Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 8, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,545
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Wetu
  MwanaHALISI

  RAIS mstaafu Benjamin Mkapa, aliyetegemea mno nchi wafadhili kuongoza serikali kipindi chote alichodumu Ikulu, analalamika.
  Anawatupia lawama wafadhili walewale ambao baada ya kumuinua hadi kuonekana kiongozi mzuri kabla ya kubadilika alipoingia muhula wa pili, alidiriki kubeza wataalamu wazalendo na kuwasifia wa nje.
  Hoja yake kwa wafadhili ni kwamba hawataki kusaidia elimu ya juu, bali tu ya msingi, katika nchi zinazoendelea. Msimamo huo wa wafadhili,
  Anatoa hoja kwamba mtiririko wa maendeleo unatimia kwa kuunganisha elimu ya sekondari na elimu ya juu. Hapo ndipo panajenga msingi wa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
  Mkapa anasema nchi masikini, akimaanisha na kuijumuisha Tanzania, zinachelewa kupiga hatua ya maendeleo kwa sababu hazisaidiwi na wafadhili kutekeleza programu za kujenga wataalamu.
  Wataalamu hao wanapatikana tu kwa kufundisha vijana wa nchi hizo kada mbalimbali za kitaaluma kwenye ngazi ya shahada hadi udaktari wa falsafa.
  Yeye anaona kusaidia programu hizo kungechochea maendeleo makubwa kwani, anasema, elimu ya juu inatangamana mno na maendeleo ya sekta mbalimbali.
  Ninavyofahamu wafadhili ndio waliomsaidia Mkapa kutekeleza mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na wa sekondari (MMES) uliobuniwa wakati wa uongozi wake na utekelezaji kuendelezwa alipostaafu.
  Shule nyingi zilijengwa nchini. Bali nyingi zilikosa madawati na vifaa muhimu. Wala hakukuwa na utashi wa kutazama na kuongeza maslahi ya walimu hadi leo.
  Hii ilichangia kwa kiwango kikubwa walimu kupunguza imani juu ya serikali yao; na hatimaye wakaanza kutafuta maisha bora huku wakitafuta njia za kudai haki zao.
  Walimu wasio maslahi mazuri; wasiokuwa na nyumba bora za kuishi pale wanapofundisha; na wanaodai malimbikizo mengi ya fedha za likizo na kupanda madaraja, watafundishaje kwa utulivu?
  Udhaifu katika mipango ile umebebesha serikali mzigo mkubwa. Tatizo la madeni ya walimu kwa mwajiri wao, serikali, linaendelea kuinyanyasa serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Bila ya shaka mbali na kushusha ufanisi katika ufundishaji, limeitikisa serikali.
  Hivi Mkapa alitolea wapi kilio cha kutaka wafadhili wasaidie elimu ya juu. Hatukumsikia akilalamika kwa hilo. Lakini ipo kazi aliifanya tena kwa nguvu kubwa na gharama nyingi. Kutangaza utandawazi na mikakati ya ujasiriamali ambao haujamtoa Mtanzania mnyonge katika umasikini.
  Mkapa alidiriki hata kualika kwa fedha za Watanzania wanyonge, aliyemuita mtaalamu kutoka visiwa vya Caribbean, kwa ajili ya kuja kujenga mtandao wa kuendeleza sera zake hizo.
  Matokeo ya mtaalamu yule, ni kilichokuja kuitwa MKURABITA, mpango wa kurasimisha mali za Watanzania – mamilioni ya wanyonge wanaohangaikia kula yao.
  Mpango huo ulichozalisha ni kuorodhesha mali na miradi midogo ya wananchi lakini badala ya kuiwezesha, kumbe ilikuwa ni mpango wa kuhakikisha kila mmoja analipa kodi kupitia kwayo.
  Lakini pili, hivi alitaka asaidiwe nini hasa? Anakusudia wafadhili wangetoa fedha za kudhamini vijana wa Tanzania wakasomee taaluma mbalimbali ngazi ya shahada nje ya nchi?
  Kama hivyo ndivyo, najiuliza vile vyuo vikuu vilivyokuwepo na vingine vilivyochipuka baada ya vyuo mbalimbali kupandishwa hadhi, vingekuwa vya kazi gani iwapo wafadhili wangeingia kugharamia masomo ya Watanzania nje ya nchi?
  Isitoshe, Mkapa amesahau kwamba alikosea (sana) kushughulikia mambo yake binafsi alipoingia muhula wa pili wa uongozi na hivyo kukandamiza misingi mizuri ya ukuaji wa uchumi wa taifa aliyoijenga katika miaka mitano ya kwanza.
  Kwa namna alivyofanikiwa kuongeza mapato ya serikali, Mkapa alijikuta akiachia wasaidizi wake na rafiki zake watafune nchi kwa sababu hakukuwa na wa kuwahoji. Mteuzi wao ala, wao watendeje? Wangoje nini?
  Laiti Mkapa angetumia vizuri mapato asingelalamikia wafadhili ambao wana haki ya kuishika shingo serikali wanayoisaidia bajeti hata asilimia 40 tangu akiwepo Ikulu.
  Na Mkapa angefanya hivyo, angeondoka na hadhi kubwa kama kiongozi muadilifu aliyepata kuongoza Tanzania. Alishindwa kazi akageuka wananchi.
  Mipango yake mingi ililenga kujinufaisha na familia na rafiki zake. Ndio maana leo ninaamini anajisikia fedheha kuzungumzia hadharani kinachoitwa “uongizi adilifu” na kubaki tu kupasapasa tena akiwa kwenye hafla zisizokuwa na waandishi wachokonozi.
  Ndio kusema Mkapa siku hizi anakwepa vyombo vya habari makini kwa kujua atalazimika kukabili maswali magumu yanayoendelea kuhangaisha Watanzania.
  Pale anapojitokeza katika baadhi ya mikutano ya kijamii, anazungumza kwa ufupi huku akipinda kujitoa kwa umma. Watu wenye akili wanatamani kumbana aseme kwanini aligeuka wananchi katika awamu ya mwisho ya uongozi wake.
  Hadi sasa hajathubutu kujieleza vizuri kuhusu tuhuma zinazomkabili za kukiuka maadili ya uongozi. Anatuhumiwa kuwa aliunda kampuni binafsi na akajiuzia kifisadi mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.
  Aibu gani kukuta mgodi ulioridhiwa utolewe kwa sekta binafsi kwa zaidi ya Sh. 200 bilioni, utolewe kwa Sh. 70 milioni?
  Lakini hili lilifanyika mbele ya macho ya Mkapa tena katika kiti cha Rais wa Tanzania. Kibaya zaidi alihusika yeye na mmoja wa mawaziri wake vipenzi, Daniel Yona.
  Inasikitisha kuona rais mstaafu akitamba kuwa anavyo baadhi ya vigezo vya kuwa kiongozi bora. Ni kama vile anaota kuwa anafaa kutunukiwa tuzo ya taasisi ya Mo Ibrahim ambayo imekosa mshindi mwaka huu wa 2009.
  Mo Ibrahim wamesema wazi kwamba wamekosa kiongozi mstaafu barani Afrika wa kufaa kumtunuku tuzo hiyo. Ikabaki kapuni kwani haikumpata aliyefanana na Joachim Chissano wa Msumbiji na Festus Mogae wa Botswana.
  Hawa, tofauti na Mkapa, walitumikia watu wao kwa uadilifu mkubwa. Waliwajali na kiuwathamini. Walijua wajibu wao ni kuwatumikia tu washibe, wapate elimu nzuri, wafanye shughuli za uzalishaji kwa urahisi zaidi.
  Chissano na Mogae walionyesha uongozi uliotukuka. Walizuia rushwa kushamiri. Ilipotokea walikasirika na kubana wahusika. Walitumia vizuri raslimali za nchi; lengo likiwa kunufaisha watu.
  Mkapa angethibitisha uongozi bora iwapo angefuata nyayo zao. Alikuwa nayo nafasi. Aliitupa. Akaamua kuzonga mambo. Inauma.
  Matokeo yake, alishindwa hata na John Kuffour wa Ghana, Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Olusegun Obasanjo wa Nigeria waliofikiriwa wangetuzwa na Mo Ibrahim.
  Tumweleweje anapotaja vigezo vya kiongozi bora leo wakati hakuvipata alipopewa nafasi ya kuongoza taifa.
  Vizuri atoke hadharani na kuungama; wala siyo kwa kusema anamuachia Mungu. Muumba anaombwa msamaha. Lakini Mkapa anapaswa kuomba msamaha kwanza kwa Watanzania aliowaangusha kiuongozi.
  Sijui, labda anayo majuto. Anajuta kweli huyu? Hapana. Bado hatujathibitisha. Lazima akiri alivohusika.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Yaani nimechoka kabisa kusikia
  mkapa anasema nini,
  as far as i am concern,he is irrelevant...
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kuna bolt fulani za kichwa zikigongwa zikalegea mtu unaanza kukosa consistency.Mkapa mbona kama simuelewi elewi anayoyasema au ni vyombo vya habari vinamnukuu vibaya.
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mwacheni Mzee Mkapa apumzike...
   
 5. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mwanahalisi nalo ni gazeti la JK. Kwa hiyo sishangai sana kuona wanatoa makosa wengine tu, mwenye gazeti lake wanamwacha!
   
 6. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  watanzania tugange ya jayo,
  huyo Mkapa hapelekwei mahakamani, na hakuna mtu atakaye jaribu.
  kila siku ben, ben, ben sasa tumechoka...tuangalie mambo ya nchi yetu yanayotukabili sasa.
   
 7. O

  Omr JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapemba mamesha mroga huyo
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,545
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Mwalimu aling'atuka miaka 24 iliyopita na alifariki miaka 10 iliyopita na hadi hii leo bado tunajadili mambo mbali mbali kuhusu Mwalimu.

  Hivyo huyu Mkapa naye whether anafikishwa mahakamani kwa ufisadi wake alioufanya alipokuwa madarakani or not, Watanzania tutaendelea kumjadili Mkapa kwa miaka chungu nzima ijayo na tuna haki ya kufanya hivyo
   
 9. M

  Mtukufu Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nasema hivi wanaosema Mkapa aachwe apumzike wanakose kwanin nani amempa kazi? Na vile vile vile lazima tutumie usomi wetu vizuri na taaluma zetu sawa sawa kwamba kila baada ya kazi kufanyika lazima tufanye analysis na kwa maana hiyo lazima tuzungumze mpaka Yesu arudi na pia naomba niseme kuwa Mkapa kwa mazuri tutampongeza na kwa mabaya yake tutamponda ili kila aliyeko madarakani ajue kuwa baada ya kazi ni tathmin na matokeo ya kazi yake madarakani.
   
 10. M

  Mtukufu Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  China miaka ya nyuma baadhi ya viongozi wao walifanya makosa kama haya haya ya kina Mkapa matokeo yake leo hii wanaishia kunyongwa na wengine wanaishia kujiua kwa kujirusha kwenye miamba na kufa .
  MIMI NASEMA IKO SIKU INAKUJA KATIKA NCHI YETU AMBAPO WANAYOYAFANYA WENZETU TUTAYAFANYA NA SISI.
   
 11. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Yeye mwenyewe hataki kupumzika ndo maana anatoa kauli hizo. Kama anataka kupumzika, basi ajitokeze hadharani kukubali au kukanusha tuhuma zote zinazomkabili, and then anyamaze.
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  mwacheni apumzike.............kikwete nae tutamwacha atapumzika.
   
Loading...