Mkapa apondwa

Mkapa apondwa

Django

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
354
Reaction score
147
TUHUMA za matumizi mabaya ya ofisi zimezidi kumuandama Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Benjamin Mkapa, ambapo safari hii Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ameponda sera ya ubinafsishaji.

Sera ya ubinafsishaji iliyoanzishwa chini ya utawala wa Mkapa licha ya kupata upinzani mkali, kiongozi huyo alisisitiza ndiyo njia pekee ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

Kinana alitoa kauli hiyo juzi jioni ambapo alisema ubinafsishaji haujafanikiwa vizuri, kwani tangu sera hiyo ianze nchini viwanda vingi vilivyobinafsishwa havijafanya kazi wala kutoa ajira kama ilivyokusudiwa.

Kiongozi huyo alielezea kushindwa kwa ubinafsishaji huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kwenda kuzungumza na wawekezaji wa sekta binafsi kwenye mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.

“Ubinafsishaji haujasaidia sana, kwa kuwa kuna viwanda havifanyi kazi, havijatoa ajira kama ilivyotarajiwa. Mahali ambapo serikali imeshidwa katika sekta kama bandari, barabara na viwanja vya ndege, sekta binafsi zinaweza kusaidia,” alisema.

Kinana alitoa mfano wa Kitengo cha Makontena cha TICTS kilichoingia mkataba katika Bandari ya Dar es Salaam tangu mwaka 2000, kina changamoto nyingi ambazo hazikutarajiwa.

Aliongeza kuwa hata mikataba ya kununua umeme kati ya TANESCO na wazalishaji binafsi na wale wanaoiuzia TANESCO umeme wa dharura, mikataba hiyo pia haikufanya kazi kwa kadiri ilivyotarajiwa.

Kinana alisema, mkataba wa Reli ya Kati ulioingiwa mwaka 2007 kwa ajili ya uendeshaji wa huduma za abiria na mizigo kutoka kwa Kampuni ya RITES ya India, mkataba huo ulivunjwa, kwa kuwa shirika hilo lilifanya kazi chini ya kiwango kutokana na kuingia mkataba mbovu usio na tija.

Kinana alitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya taasisi kuwa na uwezo mdogo, pia kukosekana kwa makubaliano na uwezo wa kiutawala kwa uendeshaji, uzalishaji na shughuli za masoko.

Changamoto nyingine ni mfumo wa kisheria na udhaifu wa uratibu na uwezo wa udhibiti, ikiwemo ukosefu wa fedha na kukosekana kwa upembuzi yakinifu.

Januari 1992, serikali chini ya Rais Benjamin Mkapa ilitangaza rasmi mwanzo wa utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji. Mwaka uliofuata, ikaundwa tume ya kubinafsisha mashirika ya umma iliyoitwa PSRC. Hadi kufikia Machi 2000, jumla ya mashirika ya umma 283 yalikuwa yamebinafsishwa.

Lengo ni kusimamia na kuratibu masoko ya hisa na mitaji, ni kuharakisha ubinafsishaji wenyewe na hadi mwaka 2000, mashirika ya umma yapatayo 283 kati ya 425 yalikuwa yamebinafsishwa.

Zoezi la ubinafsishaji lilipata msukumo zaidi mwaka 1997 baada ya kuanzishwa Kituo cha Uwekezaji (TIC), ambapo mojawapo ya majukumu yake ni kuivutia na kuifanya sekta binafsi ishiriki zaidi katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, Machi 2003 mashirika ya umma mengi yalibinafsishwa yakitarajiwa kuwa yangeleta unafuu katika uzalishaji, na kutoa ajira kwa Watanzania.

Taarifa rasmi zilizotolewa na Waziri wa Mipango na Ubinafsishaji, Abdalah Kigoda, bungeni Februari mwaka huo, zilionesha kuwa mashirika 134 yalinunuliwa na Watanzania kwa asilimia 100, mashirika 16 yalipata wawekezaji wa nje kwa asilimia 100 na mashirika 116 yamebinafsishwa kwa njia ya ubia kati ya wawekezaji wa nje na wawekezaji wa ndani.

Mashirika 16 kati ya mashirika yaliyonunuliwa na Watanzania yamebinafsishwa kwa njia ya kuwauzia wafanyakazi wa mashirika husika.

Wakati wa utawala wa Mkapa mwaka 2002, kazi ilielekezwa katika kuandaa mikakati mbalimbali ya kubinafsisha au kurekebisha mashirika ya miundombinu na huduma yakiwamo Dawasa, ATC, TANESCO, THA, TRC, NIC na NMB.
 
Kama Kinana anaponda hizo sera za ubinafsishaji,wakati haya yanafanyika yeye (Kinana) alikuwa wapi kwa wakati huo na alikuwa na cheo gani na kwa nini alikaa kimya hakuongea that time aje kuongea saiv? Aache unafiki wa kisiasa.Kama ni sera za ubinafsishaji anazoponda leo zote ziliratibiwa na serikali ya CCM. Meaning that anakosoa awamu ya tatu ya serikali ya chama chake at the wrong time.CCM wanatakiwa kujifunza kukosoana at the right time na sio kusubiria mambo yameshapita ndo wanaigiza kukosoa mfano mzuri ni Mbunge Kessy alivyopinga bajeti ya wizara ya Magufuli.
 
Januari 1992, serikali chini ya Rais Benjamin Mkapa ilitangaza rasmi mwanzo wa utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji. Mwaka uliofuata, ikaundwa tume ya kubinafsisha mashirika ya umma iliyoitwa PSRC. Hadi kufikia Machi 2000, jumla ya mashirika ya umma 283 yalikuwa yamebinafsishwa.
Comprehending.................
 
Kama Kinana anaponda hizo sera za ubinafsishaji,wakati haya yanafanyika yeye (Kinana) alikuwa wapi kwa wakati huo na alikuwa na cheo gani na kwa nini alikaa kimya hakuongea that time aje kuongea saiv? Aache unafiki wa kisiasa.Kama ni sera za ubinafsishaji anazoponda leo zote ziliratibiwa na serikali ya CCM. Meaning that anakosoa awamu ya tatu ya serikali ya chama chake at the wrong time.CCM wanatakiwa kujifunza kukosoana at the right time na sio kusubiria mambo yameshapita ndo wanaigiza kukosoa mfano mzuri ni Mbunge Kessy alivyopinga bajeti ya wizara ya Magufuli.

Nipe jina la mwanasiasa asiye mnafiki, nitakupa evidence ya kuwa ni mnafiki
 
huyu na maghufuli wote walewale.sema ben ni nyangumi while pombe ni tilapia.
 
1992 Rais alikuwa ni Mwinyi.

Hapa Mkapa analaumiwa bure. Ubinafsishaji ilikuwa ni sera ya CCM na ilianza wakati wa Mzee Ruksa na wakati huo Kinana lazima alikuwepo kwenye balaza la Mawaziri!!!
 
Comprehending.................

siyo kauli yangu hiyo kaka nimemnukuu KINANA jana alipokuwa anaongea na wandishi wa habari hii ni kawaida kwa viongozi wetu kutokuwa na kumbukumbu sihihi za matukio muhimu kwani hata Naibu waziri wa elimu alishawahi kuchemka kuhusu tarehe ya uhuru wa tanzania na muungano wa tanganyika na zanzibar tena kwenye kikao cha kimatifa so sishangai.
 
Sasa kinana kwa nini msiboreshe kama chinga alichemka na wewe ni katibu mkuu wa ccm unalia nini sasa????
 
Kazi kulaumu tuu,.... Dhaifu sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
1.mkapa+kinana=ccm

2.ubinafsishaji+mkapa=ccm

nenda lushoto tanga kwa mkapa atakupa maana ya milinganyo hiyo hapo juu.
 
siyo kauli yangu hiyo kaka nimemnukuu KINANA jana alipokuwa anaongea na wandishi wa habari hii ni kawaida kwa viongozi wetu kutokuwa na kumbukumbu sihihi za matukio muhimu kwani hata Naibu waziri wa elimu alishawahi kuchemka kuhusu tarehe ya uhuru wa tanzania na muungano wa tanganyika na zanzibar tena kwenye kikao cha kimatifa so sishangai.
I knew it wasn't yours Django
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom