Mkapa akosoa uwajibikaji wa viongozi Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa akosoa uwajibikaji wa viongozi Afrika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  NCHI za Afrika zimeshauriwa kutazama upya mifumo ya uchaguzi ili iendane na maslahi ya watu wake pamoja na kuwaletea maendeleo ya kweli kiuchumi.

  Viongozi wa Afrika pia wametakiwa kuwa tayari kusikiliza maoni ya taasisi za nchi zao na wanaowaongoza na kuyafanyia kazi maoni wanayopewa na kwamba wasiosiliza basi hawaongozi vizuri.Hayo yalisemwa jana na rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Graca Machel, mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela kwenye Mkutano wa Kiuchumi wa Dunia (WEF) unaozungumzia Afrika na ambao ulimalizika jana jijini Dar es Salaam wakati wakijadili mada kuhusu uongozi katika rika zote barani humo.

  Graca, ambaye pia alikuwa mke wa rais wa zamani wa Msumbiji, Samora Machel, alisema anapata shida kila anapofikiria na kuona kuwa katika Afrika viongozi wanaochaguliwa wanatoka katika vyama vya siasa pekee, jambo alilosema si lazima kwa hali ya sasa.

  “Nafikiri Bara la Afrika linahitaji kutazama upya mifumo ya uchaguzi. Napata shida kuona vyama vya siasa ndio vinatoa viongozi pekee, hii si lazima,” alisema Graca.

  Alifafanua kuwa walio katika vyama vya siasa huangalia na kusaidia vyama husika na marafiki zao huku wakiacha wananchi wengi wakikosa fursa na mambo muhimu ambayo yangesaidia kuboresha uchumi wa nchi zao na maisha yao.
  “Tunachanganya, tunapofikiri kuwa kila aliye na madaraka ni kiongozi, hii si sahihi, uongozi unakuja na utu, utaifa na kujali maslahi ya unaowaongoza,” alisema Graca.

  Graca alisema inashangaza kuona wanasiasa wanapotafuta kura wanakuwa na sura tofauti kwa kuvaa mavazi ya kawaida ambayo yana fanana na ya mwananchi wa kawaida, lakini wanapopata uongozi wanakuwa tofauti," alisema.

  "Mtu akishachaguliwa, hujifanyia maamuzi bila ya kujali wengine. Wananchi wanakosa hata nafasi ya kumsogelea na kumwambia 'rais huyu hatufai, teua mwingine'. Wanakosa nafasi hiyo," alisema Graca.

  Naye Mkapa alisema ni vizuri taasisi zinazofanya vizuri zikamshauri rais na rais anayeshauriwa anapaswa kumsikiliza ushauri anaopewa.

  Alisema kama kuna taasisi za kijamii kama chama cha walipa kodi na vingine ambavyo vinawajibika vizuri, vitaweza kumshauri rais, lakini ni lazima pia kiongozi anayeshauriwa kuwa msikivu na kuweza kufanyia kazi ushauri wao.

  “Mimi nimestaafu hata mawazo yangu pia, lakini ninachoona ni kuwa viongozi lazima wajiandae kuongozwa, wapo wasiosikiliza mawazo ya tasasisi na watu wanaowaongoza, usiposikiliza hayo wewe si kiongozi.

  “Kiongozi ukifikiri washauri wako hawafuati unayotaka wewe, utawadharau na ukifanya hivyo watu hawatakusikiliza unaposema jambo,”alisema Mkapa.

  Alisema ili kiongozi awe bora katika nchi yake ni lazima ajengee timu nzuri ya mashauriano na taasisi mbalimbali.

  Akitoa maoni yake waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba alisema ili kupata viongozi bora, vyama vya siasa ni lazima viweke msisitizo katika kukubali viongozi wanaokubalika na wananchi.

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/1432-mkapa-akosoa-uwajibikaji-wa-viongozi-afrika
   
 2. M

  Mchili JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Anayosema ni point nzuri. Je yeye alikua anasikiliza??? Ukiwa jukwaani ni rahisi kukosoa wanaocheza uwanjani.
   
Loading...