KERO Miundombinu ya soko la Buguruni ni hatari kwa afya ya watumiaji

KERO Miundombinu ya soko la Buguruni ni hatari kwa afya ya watumiaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Apr 23, 2019
Posts
67
Reaction score
90
Habarini wanajukwaa, leo nmekuja kuwasilisha changamoto na baadhi ya kero katika soko la Buguruni.

1. Soko linamiundo mbinu ya kizamani sana ukilinganisha na idadi ya watu inaowahudumia, ukitazama njia za kupita (kupishana) ndani ya soko kwa sasa ni vichochoro, vizimba vidogo mno kiasi kwamba wauzaji wanaweka vitu kwenye njia za wapita kwa miguu hali inayoongeza msongamano.

2. Hali ya usafi wa vyoo na mifumo ya mashimo ya kunyonyea kinyesi baadhi yake ipo upande wa sokoni mvua ikinyesha inatapika na kuingia sokoni

3. Mvua ikinyesha soko linajaa maji na matope hapapitiki na vyakula vinakua katika hali ya uchafu na hatarishi kiafya.

NATOA WITO KWA MAMLAKA WASHUGHULIKIE KERO HIZO, LILE SOKO LINATOA MAPATO MAKUBWA SANA KWA MIZIGO INAYOINGIA NA KUTOKA PALE.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom