Mjengo wa Ajabu anaomiliki Mh. Sitta Huu hapa

Status
Not open for further replies.
Tatizo ni fikra potofu kwa hao akina 6.Ngoja akose ubunge uonee kama atakuwa na hamu ya kukaa humo.
 
Mmmmmh eti kufuru🏃hiyo nyumba ni kufuru? Ngoja wakuonyeshe hao majambazi wenye kufuru za kweli.... Acheni mbwembwe, unasema kufuru ya mtu mwenye upeo wa kujua thamani ya mahali pa kuishi au uhalali wa kuipata? Sijaona logic
#uhalali ndio ishu, kachunguze kama si halali ndio upost tena
 
MKUU Hii picha imepigwa kwa mbali na hakika mimi niliwahi kukatiza hapo mtaani kwake kwa kweli ni kufuru,hii nyumba huwezi kuamini imejengwa na mtumishi wa sirikali anayepangiwa mshahara,ni hatari sana na hapa kina ufisadi wa kutisha.6 hafai hata uenyekiti wa kitongoji.

Akili ni nywele.... Unajua sitta ni mfanyakazi wa serikali kwa miaka mingapi? Ngazi gani? Mshahara gani? Aaaahahahahaha asingekuwa na mahali bora pa kuishi angekuwa ----- maana mishahara yote tangu sijazaliwa angekuwa ametupa chooni, achilia mbali mafao, malupulupu,biznes zake .... Acheni mawazo ya kimaskini... Niambieni kuhusu uhalali wa kuwa na hiyo nyumba kama hakupata fedha kwa uhalali, zito tu ana miaka michache ameizidi hiyo........
 
Habari wana JF,

Ebu angalia mjengo wa ajabu wa kutisha anaomiliki Mh. wa Viwango na Speed,Mjengo upo Mbweni 2km from Ndege Beach,Mjengo upo kwenye kiwanja cha sqm 3000,Ukuta wake na garden ni kufuru,Nimeshindwa kuweka,kwa sababu za kiusalama,Kuna HD CCTV Camera with Night Vision,StandBy Generator 20KvA,Tumemkabidhi kuendesha muimili wa Dodoma kafanya haya,Je tukimkabidhi aendeshe muimili wa Magogoni si itakuwa balaa?

View attachment 248668

View attachment 248670

BR,
The Cat.

Nadhani na mbinguni washajijengea masaki ya vigogo
 
Mapanya wanashindana kuiba kwa kuwa wamefanikiwa kuwarubuni watanzania basi wanatusilisi.

katika bajeti matumizi ni makubwa mipango ya maendeleo haipewi kipaumbele wanatafuna rasilimali kama wadudu wa chooni bajeti 2015/2016 23 trilions vs 5trilions for development plans
 
Mbona kuna wachagga wengi sana wako serikalini wananyumba zaidi ya hiyo? Ni vitu vya kawaida. Huwezi kukuta mchagga anategemea mshahara tu peke yake......Anafuga mifugo, mashamba, biashara nk. Kwa kuwa Sitta ni mnyamwezi hamuamini kuwa anaweza kuwa na biashara zingine?
Ni kweli kwa juhudi mtu anaweza kujenga jengo zuri tu. Vile vile ni haki Mh Sitta kujejnga jengo lenye hadhi au mtumishi mwingine ye yote.
Ikiwa tunataka watumishi wafanye kazi kwa kiwango stahili ili taifa liendelee ni vigumu wakati huo huo tuwatazamie kufanya shughuli nyingine kubwa. katika utumishi wa umma kuwa na nyumba ya mil. 50 au zaidi kidogo si mbaya sana. lakini nyumba inafika hadi bilioni ni wazi hapa kuna kitu kimejificha. watu wanaolipwa sana sana ni mil. 3 kwa mwezi sawa na mil. 36 kwa mwaka sawa na mil. 360 kwa miaka 10. lakini mtu huyo huyo ana gari mil 100 nyumba za kufa mtu. KUbali kataa hapa kuna tatizo na si suala la miradi pekee. utahitaji kuuza ng'ombe wangapi ili ujenge nyumba ya mil. 300?
 
Huyo mchaga ni muhindi? Mbona kuna mdau amesema anakaa mhindi? Kama ni ya mchaga halafu ni rafiki yake nenda kapige picha ya mbele ndio tutaamini kweli siyo ya sita ni ya mchaga.

mbweni hii ya ndege beach hakuna mhindi anaeshi kule kaka. huwa tunajuana kwa kiasi kikubwa.
 
Haikuti mahekalu ya Lowassa! Manake ni mengi! Kama Sitta hafai kwa kimiliki kagorofa kamoja mbweni Lowassa ni wa kikimbiza kabisa!
 
Mleta mada anaonekana hajatembea ajionee Nyumba ndani ya nchi yake. Tulia tafuta pesa kwa bidii
 
Safi sana wenzenu wanajenga nyie mnahongea mtasema sana mwaka wewe unamademu sita utajenga lini?
 
Haikuti mahekalu ya Lowassa! Manake ni mengi! Kama Sitta hafai kwa kimiliki kagorofa kamoja mbweni Lowassa ni wa kikimbiza kabisa!
Weee ! unasema kweli mkuu ? lakini huyu si wanasema ana utajiri wa ng'ombe 8000 ( miaka yote hawapungui wala hawaongezeki ! )
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom