KERO Malalamiko kuhusu baraza la mji Mkongwe na askari wa Malindi wanavyotumia vibaya mamlaka yao

KERO Malalamiko kuhusu baraza la mji Mkongwe na askari wa Malindi wanavyotumia vibaya mamlaka yao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Suleiman al rasady

New Member
Joined
Aug 20, 2019
Posts
1
Reaction score
2
Mimi ni mzanzibar na mtanzania kadhaalika.... Leo nimeona tena maovu makubwa sana kwa eneo la Malindi zanzibar... Askari wamekua Hawna ubinaadamu wala imani ktk kazi zao..

Askari amenikamata kwasbb anasem nimpta wrong site wakati huo huo mimi naenda kumchukua mgeni wangu kwenye meli bandarini.... Nkamuuliza nikapaki wap chombo changu ikanibidi aseme mm nimjeuri kumuulixa kosa langu... Chombo kimepasi vzr tu na kila kitu kimo... Mwsho aknmbia either anipelke mji mkongwe au nimpe elfu 80..

Wakati huo mfukoni mim sina Mia... Ikanibidi niitafte ili nimpatie ili niondke

Point yangu ni mbili

Kwanza % ya askari wa Tanzania ni njaa wala hawatosheki na wanchopewa na serikali kwaio waongexewa mshahara ili kidg watulie roho zao pia waache ufisadi na roho mbya

Pili serikali ijenge au ueke utaratibu mzuri wa kueka vyombo vyao cio kututishia kwa askari au mji mkongwe kutupatia adhabu 🙏🙏🙏🙏
 
Hao hao mabos zao wanaiba mabilion ya fedha lakini hawatosheki, hata hao askari wakiongezwa mshahara hawawezi kubadilika.
 
Wewe utakuwa mtanganyika tuu, ungekuwa mzanzibari ungeonyesha kitambulisho Cha ukaazi ungeachiwa fasta. Shurba ni ksaajili ya watanganyika tuu.
 
Mimi ni Mzanzibari na Mtanzania kwa ujumla. Leo nimekumbana na tukio lililonisikitisha eneo la Malindi, Zanzibar, ambapo nahisi baadhi ya askari wamekuwa wakitumia vibaya mamlaka yao bila kuzingatia utu na haki za wananchi.

Nilisimamishwa na askari kwa madai ya kupaki sehemu isiyoruhusiwa, wakati nilikuwa nimefika bandarini kumchukua mgeni wangu aliyekuwa akiwasili kwa meli. Nilipomuuliza ni wapi napaswa kupaki na kosa langu lilikuwa nini, nilielezwa kuwa nina jeuri kwa kuuliza.

Chombo changu kilikuwa na vibali vyote vinavyohitajika, lakini mwisho niliambiwa nichague kati ya kupelekwa Mji Mkongwe au kutoa shilingi 80,000. Kwa kuwa sikuwa na fedha hiyo mfukoni, ilinibidi nitafute ili niweze kuondoka.

Naomba kusisitiza mambo mawili:

Kwanza, Serikali iendelee kuboresha maslahi ya askari ili kupunguza vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi yao.

Soma Pia: Mji mkongwe na askari wake


Pili, kuwe na utaratibu mzuri wa maeneo ya maegesho na utoaji wa taarifa kwa wananchi ili kuepusha vitisho, migogoro na adhabu zisizoeleweka.

Tunaiomba Serikali ifuatilie malalamiko haya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma yenye haki na heshima.
 
Hiyo 80 ulipewa risti nje ya hapo na wewe ni mtuhumiwa.
 
Back
Top Bottom