MKAPA: Kikao cha kwanza cha mazungumzo ya amani Burundi, kufanyika Tanzania

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa ametangaza kwamba kikao cha kwanza cha mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi kitafanyika wiki ijayo.

Mkapa aliteuliwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki mapema mwezi uliopita kuwa mfanikishi wa mazungumzo ya kutatua mzozo wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisalia kuwa mpatanishi mkuu.

Mazungumzo ya kutafuta amani yalifeli mwishoni mwa mwaka jana baada ya upande wa serikali kusema hauwezi kuzungumza na watu waliohusika kwa njia moja au nyingine katika jaribio la mapinduzi la mwezi Mei mwaka jana.

Bw Mkapa ameandika kwenye Twitter kwamba wadau wote wanatarajia kuhudhuria kikao cha kwanza cha mazungumzo ambacho kitafanyika mjini Arusha kuanzia tarehe 2 Mei hadi 6 Mei.

"Nimepata idhini kutoka kwa Rais wangu, kiao changu cha kwanza cha Mashauriano ya Burundi kitakuwa mjini Arusha,” aliandika.

Ukosefu wa usalama umeendelea kuwa tatizo kuu nchini Burundi na visa vya watu kuuawa kiholela vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.

Chanzo: BBC
 
Fanya hivyo mheshimiwa tunaomba iwe haraka,watu wanaendelea kufa bila sababu huko burundi,juzi kamanda anampeleka mtoto shule na mkewe wote wakauliwa.mbaya sana
 
We on that shit now, Somalia better be ready...
Naiona Afrika Mashariki mpya!
 
Fanya hivyo mheshimiwa tunaomba iwe haraka,watu wanaendelea kufa bila sababu huko burundi,juzi kamanda anampeleka mtoto shule na mkewe wote wakauliwa.mbaya sana
Salute Salute.
Najisikia vyema kwamba kuna Watanzania bado wana utu. Kuna Watanzania wanafurahi mauaji kisa yuko upande anaoshabikia. Shame on them!
Life is invaluable. You made me feel good today.
Thank you!
 
Rejea Mgogoro wa Kenya 2007 alikuwepo, Zbar yupo pia.
Acha uongo Jk ndo aliyesuhisha mgogoro wa kenya na huko Znz alisuruhisha mgogo upi?maana tunavyojua yaliyofanyika Enji ni nguvu ya watawala ndo maana Seif mpaka haitambui serikali ya mapinduzi
 
Acha uongo Jk ndo aliyesuhisha mgogoro wa kenya na huko Znz alisuruhisha mgogo upi?maana tunavyojua yaliyofanyika Enji ni nguvu ya watawala ndo maana Seif mpaka haitambui serikali ya mapinduzi
JK alitengenezewa mazingira na Condolizer rice kwa maelekezo ya Bush na alienda siku ya mwisho tu waliokuwa Kenya kwa zaidi ya mwezi ni Koffi Anan na kina Mkapa, unajifanya unajuua unataka kusema Mkapa hakuwepo kwenye Mgogoro wa Kenya?
Kuhusu Zbar hawa jamaa walikuwa na mkono katika maamuzi ya hatma ya uchaguzi Zbar.
 
Umejibu vema sana.

Kuna watu wanajifanya kujua mambo, kumbe hawajui kitu
 
JK alitengenezewa mazingira na Condolizer rice kwa maelekezo ya Bush na alienda siku ya mwisho tu waliokuwa Kenya kwa zaidi ya mwezi ni Koffi Anan na kina Mkapa, unajifanya unajuua unataka kusema Mkapa hakuwepo kwenye Mgogoro wa Kenya?
Kuhusu Zbar hawa jamaa walikuwa na mkono katika maamuzi ya hatma ya uchaguzi Zbar.
Kuhusu swala la Znz usuruhishi wa Mkapa uko wapi hapo zaidi ya kupendelea chama chake na isitoshe kwenye utawala wake ndiko mauaji makubwa yalitokea kule znz
 
...Mkapa ndio msuluhishi?!,kweli wonders shall never end,hebu basi akasuluhishe na Znz!!
 
Wapi, Kenya?
MK254 kuya kaka, kumbe Mkapa ni nabii huko jirani?

Mphamvu Huku unaniita sioni umuhimu wake, maana nyie ndio chanzo cha hayo matatizo mnayojifanya kuyatatua. Mumemkingia kifua huyo nduli miaka yote. Halafu mnayemtuma ndiye nachoka nikiwaza alivyowatukana nyie kuwa malofa na wapumbavu. Sijui ana ujuzi gani kwenye kusuluhisha mambo wakati mwenyewe hana lugha ya demokrasia wala diplomasia.

Nakumbuka alivyokuja kushanga shangaa hapa Kenya wakati tulikua na vurugu.
 
Ha ha ha ha, umeenda mbali sana ndugu. Ishu ya malofa ilikuwa 'petty politics', huwezi kuchujusha utukufu wa Ben kwa neno, tusi moja kwa watu ambao indeed walikuwa malofa kweli.
Chanzo cha mgogoro sie hatukijui, lakini huwa sio waingiliaji sana wa mambo ya ndani ya nchi za watu. Kama Rais ni halali sie humuunga mkono, kitu ambacho wewe ungefasiri kama kukinga kifua!
 
Back
Top Bottom