MJADALA HURU:- Said Issa Mohamed

MJADALA HURU:- Said Issa Mohamed

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
1,487
Reaction score
913
Ndugu wanajamvi ..

! Ukweli tuuseme tu SINA mistari Mingi ya kumuelezea Makamu Mwenyekiti wa CDM Zanzibar, Said Issa Mohamed, lakini siku Moja nilibahatika kusikia interview Yake Na waandishi wa habari Kwenye uwanja Wa Ndege Zanzibar akijiandaa Na Safari ya kichama nje ya nchi..juu ya Udini unaoongelewa Ndani ya Chama.

Kichwa hiki Kiliongea point sana, nadhani ni moja Kati ya Hazina safi kabisa Chadema. Embu anaejua zaidi atujuze Ndani ya mhadala huru .
Swali: Unazungumziaje suala la chama chenu kudaiwa kuwa na udini, ukabila na ukanda? Dini yenyewe inayozugumzwa ikiwa ni Ukristo wa madhehebu ya Katoliki na inasemekana mmewekwa pale kwa ajili ya kuficha madai hayo?

Mohamed: Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukuongoza kuniuliza hayo, hapo kuna maswali matatu, nitakujibu kila swali kwa nafasi yake, nikianza na suala zima la udini.

Kama watu wanafuatilia historia ya kuanzishwa kwa vyama vingi na wakaamua kukataa propaganda zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali nzima basi watabaini kuwa hakuna kitu kama hicho kwa Tanzania, ila waliofilisika kisera wanataka kutumia turufu hiyo ya udini kama nafasi ya kuonewa huruma katika jamii.

Nasema hivyo kwa sababu mtiririko mzima wa uongozi ndani ya CHADEMA, kuanzia kuasisiwa kwake haukuwa wa kuangalia dini bali uwezo wa mtu, na katika hili linadhihirishwa na namna uongozi ulivyokuwa tangu mwanzo hadi sasa, mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA alikuwa mzee Edwin Mtei.

Huyu ni Mkristo na katibu mkuu alikuwa mzee Ally Nyanga Makani ‘Bob Makani’, huyu ni Mwislamu, naibu wake kwa Bara alikuwa mzee Saidi Arfi, naye huyu ni Mwislamu na kwa viongozi waliotoka Zanzibar wote walikuwa Waislamu.

Awamu ya pili, mwenyekiti alikuwa Bob Makani, makamu Dk. Willbrod Slaa na katibu mkuu alikuwa Amani Walid Kabourou.

Awamu ya tatu, mwenyekiti wetu alikuwa Freeman Mbowe, makamu Kabourou, katibu mkuu, Dk. Slaa, katika nafasi ya makamu mwenyekiti hapa alikuwa Shaibu Akwilombe na baadae akawa Chacha Wangwe (marehemu).

Awamu hii tunayokwenda nayo sasa, Mbowe ameendelea kuwa Mwenyekiti, Makamu wake Bara ni Said Arfi, Zanzibar ni mimi, Katibu Mkuu ni Dk. Slaa, Naibu wake Bara ni Zitto Kabwe na Zanzibar ni Hamad Yusuph, hapa utaniambia Ukristo na huo Ukatoliki uko wapi?

Pia ukiangalia namna viongozi walivyo kuanzia mwanzo, hakuna safu nzima ya viongozi wakuu waliotoka kanda moja au kabila moja.

Kama kungekuwa na udini katika CHADEMA huo unaosemwa, basi Waislamu wasingepita na kuwa katika nafasi walizonazo leo, kwa kuwa nafasi zote za juu ni za kupigiwa kura.

Swali: Sasa unafikiri kwanini mambo hayo yanazungumzwa kuhusu ninyi na si vyama vingine?

Mohamed: Sasa hivi CHADEMA tupo katika mioyo ya watu na hili ni tishio kwa chama tawala, kama utakumbuka wakati ule CUF ilipokuwa juu waliambiwa ni chama cha kigaidi, cha Waislamu na mwisho kikaitwa cha Wapemba, nao walikubaliana na propaganda hizo pasipo kujua kuwa zinawamaliza, unaona leo wameshuka wale waliowazushia hawaoni tishio la CUF tena, sasa wameivamia CHADEMA.

Hii ni baada ya kutangazwa Kwa Dk. Slaa kuwa mgombea wetu mwaka 2010, lengo lilikuwa kuwagawa wananchi na kisha wawatawale, serikali inafanya hivi makusudi kwa kutumia idara zake za usalama ambao hawataki kutambua kuwa wapo kwa ajili ya masilahi ya taifa na si chama cha siasa.

Watanzania wanapaswa wajiulize kama CHADEMA kinasemwa ni cha Wakristo, CUF ya Waislamu na CCM itakuwa ya dini gani? Au hao wenye dini hizo zinazotajwa kuwa ni za CUF na CHADEMA wanajipendekeza ndani ya CCM?
 
Sisi hatujui ila kwa vile ulisikia interview yake basi wewe ndio utuelezee kwa ufasaha nini kasema,maana sisi hatujui tutakujuvya nini??
 
Kuna Mbunge Viti Maalumu wa chadema anayetoka Zanzibar??
 
Ndugu wanajamvi ..

! Ukweli tuuseme tu SINA mistari Mingi ya kumuelezea Makamu Mwenyekiti wa CDM Zanzibar, Said Issa Mohamed, lakini siku Moja nilibahatika kusikia interview Yake Na waandishi wa habari Kwenye uwanja Wa Ndege Zanzibar akijiandaa Na Safari ya kichama nje ya nchi..juu ya Udini unaoongelewa Ndani ya Chama.

Kichwa hiki Kiliongea point sana, nadhani ni moja Kati ya Hazina safi kabisa Chadema. Embu anaejua zaidi atujuze Ndani ya mhadala huru .

Ni sawa mkuu uko sawa., lakini sitegemei kutokea kiongozi wa siasa atakayeulizwa suala kuhusu chama chake ni cha kidini akaunga mkono., yeye anafahamu hivyo lakin pengine na jengine lipo
 
Wala hatotokea hd chama kitakufa.

Tukusema magamba hamna uelewa mnabisha? Kazi yenu kuropoka ropoka tu kama wenda wazimu vile.Ndiyo maana nakubaliana na ile slogan kuwa ukiona kijana yupo ccm siyo bure ujue tahira hiyo na wala hajitambui. Wamekujibu sasa wewe kenge kabisa.
 
Ndugu wanajamvi ..

! Ukweli tuuseme tu SINA mistari Mingi ya kumuelezea Makamu Mwenyekiti wa CDM Zanzibar, Said Issa Mohamed, lakini siku Moja nilibahatika kusikia interview Yake Na waandishi wa habari Kwenye uwanja Wa Ndege Zanzibar akijiandaa Na Safari ya kichama nje ya nchi..juu ya Udini unaoongelewa Ndani ya Chama.

Kichwa hiki Kiliongea point sana, nadhani ni moja Kati ya Hazina safi kabisa Chadema. Embu anaejua zaidi atujuze Ndani ya mhadala huru .

mbona pointless tupu. Aje agombee bara ndio atajijua yeye ni kichwa au maka...lio.
 
Back
Top Bottom