Mkapa: Uongozi bora ni kuwa msikilizaji, mvumilivu na kupenda kusoma mambo ya ndani na nje ya nchi.

gillard

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
227
165
Mkapa amesema mambo ya kuzingatia ktk uongozi bora ni kuwa msikilizaji, mvumilivu na kupenda kusoma mambo ya ndani na nje ya nchi.
Mkapa aliyasema hayo kwenye kongamano maalum la maadhimisho ya kumbukuzi ya Mwalimu Nyerere.

Je hii huenda ni dalili kuwa atatoa kauli kumshauri au kumkemea Rais Magufuli? Tusubiri.....

Source MTANZANIA
 
Kuna kiongozi aliyekuwa na kiburi na dharau kama yeye? Hata haya mamikataba ya madini na rasilimali nyinginezo yanayopigiwa kelele kila siku yalianzia kwake. Au amesahau ya akina Balali na uchafu wa ajabu uliofanyika BoT enzi zake? What about Kiwira Coal Mine? Huyu naye akae tu kimya.
 
Kila Rais anayetoka madarakani lazima aone mapungufu ya aliyepo madarakani.

Tumeona Mwl Nyerere alivyokuwa anamshauri Mzee Rais Mwinyi.

Mzee Mwinyi hakutoa ushauri wowote kwa Mzee Mkapa.

Mzee Mkapa na Dr Kikwete hawakuwa kwenye good terms kiasi cha Mzee Mkapa kujiondoa kwenye Siasa na Public wakati wa utawala wa Dr Kikwete.

Kwa sasa Dr Magufuli amesema Hataki kusikia la MTU yoyote kwasababu anajiamini na inaweza na anajua anachokifanya na wote wanaompinga watajimaliza wao.

Na Hataki masihara kabisa ktk misimamo yake na mipango yake na yoyote asiyetii na bora akae pembeni.

Hawezi kuendelea kuona Mali za nchi hii zikinufaisha wachache na wengi wakiumia.
 
Mkapa amesema mambo ya kuzingatia ktk uongozi bora ni kuwa msikilizaji, mvumilivu na kupenda kusoma mambo ya ndani na nje ya nchi.
Mkapa aliyasema hayo kwenye kongamano maalum la maadhimisho ya kumbukuzi ya Mwalimu Nyerere.

Je hii huenda ni dalili kuwa atatoa kauli kumshauri au kumkemea Rais Magufuli? Tusubiri.....

Source MTANZANIA
Shida ya wanasiasa wetu kinachowaponza ni unafiki. Sasa hapo ukimuuliza mkapa alichokisema yeye alikifanya kipindi cha utawala wake? Au ndio kaongea tu ili ajiongezee umaarufu maana alishasahaulika.
 
Majitu mafupi huwa yana akili fupi sana hili nalo ni kushauri mtu lilienda Burundi matokeo yake wakalikataa kwa sababu ni jinga babe lina dharau kwanza limetuletea mikataba mibovu inatuumiza mpaka leo PUMBAVU MKAPA NA ULOFA WAKO Mbona ulishindwa kuwavumilia Wazanzibar matokeo yake ukatumia nguvu ya dola
 
Kuna kiongozi aliyekuwa na kiburi na dharau kama yeye? Hata haya mamikataba ya madini na rasilimali nyinginezo yanayopigiwa kelele kila siku yalianzia kwake. Au amesahau ya akina Balali na uchafu wa ajabu uliofanyika BoT enzi zake? What about Kiwira Coal Mine? Huyu naye akae tu kimya.
Tunapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa mkuu,,,kwan we hujui?
 
Shida ya wanasiasa wetu kinachowaponza ni unafiki. Sasa hapo ukimuuliza mkapa alichokisema yeye alikifanya kipindi cha utawala wake? Au ndio kaongea tu ili ajiongezee umaarufu maana alishasahaulika.

Hapo sasa, nakumbuka alikuwa jeuri sana kipindi chake.
Japo tofauti yeye mambo ya uchumi yalikuwa yanaonekana mwelekeo wake.
 
Kuna kiongozi aliyekuwa na kiburi na dharau kama yeye? Hata haya mamikataba ya madini na rasilimali nyinginezo yanayopigiwa kelele kila siku yalianzia kwake. Au amesahau ya akina Balali na uchafu wa ajabu uliofanyika BoT enzi zake? What about Kiwira Coal Mine? Huyu naye akae tu kimya.
Kiwira alijiuzia kwa milioni sabini tena kwa mkopo!!! Alipoingia kikwete akaleta jambajamba ya migodi naona wakamwambia mzee utaumbuka with due regard kikwete hakuwa mtu wake. Akaamua kujifanya eti ameurudisha mgodi serikalini kama uzalendo kumbe alistukia watu wangemkomalia!!!
 
Back
Top Bottom