Mji Mdogo Italia washerekea kuzaliwa kwa Mtoto

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Mji mmoja mdogo kaskazini mwa Italia unasherekea kuzaliwa kwa mtoto kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1980.

Meya wa mji huo wa Ostana, uliopo kwenye milima ya Piedmont amesema kuzaliwa huko ni "ndoto kuwa kweli" kwa jamii hiyo ambayo imeshuhudia idadi yake ya watu kupungua katika kipindi cha miaka 100 iliyopita.

Mtoto huyo, Pablo, ambaye alizaliwa katika hospitali ya Turin wiki iliyopita, sasa anafikisha idadi ya wakazi wa mji huo kuwa 85, ingawa nusu ya wakazi hao hawana makazi ya kudumu mjini humo, limeripoti gazeti la La Stampa.

Meya huyo Giacomo Lombardo amesema ingawa watu 1,000 walikuwa wakiishi Ostana katika miaka ya 1900, uzazi ulianza kupungua baada ya Vita vya Pili vya Dunia. "

Idadi hasa ilianza kuporomoka mwaka 1975, ambapo watoto 17 walizaliwa kati ya 1976 na 1987, na mtoto wa mwisho alizaliwa 1987 kabla ya kuzaliwa kwa Pablo" amesema meya.

Miji midogo nchini Italia inakabiliwa na kupungua kwa idadi ya watu, kutokana na vijana wengi kuondoka kwenda kutafuta kazi.

Baadhi ya miji imejaribu mikakati ya hata kutoa nyumba bure, huku meya wa mji mmoja akipiga marufuku watu kuugua, ili kudhibiti upunguaji wa watu.
 
Huko ndo ningefaa mie kuishi, napenda sana kuwa mwenyewe mwenyewe. Nimezoea kwenda out mwenyewe picknic mwenyewe, kusafiri long drive mwenyewe.
 
amepiga marufuku watu wasiugue?au nimesoma vibaya.....waje africa kuna watoto wengi wamtaani wawachukue
 
amepiga marufuku watu wasiugue?au nimesoma vibaya.....waje africa kuna watoto wengi wamtaani wawachukue
Hahahaaa! Eti amepiga marufuku watu kuugua!! Ina maana kabla ya hapo watu walikuwa wanaugua kwa mamlaka yake?! Tusubiri siku akiugua huyo Meya itakuwa kavunja sheria aliyoiweka yeye mwenyewe,halafu huyo Meya hakusema ni adhabu gani mtu ataipata ikiwa atavunja amri ya kutokuugua!! Labda angazifunga Hospitali zote! Huyo Meya Bangi inampeleka pabaya Aisee!!
 
Back
Top Bottom