Mbavu mbili
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 1,457
- 874
Wakuu
Nimetafakari sana wazo la kuanzishwa shule za Kata na kubaini kuwa lilikuwa zuri, licha ya changamoto za hapa na pale. Ni dhahiri tangu kuanza kwake zimesaidia Watanzania baadhi kutimiza ndoto zao za kielimu.
Ukichunguza shule hizi zimejengwa walau karibu kila kata kuanzia mijini hadi vijijini. Pia kumekuwa na idadi ya wanafunzi wengi wanaofeli mitihani ya kidato cha NNE ukilinganisha na idadi ya ufaulu wao.
Wazo langu:
Tubadili baadhi ya shule za Kata ziwe shule za Ufundi. Wanafunzi watakaofeli kidato cha PILI na cha NNE wahamishiwe katika shule hizo Mpya za ufundi. Huko masomo mbalimbali ya ufundi yafundishwe kwa miaka mitatu au miwili.
Ninafikiri hili litasidia sana kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira nchini mwetu. Pia litaongeza uwezo wa vijana kujitegemea wao wenyewe pindi wamalizapo masomo yao, na Mwisho itapunguza athari mbaya za makundi ya vijana wanaomaliza kidato cha NNE na kupata alama zisizokuwa na msaada wowote katika maisha husika.
Imani yangu ni kuwa si kila mtoto anayefeli masomo darasani basi hana uwezo wa kujifunza masuala mengine katika maisha. Hili litaongeza idadi na chachu ya vijana wasio tegemezi .
Ni imani yangu Shule hizi zikitumika vizuri zitalikomboa taiifa katila masuala mbalimbali.
Naomba kuwasilisha.