisema. Nikasimama na kutoka nje.
Daniel ama Dani kama alivyopenda kuitwa, hakuwa na chochote cha kufanya kunituliza. Niliondoka na kuelekea Sinza. Muda mfupi badaye nilikuwa La_Charse Hoteli, bado nilikuwa kwenye mkanganyiko mkubwa sana.
Nikiwa pale, mhudumu alipofika mezani, nikaagiza maji ya Kilimanjaro ya baridi sana, yalipoletwa, nikayafakamia na kuyanywa yote, angalau nikahisi ahueni nafsini.
Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi, ilikuwa yapata saa saba kasoro mchana, hadi wakati huo, yalikuwa yamepita masaa 17 nikiwa sijatia chochote tumboni, njaa sikuisikia kutokana na mfululizo wa matukio yaliyonifanya niwe na mawazo muda wote.
Kwa kuwa niliazimia kuwafanyia kitu mbaya, mke wangu na hawala yake, nilianza kuseti mipango muda ule ule.
Nilimpigia simu mwandishi mashuhuri wa Gazeti la Uwazi, Issa Mnally, ili nimweleze kisanga chote sambamba na lengo la kuweka hadharani uchafu wote wa mke wangu na hawara yake ambaye, Ally.
Simu iliita muda mrefu bila kupokelewa. Sikuchoka. Nikapiga tena. Hali ikabaki vilevile, simu ya mwandishi yule haikupokewa.
Moyo ukaniuma mno kwa kutompata Issa, mwandishi asifikikaye kwa habari za kichunguzi, nikaona mipango ya fumanizi lile linaanza kuingia doa.
Nikajiuliza, sasa nifanyeje endapo sitampata mwandishi Issa na kutengeneza lile fumanizi? Nimwache mke wangu kiroho safi kwa kumpa talaka? Ama nitumie njia gani nyingine ya kumwadabisha?
Baada ya kufikiri kwa kina, bado nafsi yangu iligoma kabisa kumpa talaka mke wangu bila kumwachia maumivu maishani mwake.
“Sasa nimkomeshe vipi?” nikanong’ona peke yangu.
Suala la kuua. Hapana. Kuumua Nasra na hawara wake kungenisababishia misukosuko maishani. Wazo hilo nikalifutilia mbali. Sasa nifanye nini? Swali hili likaendelea kutembea kwenye kuta za ubongo wangu, bila majibu.
KITABU HIKI KIPO MTAANI, NI KITABU KIKUBWA CHA KURASA TAKRIBANI MIA TATU (300) BEI YAKE NI SHILINGI ELFU KUMI (10, 000/=)
Kamwe hutojuta kununua kitabu hiki.. Ni hadithi ya aina yake, usipotokwa na machozi baada ya kumaliza kusoma kitabu hiki, basi hutolia kwa jambo lolote lile maishani, ni hadithi itakayokuacha na funzo kubwa.
Kumbuka: Riwaya hii iliwahi kufanya vizuri kwenye gazeti la Champion toleo la kila ijumaa
Nicheki kwa namba 0687750295 utaletewa nakala ya kitabu hiki hadi mlangoni (Kwa wasomaji wa hapa Dar tu.)

KWA WASOMAJI WA MIKOANI.
Wasomaji wa mikoani mtatumiwa nakala kwa njia ya basi, baada ya kuwa umekwisha wasiliana na mimi (Ally Katalambula) kwa namba yangu hapo juu. Na nitakutumia nakala yako ambayo utaipokea kwenye ofisi za basi husika (Nauli ya basi ni elfu 5 ambayo ni juu yako)
Vinginevyo kama unaye ndugu ama mtu wa karibu hapa mjini Dar unaweza kuniunganisha naye, nikampa nakala yako.
 
DAMU YA MWANAMWALI
MTUNZI: ALLY KATALAMBULA
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA
Baada ya kufikiri kwa kina, bado nafsi yangu iligoma kabisa kumpa talaka mke wangu bila kumwachia maumivu maishani mwake.
“Sasa nimkomeshe vipi?” nikanong’ona peke yangu.
Suala la kuua nikakiri lingenisababishia misukosuko maishani, hivyo nikalifutilia mbali. Sasa nifanye nini? Swali hili likaendelea kutembea kwenye kuta za ubongo wanguu.
SASA ENDELEA NAYO...
Akili ilichoka. Muda ulizidi kwenda bila kupata majibu. Nilimwita mhudumu wa jikoni na kumtaka anitayarishie ugali wa dona na nyama choma, nikaendelea kufikiri ni kitu gani nimfanye mwanamke yule.
Muda mfupi badaye, chakula kilikuwa tayari, wakati mhudumu ananinawisha maji, mara simu yangu iliita, nilipocheki kwenye kioo cha simu, mpigaji alikuwa ni Issa, mwandishi wa gazeti.
Niliinyakua simu na kuweka sikioni.
“Mnally.”
“Nambie bosi.”
“Nakutafuta sana. Hupokei simu yangu.”
“Samahani aisee, nilikuwa kikaoni.”
“Ninayo habari.”
“Acha wewe! Habari gani?”
“Njoo La_Charse, ni stori nyeti, siyo ya kuongelea kwenye simu.”
“Nidokeze kwa ufupi ili nimshirikishe mhariri wangu.”
“Ni habari ya fumanizi”
“Acha wewe!” Issa alimaka. Mwandishi yule anapenda sana habari za namna ile.
“Ndiyo ukweli wenyewe.”
“Nani tena?”
“Mke wangu”
“Shemeji huyuhuyu!!”
“Hakuna mwingine”nilimwambia.
Kwa mbali nilimsikia mwandishi yule akizidi kifurahia kupata habari ile ambayo ingemfanya apate sifa kemkem kwa uhodari wake.
Baada ya kukata simu. Nilianza kukishmbulia kile chakula. Dakika chache badaye, Issa aliwasili, alikuwa ameongozana na mwandishi mwenzie, ambaye alinitambulisha kuwa ni ‘partner’ wake kwenye kazi zao.
Nilimsimulia mwandishi yule mwanzo mwisho. Nikamwonyesha picha na ‘screenshort’ za mazungumzo kati ya mke wangu na hawala yake.
“ Wamepanga kukutana lini kwa ajili ya kufanya uchafu wao?” hatimaye Issa aliniuliza baada ya kutumia muda mwingi kunisikiliza.
“Kwa mujibu wa mazungumzo yao inaonesha ni kesho saa nne.”
“Wapi?”
“Kuna lodge moja inaitwa Madrid, ipo Kinondoni Studio, jirani na anapoishi mzee Beka Mfaume”
“Sasa nisikilize…” alisema, akaendelea.
Kuanzia sasa, unachotakiwa kufanya ni kutomuonyesha kama kuna mpango umeusuka.
“Na itabidi kuanzia kesho asubuhi tutakuwa mitaa yako kuweka kambi ili kufuatilia nyendo zote za mkeo bila kumpoteza hata point moja”
“Sawa”
Tukakubaliana. Tukazungumza mawili matatu, kisha tukaagana. Wakati huo ilikuwa imetimu saa kumi na mbili jioni.
Nilichukua usafiri wa bodaboda nikarudi nyumbani, nilimkuta mke wangu akiwa ameketi sofani, alikuwa bize na simu kama ilivyo kawaida yake.
Nilizidi kuugulia ndani kwa ndani kwa kuamini wasaa ule mwanamke yule alikuwa akichati na hawara yake. Nilitamani nimvae kisha nifanye kitu mbaya, lakini sauti moja kichwani ilinisii kutofanya hivyo.
Pamoja na kuniona nimeingia, wala hakunijali, si salamu wala kujishughulisha na chochote. Yeye na simu, simu na yeye.
Nilipitiliza hadi chumbani, nikaoga na kubadili nguo, nikarudi sebuleni ambako niliuacha.
Nilimkuta akiendelea kucheza na simu yake, hakunisemesha chochote, mimi pia sikumsemesha lolote.
Masaa machache badaye, nilitayarishiwa chakula na dada wa kazi. Niliona yamesalia masaa machache kabla ya kukamilika kwa tukio baya na la aibu nililopanga kumtendea mwanamke yule na hawala wake.
Nilisahau kabisa methali isemayo: Jambo isilolijua ni sawa na usiku wa giza.
Wakati nakula, mke wangu aliendelea kuwa bize na simu yake, akawa anatabasamu, wakati mwingine anaachia kicheko kidogo. Alionekana ni mwenye kufurahishwa na jambo kwenye simu.
Roho iliniuma sana, niliamini kivyovyote mke wangu alikuwa akichati na hawara wake. Chakula nilichokuwa nikila, hakikupita kooni. Kwa mara nyingine nikatamani nimrarue mwanamke huyu, hata hivyo malaika wa hekima walikuwa wamenizingira.
Nikaendelea kula kwa tabu, baada ya kuonjaonja ule msosi, nikasimama na kuelekea zangu chumbani. Nikamuacha akiendelea kutesa na simu yake.
Nilipofika chumbani, nilijitupa kitandani nikawa nawaza hili na lile, katika kuwazawaza huko, nikakumbuka kuna kipindi mama aliwahi kuonesha hali ya kutovutiwa kwa mimi kumuoa huyu mwanamke, japokuwa fursa ya kunitafutia mke, niliwapa wao.
Je, mama aliwahi kuijua tabia ya umalaya aliyonayo mke wangu? Na kama aliwahi kujua kwa nini alikubali nimuoe huyu mrembo?
Fikra hizi zikachochea dhamira ya kuwasiliana na mama, ili anipe majibu ya utata huu. Nilipiga namba ya mama na kuweka simu sikioni. Simu iliita, muda mfupi ikapokelewa.
“Halo!”
“Asalam aleykum mama,” nilimsalimu.
“Waleykum salam, mwajionaje huko?”
“Mungu anasaidia….”nilimuitikia kinyonge kisha nikaendelea:
“Ninalo jambo ningependa nikuulize.”
“Jambo gani baba?” aliniuliza kwa shauku, nikasikia akipunguza sauti ya televisheni ili kuyapa nafasi mazungumzo yetu.
“Unakumbuka kuna siku uliwahi kunieleza kwamba Nasra alikuwa ni chaguo la baba ila wewe hukufurashishwa naye, unakumbuka?” nilisema. Nikapiga kimya kusubiri jibu.
“Endelea kueleza baba nakusikiliza…”
“Unakumbuka?” nikakazia swali langu
Mama akashindwa kujibu. Nadhani alihisi huenda mimi na Nasra tunataka kumsuta, alitambua mimi kwa Nasra sijiwezi.
“Sikumbuki,” akasema kwa sauti iliyooneshwa kukarahishwa na mazungumzo yale.
“Mama nina matatizo makubwa kwenye ndoa hii, niambie tafadhali, kwa nini Nasra hakuwa chaguo lako?”
“Kuna matatizo gani kwani?” badala ya kujibu, naye akaniuliza.
Nilikuwa sijamweleza matatizo yanayoisibu ndoa yangu. Nilichofanya ni kumsimulia songombingo lote.
Nilipoweka kituo. Mama alishusha pumzi nyingi, akaonekana kuguswa na maswahibu yale.
“Pole mwanangu ndiyo ukubwa huo.”
“Ahsante mama.”
“Sasa umepanga kufanya nini?”
“Hata sijui,” nilimdanganya sikutaka kumwambia nimesuka mpango wa kumfumania na kumfotoa picha zitakazopamba ukurasa wa mbele wa Gazeti la Uwazi
“Hujui cha kufanya?” akauliza tena .
“Kabisa.”
“Basi wewe naye una matatizo?”
“Kivipi mama?”
“Siku zote, tatizo lina pande mbili, upande wa chanzo na upande wa suluhu, ikitokea tatizo halafu ukabaki katikati ya chanzo na suluhu, basi na wewe ni sehemu ya tatizo.”
Kauli ya mama yangu ilinikata maini, ni kama vile alikuwa akinisuta, nawezaje kujua chanzo cha mke wangu kukengeuka na kushindwa kutatua tatizo hilo.
“Halo” aliniita baada ya kuona kimya.
“Nakusikiliza mama,”nilisema kwa huzuni.
“Kesho asubuhi nitafute nikueleze kwa nini huyo mwanamke wako hakuwa chaguo langu,” mama alisema. Tuliagana, akakata simu.
Nilipogeuka nyuma, kumbe mke wangu alikuwa akinisikiliza mazungumzo yangu na mama, alikuwa akiniangalia huku amefura kama kiboko. Akachia msonyo mrefu halafu akaelekea bafuni.
Kitendo cha kusonywa na Nasra kilifanya joto la mwili liongezeke, hasira kali zilinipanda, dharau za kiwango hiki zilinielemea.
Nilimtazama kwa chati kiumbe huyu akiwa anashilizia maliwato, kimoyomoyo nikasema, dawa yako inakaribia kuiva Mwarabu koko wewe.
Baada ya kutoka bafuni, hakukaa chumbani, akarudi sebuleni, huko akaendelea kuchati, sikumbuki usingizi ulinipitia baada ya muda gani, lakini kulipokucha nilijikuta niko peke yangu kitandani. Mke wangu hakuwepo. Nikatambua atakuwa alilala sebuleni.
Ilikuwa inaelekea kuwa saa mbili kamili, nilijiandaa ‘chapchapu’ nikapata kifungua kinywa, nikachukua funguo za gari, nikatoka kuelekea ofisini kwangu.
Nikiwa umbali kidogo na mji wangu, Issa akanipigia simu
“Mkuu tupo kwako hapa.”
“Mmekwishafika?”
“Zamani za kale,” akajibu kwa kujidai.
“Kwa hiyo, ndiyo mnaanza kufuatilia nyendo zake?”
“Ndiyo maana yake, jambo la muhimu jitahidi uwepo na wewe sehemu ya tukio.”
“Naanzaje kukosa sasa? Acha niwahi ofisini kisha niache maagizo halafu nirudi tuungane kwenye hiyo operation.”
Baada ya kuelezana hayo, nikaongeza spidi ya gari, muda mfupi baadaye nilikuwa kwenye maduka yangu, nilikuta vijana wangu wamekwishafungua na wanaendelea na kazi, nilipitia taarifa za hapa na pale za mauzo, nikiwa katika kupitia pitia, simu ya Issa ikaingia tena.
“Mkuu,” nilipokea.
“Nisikilize kwa makinii….”Issa alisema kwa wahaka.`
“Ndiyo, nakusikiliza.”
“Mkeo ndio anatoka, tena amejipodoa balabala, we jamaa una mke mrembo sana.”
“Anakwenda wapi?” nikajikuta nimeuliza swali la kijinga. Tumbo lilipata joto.
“Atakuwa ndiyo anakwenda gesti huyu,” kauli ya Issa ilinigusa hadi ubongoni, nikahisi kifua chote kikiwaka moto, akili ikanizunguka.
“Kweli?”
“Haki ya mama tena!”
“Mmefika wapi?”
“Tupo Mkwajuni hapa, anachukua bodaboda, nasi tupo nyuma yake, hatuko mbali naye.”
“Hakikisheni hamfanyi kosa lolote litakalopeleka kumpoteza.”
“Hilo kosa kwetu ni dhambi, na huwa halipo,” Issa aliongea kwa mbwembwe, katika namna ya kunionesha alivyo mahiri kwenye habari za kichunguzi.
Wakati simu ya Issa anakatika simu ya mama nayo ikaingia! Nikakumbuka jana tulikubaliana kuzungumza, ili anieleze kwa nini hakufurahishwa na ndoa kati yangu na Nasra ilihali yeye na baba ndio waliohusika kuniolea mwanamke huyu.
“Halo mama.”
“Asalama aleykum,” alinisalimu.
“Waleykum salama mama, mzima?”
Kabla sijajibu nikaona Issa ananipigia, nilichofanya ni kuihold simu ya mama na kupokea ya Issa.
“Nambie Issa?”
“Mkeo amefika gesti, yupo na hawara wake.”
“Eeeeh!!” nilihamaki
“Ndiyo, kafika yupo na bwana wake, fika fasta basi eneo la tukio tumalize kazi,” Issa alisisitiza, nilihisi kitu ndani ya kifua changu kikilipuka kama bomu.
KITABU HIKI KIPO MTAANI, NI KITABU KIKUBWA CHA KURASA TAKRIBANI MIA TATU (300) BEI YAKE NI SHILINGI ELFU KUMI (10, 000/=)
Kamwe hutojuta kununua kitabu hiki, ni hadithi ya aina yake, usipotokwa na machozi baada ya kumaliza kusoma kitabu hiki, basi hutolia kwa jambo lolote lile maishani, ni hadithi itakayokuacha na funzo kubwa.
Nicheki kwa namba 0687750295 utaletewa hadi mlangoni kwa wasomaji wa hapa dar.

KWA WASOMAJI WA MIKOANI.
Wasomaji wa mikoani mtatumiwa nakala kwa njia ya basi, baada ya kuwa umekwisha wasiliana na mimi (Ally Katalambula) kwa namba yangu hapo juu. Na nitakutumia nakala yako ambayo utaipokea kwenye ofisi za basi husika (Nauli ya basi ni elfu 5 ambayo ni juu yako)
Vinginevyo kama unaye ndugu ama mtu wa karibu hapa mjini Dar unaweza kuniunganisha naye, nikampa nakala yako.
 
Back
Top Bottom