KUCHITIMBO1970
JF-Expert Member
- Apr 24, 2015
- 482
- 221
MJEE/MZEE WA MUSOMA.
Katika wilaya ya Musoma kuna eneo mashuhuri kwa uvuvi na shughuli za kilimo linaitwa Majita,hili ni eneo linalokaliwa na Wajita kwa sehemu kubwa na Wakwaya ambao pia ni jamii ya wajita.
Nilipofika katika hili eneo ambalo kwa sasa limetengwa kuwa halmashauri ambayo makao makuu yako Mrangi,kabla ya kuhama kurudi Arusha niliifatilia historia ya hili eneo na kati ya mambo mengi ya kihistoria nilvutiwa na historia ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mjee.
Mjee alikuwa hajaoa na alikuwa hana makazi maalumu,alikuwa mtu wakutembea tembea leo yuko kijiji hiki na wiki kesho yuko vijiji vingine.Alikuwa hana urafiki wa karibu na watu wazima,maana huwezi mkuta akijadiliana jambo na watu wazima ama wazee bali ni watoto wadogo ndo walikuwa ni marafiki zake.
Akiingia kijijini unakuta anatembea na rundo la watoto wadogo maana watu wazima walimuona kama hazimtoshi yaani punguani,ila walikuja kujua kama hakuwa punguani pale mambo aliyokuwa anawaambia yalipoanza kutokea ikiwa ni baada ya miaka mingi kupita.
Ni mtu wa pekee ukiifatilia historia yake maana alitabiri mambo mengi na hata yeye kujitabiria angali akiwa hai kuwa baada ya kifo chake kila mwanamke katika Majita nzima atakaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima atamuita jina lake yaani Mjee iwe kwa kupenda ama kutopenda.Hili limethibitika ndani ya majita nzima,maana kwa kila mwanamke anaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima amuite jina la Mjee ingawa atakuwa na jina lake lingine.Hivyo hata wazee wa miaka 90 kule majita waliitwa jina la Mjee na mama zao na hili halina ubishi,hii inaendelea hadi leo.
Nilipoongea na wazee wakaniambia alitabiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuja kwa wakoloni,watu kuishi pamoja yaani vijiji vya ujamaa,watu kuishi kwenye vichuguu,kiongozi wa kwanza wa hili taifa kutawala akiwa tumboni,atake fuata na utawala wake,wa pili na hata wa mwisho na pia jiwe litakalo tokea.Alipo kuwa anayaongea hayo alikuwa anatoa sauti kama ya mtu anaye lia kwa kupiga mayowe.
KUJA KWA WAKOLONI.
Ikiwa ni kabula ya kuja kwa wakoloni,mjee alipita kwenye vijiji na kupaza sauti ya mayowe huku akifuatwa na msururu wa watoto na kuwaambia watu kuwa anaona mitumbwi mikubwa inakuja akimaanisha(meli na majaazi) imebeba watu ambao ni kama watoto(yaani ni weupe).Wanakuja ili kututesa na kila tulicho nacho watatunyang’anya. Alipo kuwa anayaongea haya watu wazima walisikika wakisema haaaa ni Mjee omusasi (yaani ni Mjee punguani/kichaa) alikuwa akidharaulika sana maana alionekana hazimtoshi.
Baada ya kifo chake na miaka mingi kupita ndipo wakoloni waliivamia Tanzania na hata wengine kufika majita na watu wengi kuuwawa wale walokuonesha upinzani wa kutawaliwa na wale watu.Maeneo yaliyo tumika kwa wenyeji kujificha wakati wa mapambano ni maeneo ya Makojo hadi Chimati,ambapo maeneo ya Chimati kuna mto ambapo mafuvu na mifupa ya watu ilionekan hadi miaka ya 1985.Ndipo hapo walianza kumkumbuka Mjee kuwa yule mtu hakuwa punguwani bali mtabiri.
VIJIJI VYA UJAMAA
Mjee alitabiri pia kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa ambapo alisikika akisema,ameiona mitumbwi inakuja huku imejaza mashoka(yaani jimbasa),akaona watu wanachukua mashoka na kufyeka pori(yaani kandokando) na akaona watu wanaishi ndani ya hayo maeneo. Akasema anaona watu wamejaa na wengi wanauana maana wamekosa mahala pa kuishi alipo kuwa anayasema hayo watu wazima wa maeneo aliyokuwa anapita walikuwa wanamcheka,ila kwa sasa maono yake yamesha timia.
WATU KUISHI KWENYE VICHUGUU
Miaka hiyo kila nyumba iliyokuwa inajengwa lazima ujenzi wake ulikuwa ama ukitumia nyasi,juu hadi chini ama ukitumia miti. Mjee aliona watu wakiishi kwenye vichuguu nadhani alishindwa kujua ujenzi unao tumika kwa sasa kutokana na uhalisia wa mazingira ya wakati huo na tekinolojia ya wakati huu.Vichuguu ni nyumba ya mchwa ambayo hujengwa na mchwa wenyewe kwa tope,ila alivyokua anaangalia huko mbele aliona pia watu wakiishi kwenye vichuguu yaani nyumba iliyo jengwa kwa tope kama za wakati huu.Hili halina ubishi maana maono yake yalitimia na yametimia kwa watu kutumia tope( yaani tofali) kujenga nyum
MTAWALA WA KWANZA KUTAWALA AKIWA TUMBONI
Miaka ya Mjee kuzunguka hili eneo la Majita,pia aliweza kutabiri kuhusu kiongozi wa kwanza wa nchi hii,akiwa katika kutembea na marafiki zake ambao walikuwa ni vijana wadogo,alisikika akisema(kwa sauti ya juu) kuwa ameoneshwa kuwa kiongozi wa kwanza atazaliwa huku majita,pia anaona huyo mtoto akitawala nchi akiwa tumboni maana wabaya wake watamuua,akasema ameona mtoto mwingine amezaliwa mashariki huyo ndo atakuja kuitawala nchi hadi ataacha mwenyewe,na atakuwa na amri juu ya hao watu weupe maana atawaambia ondokeni nyumbani kwangu nao watamtii maana wa mwanzo hatakuwepo tena.Aliyetabiriwa hapa ni mwl J.K.Nyerere maana Zanaki (Butiama) ipo mashariki mwa Majita
Baada ya miaka mingi kupita kati ya kijiji cha Bugunda au Bulinga alitokea mama mmoja mjamzito,ilikuwa ni kama muujiza pale mtoto aliyekuwa tumboni mwa mama yake alipo mwambia mama yake kuwa amzae ili akatawale nchi.Habari hii ilienea majita nzima kwa wakati huo hadi kwa machifu wa wakati huo hii haikuwa habari njema kwa watawala wa wakati huo kwani walidhani huyo mtoto atakuja kuwanyang’anya uchifu wao.Mtoto alipoanza kukua watawala wa wakati huo wakafanya mbinu ya kumuangamiza na hilo lilifanikiwa na kutimiza usemi wa Mjee wa kusema kuwa atatawala akiwa tumboni.Lakini baada ya mwl Nyerere kuja na kuikomboa nchi ndipo walipo kumbuka maneno ya mjee. Hili lilitokea kama maono ya mjee alivyokuwa ameoneshwa.
KIONGOZI ALIYEFUATIA.
Katika kutembea kwake huku akipiga mayowe,Mjee aliendelea na utabiri ambapo aliongea bayana kuwa baada ya utawala wa huyo atakaye tokea mashariki atakuja kiongozi mwingine atakeye tokea (Kwisinga) akimaanisha kisiwani,mda ukayoyoma na Nyerere alipo staafu kiongozi aliyefuata alikuwa ni Mzee Ruksa(Mwinyi).Waalokuwa na kumbukumbu ya kile Mjee alichoongea walikumbuka maana Mzee Mwinyi alitokea Zanzibar.
ATAKEYE MFUATA HUYO
Mjee alioneshwa kuwa baada ya huyo wa kisiwani atafuatia mtawala mwingine atakaye tokea mwisho wa nchi,Mtu akiwa Musoma(Mara) mwisho wa nchi itakuwa ni mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi.Lakini huu utabiri wake ulikuja kuthibitika pale Rais aliyefuata baada ya Mwinyi alitokea mkoa ambao uko mwisho wanchi kwa mtu atakayetokea mkoa wa Mara ama Musoma mwisho wa nchi ni mikoa niloitaja hapo juu ambapo BWMkapa alitokea mkoa wa Mtwara.
KIONGOZI ALIYEFUATA
Mjee alioneshwa katika maono kuwa atafuata kiongozi ambaye ni wa kunjekekera akimaanisha atatokea kandokando ya bahari ama ziwa.Katika awamu zilizopita tayari tumeshashuhudia kiongozi akitoka pwani ya bahari ya hindi.
Baada ya huo utawala atatokea kiongozi mwingine ambaye atatoka jirani na maeneo ya Musoma.Lakini baada ya huo utawala utafuata utawala wa LEMBESYA yaani atakayesawazisha kila kitu na kuweka kila kitu sawa ila katika maono alioneshwa kuwa Utawala huu wa LEMBESYA ataupata baada ya mapigano kidogo kutokea kutoka kwa mtangulizi wake mda huo maana atajaribu kung’ang’ania madarakani japo atakuwa ameshindwa kupitia sanduku la kura na pia utakuwa utawala wa mda mfupi maana utakuja utawala wa LISO TUNGU.
Lakini huu utawala wa LISO TUNGU utadumu japo si kwamda mrefu na utaondoshwa na utawala wa JIWE maana aliona katika maono jiwe kubwa likipiga utawala wa LISO TUNGU na baada ya hapo aliona giza tupu.
WAJITA MULIOKO HUMU MWAWEZA KUTUPA TAFASIRI YA HAYO MANENO YALOKOLEZWA NA KUTHIBITISHA UWEPO WA HUYU MTU HUKO MAJITA YA ZAMANI.