Mjadala wa ukosefu wa ajira {our strength)

Mjadala wa ukosefu wa ajira {our strength)

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,672
Reaction score
4,560
Limekuwepo tatizo la ajira nchini kwa kipindi kirefu,hata hapa jamiiforums kuna idadi ya watu ambao hawajaajiriwa au kujiajiri.ukienda kwenye jukwaa la Biashara na fursa za kiuchumi hapa Jamiiforums utakutana na michanganuo mingi ya jinsi ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo lakini changamoto kubwa inakuwa jinsi ya kupata fedha za mtaji yaani (Capital).Ningependa kuwasilisha hoja binafsi hapa jukwaani ili ikiwa na mashiko iweze kuibua mjadala utakaosaidia kupunguza tatizo hili .

Kutokana na taarifa kutoka google mtandao wa jamiiforums una watumiaji zaidi ya laki nne hawa ni registered users,kama kila mtu akitoa shilingi Elfu moja itakuwa ni jumla ya shilingi milioni mianne yaani [400000*1000=400000000].Na fedha hii ikiwa elfu 10 kwa kila mwana jamiiforums itafikia shilingi bilioni nne fedha ambazo zainaweza kutumika kuanzisha miradi mbalimbali .

Nimefikiria wazo hili kwakuwa hapa jamiiforums tumekuwa kama ndugu na hivyo pamoja tunaweza kujadili changamoto mbalimbali zainazotukabili,ikumbukwe kuwa tuna wataalamu wa kutosha wa kila idara ikiwemo uhasibu,ualimu,udaktari,ufundi mbalimbali,sheria,madini,biashara kwa ujumla,uwekezaji, na zangine nyingi na hii itakuwa fursa ya kuutumia utaalam wao kwa manufaa mapana ya taifa na mtandao huu kwa ujumla.Wanansheria wanaweza kutusaidia kuandaa andiko la kuanzishwa kwa kampuni au saccos au kwa namna yoyote itakavyokubalika na katiba itakayotuongoza na chombo hicho kijielekeza kuinua uchumi wa wanachama na kijitegemee kiuendeshaji .

Kwa hali ya kawaida ni ngumu ila kwa nia thabiti tunaweza kwa pamoja kutumia utaalam tulionao na ushirikiano wetu kuhakikisha tunafanikiwa,hivyo basi nawakaribisha kwa michango yenu,kwa jinsi gani tunaweza kupunguza tatizo hili la ajira au kwa namna gani tutashirikiana kulipunguza tatizo hili .

Niko tayari kukosolewa,kupokea mawazo mbadala na fikra mpya juu ya swala hili hivyo karibuni kwa michango ya mawazo .Mods muiweke ifikie wanajamii wote Mshama Jr Maxence Melo Ontuzu the banker The bold Nifah Zitto zitto junior Mtzed Wakiafrika King Bannizzo JamiiForums MODA Watunduru DeepPond An Enterpreneur mmuru ericka mtzmweusi Mo Genius Gebo2 Leyaleah na wanachama wote wa JF .

GIRLAND
 
Good idea, katika hili unahitajika utashi wa hali wa hali ya juu.
Ushauri kabla ya kuchangisha tupate aina ya biashara, then tupate tathimini kwa ujumla hapo tunaweza kutembezeana kapu
 
Good Idea!!!

Sasa ni hivi, tuanzie hiki kitu kwa muanzisha mada awatangazie wote wenye nia ya kufanya kitu tujiandikishe/tuonane na kuanza mikakati ya hiki kitu. Tegemea majibu kwa wanaojielewa na wasiojielewa lakini mwisho wa siku tutapata kundi lenye nia moja na kitu kitafanyika!
 
Good idea, katika hili unahitajika utashi wa hali wa hali ya juu.
Ushauri kabla ya kuchangisha tupate aina ya biashara, then tupate tathimini kwa ujumla hapo tunaweza kutembezeana kapu

good! ila nafikiri kabla ya kujua ni biashara gani, tungepata kundi la wenye nia. ikiwezekana watu tukutane hata kama ikiwa ni kwa mafungu mafungu kutokana na sehemu tunazoishi. Tujipangie mikakati ya mwanzo ya kukutana kwetu. Mwanzo utakuwa mgumu lakini tutakaa sawa
 
Changamoto ninayo ona ni idadi yetu kuwa kubwa na kama ni kubwa na tuna aim tufanikiwe basi na huo mchango inabidi uwe mkubwa /all in all is a good idea
 
Good idea, katika hili unahitajika utashi wa hali wa hali ya juu.
Ushauri kabla ya kuchangisha tupate aina ya biashara, then tupate tathimini kwa ujumla hapo tunaweza kutembezeana kapu
asante ndugu plainpaper karibu kwa mawazo zaidi
 
Changamoto ninayo ona ni idadi yetu kuwa kubwa na kama ni kubwa na tuna aim tufanikiwe basi na huo mchango inabidi uwe mkubwa /all in all is a good idea
Hicho kiwango 10000 kimekadiriwa kuweza kutolewa na yoyote ila mawazo zaidi yanakaribishwa
 
Mods mnaweza kunisaidia kuwatag JF wote tafaadhali
 
Idea ina mashiko nadhani ni jambo zuri tunaweza kufanya kitu kama wote tutakua na nia moja.. Tufahamiane wenye nia za dhati kwanza ili tuweze kutengeneza jumuiya ya watu wataokua tayari kupigania kile tunachokiamini... Who knows a couple of years later we might be the new faces on forbes magazine..
 
I'm inn.

Haya profession zitumike kuliweka hili wazo sawa na lenye kuishi
 
Asante kwa mchango wako ,Lets do it.
 
I'm inn.

Haya profession zitumike kuliweka hili wazo sawa na lenye kuishi
Kweli kabisa kila mtaalamu atatusaidia ,nafikiri baada ya kutambua wenye nia ya dhati mengine yatafuata.
 
Back
Top Bottom