PreGE2025 Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Comrade Samira Khalfan Amour awapa furaja watoto wenye mahitaji maalumu biharamulo

PreGE2025 Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Comrade Samira Khalfan Amour awapa furaja watoto wenye mahitaji maalumu biharamulo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
11,718
Reaction score
27,812
CDE SAMIRA KHALFAN ASHEREHEKEA SIKU YA MAMA DUNIANI KWA KUTEMBELEA SHULE YENYE WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM ATOA RAI KWA JAMII KUWAJALI NA KUWATHAMINI, AKABIDHI MATENKI YA MAJI, MASHUKA NA KUTOA MOTISHA KWA WALIMU - BIHARAMULO.*

Maadhimisho ya siku ya mama Duniani, Kata ya Kabindi Wilaya ya Biharamulo

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera na Mjumbe wa Kamati ya Uchumi, Fedha na Mipango UWT Taifa, Cde. Samira Khalfan ameadhimisha Siku ya Mama Duniani kwa kuwatembelea wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Kabindi wilayani Biharamulo ambapo ameonyesha upendo Wa kipekee na kuwapa faraja wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kusherehekea siku hiyo maalum pamoja nao, leo tarehe 11 Mei 2025.

Katika maadhimisho hayo, Cde. Samira Khalfan alitoa matenki makubwa ya kuhifadhia maji, ili kusaidia shule hiyo kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na kueleza kuwa maji ni hitaji muhimu kwa mazingira bora ya kujifunzia, hasa kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Aidha Cde Samira Khalfan alimpongeza Mhe. Eng Ezra Chiwelesa Mbunge wa Biharamuro Magharibi ambaye tayari ameshatoa msaada wa Magodoro 50 na amemuunga mkono kwa kutoa mashuka 30 kwa ajili ya kujifunika wanafunzi wanapolala katika mabweni ya shule hiyo ambayo yatasaidia kuboresha hali na Afya kwa kuwafanya wanafunzi kujisikia kustarehe na kujihisi kuthaminiwa kama watoto wengine hasa nyakati za baridi.

Katika hatua nyingine Cde Samira Khalfan ametoa motisha ya shilingi 400,000 kwa walimu wa shule hiyo kama ishara ya kutambua na kupongeza kazi kubwa wanayofanya ya kuwalea na kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalum kwa moyo wa kujitolea. Alisisitiza kuwa walimu wa kundi hili wanastahili kutunzwa na kupewa motisha zaidi na kuwahimiza wananchi kuwatembelea watoto na Walimu shuleni hapo.

Katika hotuba yake kwa wanafunzi, walimu na wazazi waliohudhuria, Cde. Samira alitoa wito kwa jamii kuendelea kuwajali watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwapa upendo, msaada na mazingira bora ya kujifunza. Alieleza kuwa kila mtoto ana haki ya kufurahia maisha na kupata elimu bora, bila kujali changamoto zake za kiafya au kimaumbile.

Kazi na utu tunasonga mbele na SSH na Eng Ezra Chiwelesa 2025-2030 🇹🇿🇹🇿🇹🇿
BlendMePhoto1749373935822.jpg
IMG-20250608-WA0024.jpg
 

Attachments

  • BlendMePhoto1749375040601.jpg
    BlendMePhoto1749375040601.jpg
    522.3 KB · Views: 15
Back
Top Bottom