Miundombinu Kahama mjini bado changamoto

Miundombinu Kahama mjini bado changamoto

MWAKATA KWETU

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
560
Reaction score
320
Mji wa Kahama ndio mji unaokua kwa kasi kubwa kanda ya ziwa na Magharibi mwa Tanzania.Sifa kubwa ya mji huu ni kilimo na biashara,.

Upande wa kilimo zao la mpunga ndio limepewa kipaumbele kikubwa sana kutokana na kutoa ajira kubwa kwa vijana ila cha kushangaza mji huu suala la miundombinu hasa pembeni mwa mji ni shida.

Nashauri wahusika especially TAMISEMI liangalieni hili ni aibu.
 
Ni aibu Kahama iko vizuri hata uchangiaji WA pato la taifa ila kimiundo mbinu iko nyuma sana .tatzo viongozi ni tatzo halmashauri..na aina ya wabunge ambao huwa tunachangua nao wanachangia kwa uzolotoshaji WA miundo mbinu.
 
Hii barabara ya busisi msalala kahama, ni noma, nadhani toyota wakiiona mashindano ya paris capetown yatapitia huko. Kutoka kahama geita utadhani unaenda juba.
 
Chakushangaza 80% ya dhahabu inatoka eneo hili, makao makuu ya wilaya ya msalala yako kahama mjini, hata mbunge hana nyumba huko.
 
Barabara ya bukondamoyo kwenda wilaya mpya ya ushetu mkuu aliahidi lami mpaka sasa wananchi wanapigwa vumbi...
Wakati barabara hii inaingiza mazao mengi kama tumbaku,pamba,karanga n.k
 
Nasikia kuna shortcut nyingine kutokea hapo mjini hadi mwanza kwa basi unatokea misungwi ni kama masaa mawili, kwa nini isiboreshwe kahama ikawa na direct link na mwanza au wanaogopa shinyanga itakufa. Ni mji pekee usiojaliwa lakini una potential ya kuiingizia tanzania mabillioni. au kuwa Hub kubwa ya kibiashara na nchi za maziwa makuu
 
Barabara ya bukondamoyo kwenda wilaya mpya ya ushetu mkuu aliahidi lami mpaka sasa wananchi wanapigwa vumbi...
Wakati barabara hii inaingiza mazao mengi kama tumbaku,pamba,karanga n.k
Hii barabara nimepita juzi juzi tu nilikuwa naekea Nyamilangano aisee sijaona hata kipande cha rami wakati kuna tumbaku na pamba nyingi sana inalimwa ushetu
 
Hii barabara ya busisi msalala kahama, ni noma, nadhani toyota wakiiona mashindano ya paris capetown yatapitia huko. Kutoka kahama geita utadhani unaenda juba.
Na magari huwa yanakimbia sana vumbi tupu
 
Ila kahama ikiwekewa miundombinu safi hasa barabara ndio kilio kikubwa baada ya miaka kadhaa kahama naiona mbali sana.
Kahama ipo vizuri kibiashara,pia kielimu naona inakuja vizuri sana matokeo ya darasa la saba wananafunzi 7 kwenye kumi bora tz wametoka kahama na wote wanatoka kwema medium school.
Hivyo muingiliano wa watu ni mkubwa wanaoingia na kutoka leo mabasi yaendayo dsm kutoka khm ni zaid ya 9 na yote yanajaa lakini shy hakuna hata basi linaloanzia safari pale.
Kunahitajika viongozi wenye utashi na uchungu na hii wilaya
 
Back
Top Bottom