Mkaa wazidi kumaliza miti asili, Gesi bei juu

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,945
3,237
Imeripotiwa na watafiti kuwa mkaa wazidi kumaliza miti asili.

Kwanza tuangalie manufaa ya miti asili

A - Hali ya hewa kuwa nzuri (mvua)

B- Vyanzo vya Maji

C- Madawa ya Asili

D - Nyumbani kwa wanyama (mammals, reptiles and birds).

Sababu za watu kukata miti ni mkaa na kuni

Gesi bei juu

Umeme bei juu

Source: Ippmedia media Gazeti

Mawaziri wanaohusika ni Mh. Maghembe, Mh. Makamba, Mh. Muhongo (bei ya gesi na umeme) na Mh. Simbachawene (serikali za mitaa)

===============================

Mkaa wazidi kupuputisha miti ya asili

Kutokana na hali hiyo, Shirikika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania TFCG na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) wameiangazia athari hiyo wilayani Kilosa na kuwashauri wadau mbalimbaku kushiriki kukabiliana na vitendo hivyo vya uvunaji ovyo wa misitu.

Akizungumza na wadau wa misitu Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro uliolenga kujadili kuhusu mpango wa uvunaji mkaa na mbao wilayani humo, na kuowashirikisha madiwani na wadau mbalimbali, Mkurugenzi wa Mjumita, Hidaya Njaidi, alikiri hali siyo nzuri kwa sababu hekta 350,000/= wilayani Kilosa pekee zimekuwa zikiteketea kila mwaka kutokana na shughuli za uharibifu wa mazingira.

Alisema shughuli hizo ni pamoja na ukataji miti ovyo, uchomaji wa misitu kwa ajili ya mkaa pamoja na upasuaji wa mbao, hali inayosababisha misitu mingi kuharibiwa na hata kutokea kwa mabadiliko ya tabianchi.

Aliwashauri wananchi na wadau wengine wa misitu wilayani Kilosa kuacha kuharibu misitu kiholela ili kuyalinda mazingira na kuikoa nchi kuzama katika janga la ukame.

Njaidi pia, aliwataka wananchi kubuni shughuli nyingine mbadala za kujiingizia kipato mbali na uchomaji wa mkaa, kwani kupitia TFC na Mjumita wamekuwa wakisaidia shughuli nyngine ikiwamo za uwindaji na ufugaji wa nyuki, nia ikiwa kuwawezesha wananchi kujimudu kimaisha badala ya kutegemea jambo moja.

Meneja Mradi wa Mkaa Endelevu (TTCS), Charles Leonard, alisema ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ni vyema jami ikatumia njia sahihi ikiwamo waliyoanzisha kupitia mradi wa TTCS kupata mkaa endelevu, kwa kuwa njia hiyo ni salamà na inalenga kuokoa misitu na kuwafanya wananchi kuweza kujiajiri, kusaidia ulipaji wa ushuru na kukusanya mapato.

Afisa mwingine wa Mjumita, Elida Fundi alibainisha mradi huo wa uvunaji wa mkaa endelevu unalenga kuboresha namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuboresha uendelevu wa mazingira na kuongeza faida zitokanazo na rasilimali za misitu, hivyo kuleta maendeleo endelevu kwa Tanzania na wananchi wake.

Aidha, alisema mradi ulilenga pia, kusaidia wanavijiji na wadau wengine wanaotegemea sekta ya mkaa kuanzisha, kusimamia na kufaidika kibiashara kutokana na mkaa uliovunwa kiuhalali na kwa njia sahihi.

Wadau wa misitu wilayani Kilosa wakiwamo madiwani Mariam Naheka na Ramadhani Mfaume walikiri hatari iliyopo iwapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kudhibiti uvunaji holela wa misitu na kupongeza jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kubuni namna bora ya kudhibiti hali hiyo, na kwamba kupitia mradi wa mkaa endelevu, wanaamini ni fursa kwa wananchi bila kubagua jinsia katika kuongeza kipato.
 
Back
Top Bottom