Miundombinu: Zaidi ya kaya 300 zilizojengwa ndani ya hifadhi ya TAZARA kubomolewa

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
304
236
ZAIDI ya kaya 300 ambazo nyumba zao zimejengwa ndani ya Hifadhi ya Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), kuanzia jijini Dar es Salaam hadi Tunduma, ziko hataraini kubomolewa ili kupunguza ajali zinazotokana na uharibifu wa miundombinu ya njia hiyo.

Wakizungumza na FikraPevu jijini Dar es Salaam, leo Juni 5, 2014 wananchi wanaotakiwa kuondoka katika hifadhi hiyo, wamesema wanashangazwa kuona wanatakiwa kuondoka wakati wamekuwepo katika maeneo hayo kwa muda mrefu.

TAZARA-Tangazo.jpg


"Hatutaweza kuondoka katika nyumba zetu kwamaana tumekuwepo kwa muda mrefu sasa wanavyotuambia tuhame kwasababu ya hiyo miundombinu hawaoni kuwa hata kama hi hizo fidia zao hazitatosha wala kukidhi mahitaji yetu? Waambieni hatutaondoka kwa maana sisi hatuna sehemu ya kujisemea zaidi yenu wanahabari" alisema mmoja wa wananchi hao.

Soma zaidi => Miundombinu: Zaidi ya kaya 300 zilizojengwa ndani ya hifadhi ya TAZARA kubomolewa
 
Back
Top Bottom