Mizimu Iliyowekwa Kwenye Vichupa Yapigwa Mnada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizimu Iliyowekwa Kwenye Vichupa Yapigwa Mnada

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Mar 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;"></td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Vichupa viwili vyenye mizimu inayopigwa mnada</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Monday, March 08, 2010 12:26 AM
  Mizimu miwili iliyokamatwa na kuingizwa kwenye chupa wanapigwa mnada kwenye internet na mamia ya watu wamejitokeza kuinunua mizimu hiyo.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Mwanamke wa nchini New Zealand, Avie Woodbury anawapiga mnada mizimu waliokuwa wakimsumbua kwenye nyumba yake ambao walikamatwa na mchungaji wa kanisa moja nchini humo na kuingizwa kwenye vichupa viwili vidogo.

  Avie ameweka tangazo kwenye internet akivipiga mnada vichupa viwili ambavyo anasema vina mizimu iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu.

  Avie alisema kuwa mizimu hiyo ilikamatwa na kuwekwa kwenye vichupa vidogo vyenye maji matakatifu.

  "Maji matakatifu yanawafanya mizimu waishiwe nguvu na kuwafanya walale muda wote", alisema Avie.

  Avie ameweka tangazo lake kwenye tovuti ya minada inayoitwa TradeMe. Hadi sasa dau kubwa alilopata ni paundi 1,000.

  Avie amedai kuwa tangia mizimu hiyo ilipowekwa kwenye chupa mwezi julai mwaka jana hajapata usumbufu wowote kwenye nyumba yake kama ilivyokuwa zamani.

  Mmoja wa mizimu hiyo anadaiwa kupenda kuviangusha vitu na kuzima na kuwasha vitu vya umeme. Mzimu mwingine unadaiwa kupenda kuwatisha watu.

  Ili kuizindua mizimu hiyo Avie amesema kuwa ameambiwa kuwa ayamimine maji yaliyomo kwenye vichupa hivyo kwenye dishi na ayaache maji hayo yayeyuke ndani ya nyumba anayotaka mizimu hiyo ikae.

  Chupa za mizimu hiyo zimewekewa majina maalumu ili wanunuzi wajue wanamnunua mzimu yupi.

  Mnada wa mizimu hiyo umevuta watu wengi na umebakiza siku mbili kabla ya mshindi mwenye dau kubwa kuondoka na vichupa vyenye mizimu hiyo.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">
  </td></tr></tbody></table>
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...