Miundo mbinu ya kisasa na umuhimu wa elimu ya jinsi ya kuitunza

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Serikali ya CCM ambayo imekuwa ikijivunia wingi wa wawekezaji wanaozidi kuja nchini inayo changamoto kubwa inayoambatana na uwekezaji mkubwa.

Miundo mbinu mingi inazidi kujengwa, hii ni hali ambayo inaambatana na dunia ya sayansi na teknolojia. Ukuaji wa sekta nzima ya ujenzi huambatana na umuhimu wa wananchi kuelemishwa kwa mapana, faida na hasara za kutoitunza miundo mbinu mipya.

Haiwezekani serikali ikajisifu kupokea uwekezaji mkubwa halafu ikaendelea kutumia njia zile zile dhaifu za uelimishaji umma juu ya umuhimu wa kuiona miundo mbinu kama ni mali ya kila mlipa kodi.

Nchi za dunia ya kwanza zimeshayazoea maisha ambayo wananchi wanazungukwa na miundo mbinu ya thamani kubwa, lakini huwezi kuona hujuma za kijinga zikifanyika mara kwa mara. Ni kwa sababu umekuwepo utashi wa kisiasa wa kila chama kinachokuwa madarakani, katika kuhakikisha wananchi wanadumisha uhai wa miundo mbinu waliyonayo.

Uwekezaji mkubwa unaidai serikali ile hali ya kuongeza njia mbalimbali za kuelimisha watumiaji wa miundo mbinu inayojengwa kwa fedha nyingi, ili iweze kudumu kwa miaka mingi.

Prof Ndalichako na wasaidizi wako, kaeni chini mfanye kikao kirefu juu ya umuhimu wa elimu ya utunzaji wa miundo mbinu. Watoto waanze kupewa elimu ya kuiona miundo mbiinu kama ni mali inayowahusu moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom