Mkapa Aja juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa Aja juu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 20, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu na Mwenyekiti wa Kongamano, Benjamini Mkapa akichangia mada kwenye kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.Picha na Venance Nestory

  Claud Mshana
  RAIS mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa amesema Watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri badala yake wanaruhusu hisia zao kutawala na kuishia kutuhumu vitu ambavyo hawana uhakika navyo.

  Akizungumza katika Kongamano la 12 la Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam, Mkapa alisema watu wengi wanatuhumu bila ya kuangalia uhalisi wa kitu.Katika hali iliyoonesha kuwa kiongozi huyo mstaafu alikuwa akijibu mashambulizi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakielekezwa kwake na viongozi wengine wa chama chake, aliwataka viongozi na Watanzania wote kwa ujumla kuelekeza nguvu zao kujadili masuala yenye tija kwa taifa.

  Baada ya kung’atuka madarakani, Mkapa amekuwa akiandamwa na vyama vya upinzani kwa kile kinachoelezwa, matumizi mabaya ya madaraka kwa kufanya biashara akiwa Ikulu.

  Mbali na hilo Mkapa amekuwa akilaumiwa kwa kutokuwa makini katika sera zake za ubinafsishaji zinazodaiwa kutoa nafasi zaidi kwa wawekezaji kunufaika na raslimali za taifa hususan katika mirabaha ya madini huku wananchi wengi kwenye maeneo hayo, wakizidi kubaki masikini.

  Mbali na hayo, Mkapa pia alitajwa kwenye orodha ya watuhumiwa 11 wa ufisadi kwa mujibu wa Chadema, iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam Septemba 15, 2007.

  Orodha hiyo ya Dk Slaa iligusa hisia za wananchi wengi huku hoja ya ufisadi ikiteka fikra za wengi na kuwa gumzo kwa Watanzania wengi na kupenya hadi ndani ya chama tawala (CCM), hatua iliyosababisha kuibua mkakati unaoendelea wa ‘kujivua gamba. ‘

  Katika kongamano jana, Rais Mkapa aliwataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuelekeza nguvu zao kujadili masuala nyeti yenye umuhimu na tija kwa maendeleo taifa .

  Alitolea mfano masuala mazito ya kujadiliwa yenye manufaa kwa nchi kuwa ni pamoja na ushirika wa maendeleo kati ya nchi za Afrika na Ulaya ambao kwa mujibu wa kiongozi huyo, hauna lengo la kunufaisha nchi za Afrika.
  “Mapendekezo wanayotoa hayana faida zozote kwa nchi za Afrika na sasa wanataka kuita nchi mojamoja kuzungumza nazo, hatuwezi kuwa na ushindani sawa kwa vigezo wanavyotaka wao,” alisema Mkapa na kuongeza: “Pamoja na mengine, hayo ndiyo mambo makubwa ya kuzungumzwa, tunafikiria nini juu ya mambo haya?”

  Awali wachangiaji waliotangulia walilalamikia kuhusu ongezeko la umasikini nchini, suala la ardhi, uwekezaji na kupanda kwa hali ya maisha kwa maelezo kuwa yanachangiwa na Serikali kushindwa kuwajibika.
  Akimzungumzia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mkapa alisema taifa lina wajibu na dhamana ya kulinda urithi, hekima, busara na falsafa za kiongozi huyo muasisi wa Taifa kwa kumuenzi.

  “Serikali inawajibu mkubwa wa kuendeleza juhudi hizi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na jamii nzima kwa ujumla,” alisema na kuongeza;
  “Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na utamaduni huu kwa kuzingatia hali ya maisha ya muasisi huyu,”
  Mkapa alisema, anatambua kuwa zipo changamoto nyingi zinazohitajika kuzifanyia kazi ili kufanikisha jambo hili muhimu la kudumisha misingi bora ya fikra za Mwalimu Nyerere.

  Kingunge, Warioba wawapasha vijana
  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba na mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru waliwashambulia vijana nchini kwa maelezo kwamba hawawajibiki na badala yake, wamebaki kulalamika.
  Kauli ya wanasiasa hao iliungwa mkono pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, aliyewataka vijana kuwajibika na kuacha kulialia.

  Kauli za viongozi hao zilifuatia viongozi hoja ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Hussein Bashe, aliyewalaumu viongozi wa sasa kwa kufumbia macho matatizo yanayowakabili vijana, hususan kuhusu tatizo la udini na ukabila.
  Akichangia hoja, Bashe alisema kwa hali ilivyo hivi sasa nchini, vijana wasitarajie kuwa na mafanikio wanayofikiria.
  Aliongeza kuwa, wazee wamekaa kimya wakati taifa linakabiliwa na mipasuko ya hatari kama udini na ukabila ambavyo vilianza kujitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka jana.

  “Wazee mmekaa kimya, watoto wa mjini tunasema ‘mmeingia mitini’, mpo wapi kukemea haya? Je, wajibu wenu uliishia pale mlipoondoka madarakani? ” Alihoji na kuongeza: “Viongozi wanajadili ukabila mko wapi? Hofu yangu naona viongozi mlioishi na Baba wa Taifa mnajitenga.”
  Akijibu hoja hiyo, Jaji Warioba alisema kuwa, nchi hii inaongozwa na vijana na kwamba hata wakati wa Baba wa Taifa, wazee walikuwa washauri, hata walipostaafu, waliacha madaraka kwa vijana.

  “Hatukuwa tukilalamika wala kulaumu wazee, tulikuwa tunachapa kazi na kufanya mambo yetu wenyewe, hata kama tulitofautiana, tuliita wazee, walirekebisha mambo,” alisema Warioba.Alifafanua kuwa hata wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere matatizo yalikuwepo na kwamba njia pekee ya kuyatatua, ni kuyazungumza na kuangalia namna ya kuyakabili.
  Aliongeza kuwa Mwalimu Nyerere aliishi kwa maadili, hivyo ni wajibu wa viongozi wote na Watanzania kwa ujumla kuishi kwa kufuata misingi aliyoiweka.

  Naye Kingunge alisema japokuwa vijana wanalalamikia wazee, binafsi anaona pande zote mbili zina matatizo ya msingi. “Vijana wanataka dunia isiyo na matatizo, lakini tulichofanya tukiwa vijana ni kupambana na matatizo kila yalipotokea, hadi leo tunapambana,” alisema Kingunge akijitolea mfano mwenyewe kuwa ni Kamanda wa Vijana wa CCM.

  “Napata taabu sana kuona rafiki zangu si wapambanaji, yale masuala ya msingi siyaoni… Tulianza vizuri sana wakati wetu. Kipindi kile hatukuwa tukisukumwa na vyeo wala marupurupu bali uzalendo,” alisema na kuongeza :

  “Lakini alichosema Bashe ni kweli, hivi sasa kuna kuingiza udini, mfano uchaguzi uliopita tena mambo haya yalikuwa waziwazi kabisa… Tatizo viongozi wetu ni wale wanaosema sisi hatuwezi kuzungumzia mambo hayo.”

  Alionya kuwa kama udini utaingia, hakutakuwa na Tanzania moja na kusisitiza kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai, jambo hilo angelikemea waziwazi.
  “Hatuwezi kusema tunamuenzi Mwalimu wakati tunawaogopa watu fulani wanaoongea udini,” alisema Kingunge.

  Kwa upande wake, Butiku alisema tatizo kubwa ni utekelezaji kwa vitendo wa yale yote aliyoyasimamia na kuyaamini Mwalimu Nyerere.
  “Hoja zote nimezisikia na malalamiko haya ni ya muda mrefu, vijana wamekuwa wakilalamika na inapofika wakati wa kumuenzi mwalimu ni wakati wa msiba. Lakini nataka nijue kama mnalilia vyeo au mnataka nafasi ya kubeba mzigo wa uongozi, mimi nashauri ni wakati wa kutekeleza mengi aliyosema Mwalimu na kuandika,” alisema Butiku

  Ole Sendeka Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alisema uhuru uliopiganiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ulikuwa kwa ajili ya Watanzania wote, lakini na hivi sasa, kumekuwa na tofauti kubwa ya mapato kati ya matajiri na masikini walio wengi.

  Huku akitoa mfano wa umilikaji wa ardhi na manufaa hafifu kutoka kwenye sekta ya madini, Ole Sendeka alisema mwalimu Nyerere alionyesha uzalendo kwa vitendo na kuongeza kuwa vitendo vya viongozi wa sasa , vinatia mashaka kama kweli kuna wafuasi wa Mwalimu Nyerere.Kongamano hilo lilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali, wasomi, wanaharakati, wanasiasa na wananchi wa kawaida.

  Naye Moses Mashalla, anaripoti kutoka Arusha kuwa, Mjadala wa katiba mpya hapa umezidi kushika kasi baada ya wanasheria na baadhi ya wananchi mkoani Arusha kutaka itungwe sheria za kulinda rasilimali za nchi. Walitoa ushauri huo wakati wakichangia mada katika mdahalo wa katiba uliohusu rasilimali za nchi na mustakabali wa muungano ndani ya Katiba mpya, uliofanyika jana jijini Arusha. Mdahalo huo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) uliongozwa na Elfuraha Laltaika, ambaye ni mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Makumira,.

  Akichangia mada katika mdahalo huo, Rais wa Chama wa Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Francis Stolla, alisema katiba ya sasa ina upungufu mkubwa hususan katika suala la ardhi ambalo ni rasilimali ya taifa hili. Alisema katiba ya sasa haijaelezea kwa ufasaha endapo rasilimali ardhi ni mali kwa sababu kuna kaulimbiu isemayo ‘ardhi ni uhai.’

  Hivyo alitoa changamoto kwa wananchi kuhoji suala la ardhi kama mali ya wananchi ambayo inahitaji kulindwa kwa nguvu zote. “Hivi ardhi imelindwa kwa namna gani ndani ya katiba yetu ya sasa? Nasema hivyo kwa sababu ukifungua katiba huwezi kukuta imetajwa kama mali, wakati kuna usemao unaosema ‘ardhi ni uhai wetu,” alisema Stolla Naye, Mhadhiri wa Siasa na Uchumi katika Chuo kikuu Dodoma (UDOM), Dk Sinda Sinda, alisema kuwa, rasilimali za taifa ndizo zimebeba hatma ya maendeleo yao hivyo Watanzania wana kila sababu kukataa baadhi ya sheria za kimataifa kuingizwa katika katiba mpya kwa kuwa nyingine ni kandamizi zisizo na tija.

  Alitoa mfano wa sheria ya ubinafsishaji ambayo imechangia kuuza viwanda vingi nchini vilivyokuwa vikizalisha bidhaa mbalimbali, akiwataka wananchi kuzikataa .

  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Che-nkapa hana akili.
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Nachukia mtu anayejifanya ana akili kuliko watz milioni 40 na kutaka kuwafundisha cha kujadili! Watu watajadili yanayowasibu na kuwagusa.wanayojadili watz ndio yaliyo moyoni! Wasitufundishe! Wajibu wao ni kutusikiliza sisi mabosi wao (watz).siku hizi kuna watu wanajiona wana upeo kuliko watz wote! Wakome kutuelekeza cha kusema,wanataka kusikia wanachopenda tu! Tuwapuuze! Ajenda kuu ni zile zile UFISADI,na CCM IMETOSHA!
   
Loading...