albuluushiy
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 1,404
- 687
Nikiwa na masuali mengi kichwani na moyoni mwangu nimekuwa nikijiuliza na kuwaza lakini pia nakukumbuka zile enzi za mapambano ya kisiasa zidi ya vyama viwili vikubwa vya kisiasa kule kwetu Zanzibar C.C.M na C.U.F .Licha ya vituko na vichekesho lakini pia maudhi pamoja na kejeli yalinipa taaswira ambayo nitashindwa kuisahau maishani mwangu.
Nilishuhudia baadhi ya jamii ya watu hususani Wapinzani wa Serikali wakipata kile kilichoitwa joto ya jiwe lakini pia kwa wale majirani zetu kutoka kisiwa cha pili wakifungishwa virago na mbwa na mito akiongozwa kuelekea bandarini ili kuelekea kwao walikotoka yaani Pemba huku nyimbo na chereko zikirindima waso haya wana mji wao, kwa kweli hali hii ilinisononesha sana.
Yote haya yaliokuwa yakitokea Zanzibar, serikali ilikuwa kimya na hakuna kiongozi yeyote wa Serikali ambae alikemea hali hiyo ,fikra zangu ni kwamba wale wote waliohusika kutenda yale walifanya kwa bahati mbaya au pengine hamasa za kisiasa tu kibinaadam,hilo lingewezekana.Lakini baada ya kuona majadiliano kwenye mchakato wa katiba mpya na baadhi ya hoja za Wajumbe wa chama cha mapinduzi nimepata majibu ya masuala yangu yote yaliokuwa yakinisumbua.
Ni dhahiri kwamba vitendo vile vya kiharamia walivyokuwa wakifanyiwa baadhi ya Wapinzani na hasa ndugu zetu kutoka Pemba havikuwa kwa bahati mbaya bali ni sera maalum zilizoratibiwa na Chama chetu cha Mapinduzi na Serikali zake mbili kwa malengo maalum.Na ndio maana ukaona ya kwamba baadhi ya ya Viongozi wakuu wa Serikali wamefikia mahali wameshindwa kujizuia badala yake wanatoa kejeli, vitisho.vijembe,matusi pamoja na vitisho hadharani kama vile vijana wao wa Maskani wanavyofanya.
Kwa mimi kama raia napata picha halisi kwamba C.C.M na serekali zake zinaendeshwa kwa Miujiza. Nasema ni miujiza kwa sababu ni hivi karibuni tu tulimsikia Rais wa Nchi akiwakejeli jamii ya Watu wa Wapemba "walima vitunguu" lakini kama hilo halitoshi,tumeshuhudia katika bunge la kutunga sheria maneno ya kejeli na matusi ni yale yale, hii ni kusema huo ndio msimamo wa Serikali kwa jamii ya Wapemba kwamba hawana kheri waende kwao.
Lakushangaza, na la ajabu zaidi ni kuona Viongozi hao hao wanapanda madege na mameli kwenda kwa jamii ya Wapemba wanaowatukana kila uchao na huku wanawachukia kuliko kitu chengine chochote kile, hivi tuseme kulikoni ? Ama kweli huu ni muijiza wa C.C.M.
Kuna haja gani ya nyinyi kuwafuata kwao na ili-hali wao hawana haya wanamji wao na nyinyi muna miji yenu bora ? Hivi tuseme leo wamekuwa wema au munawapenda kiasi gani ?
Huu ni miujiza kweli wa Serikali zetu mbili '.
Wapemba jibu munalo wenyewe.