Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Wana jf leo asubuhi bungeni kumetokea mkanganyiko pale ambapo mbuge mmoja toka Zanzibar alipotaka kujua nini kitaikumba Tanzania katika medani ya soka kutokana na viongozi wa ZFA kupelekana mahakamani ili hali sheria za FIFA zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa mahakamani na adhabu yake ikionekana ni kufungiwa na FIFA. Kutokana na majibu ya waziri mwenye dhamana(Nape) yaligusia kuwa chombo kinachoiwakilisha Tz huko FIFA ni TFF, ndipo mbunge mwingine aliomba mwongozo na kusema kuwa waziri Nape ametoa majibu asiyokuwa na uhakika nayo kwani ZFA na TFF ni vyombo viwili tofauti akaenda mbali zaidi kuwa hata hiyo wizara ya Nape si ya muungano kwa kuwa mambo ya michezo na burudani si ya muungano. Je, ZFA wanatambulika FIFA? Kama hawatambuliki hilo swala likiwafikia FIFA nani atapewa adhabu ya kukiuka sheria za FIFA? Na km TFF hawana ubavu Zanzibar watajinusuru vp na huo mgogoro wa ZFA ili adhabu isijeikuta Tz kutokaFIFA? Na mbona kirefu cha TFF ni "Tanzania Football Federation", kwani Zanzibar haipo Tanzania?
Tujadilini kwa facts
Tujadilini kwa facts