Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa Watanzania

Unapata mkuu ukiwa fresh wacheki jamaa wa Autocom Japan wanabei nzuri. Mfano Mitsubishi Outlander ya 2010 ukiikuta Befoward bei inakuwa tofauti na Autocom kwa tofauti ya $ hata 800 au 1000 ni vile maraia wamekariri Befoward na kwingine
Mkuu hao autocom wana office zao hapa Tanzania au u a deal nao vip kuamini wanakuleta ndinga nq si janja janja.
 
Gari nzuri zisizoongelewa sana na wabongo

Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana, ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa watanzania.

Gari hizi zinavitu vingi sana ambapo gari nyingine kama Toyota huwezi pata hasa ukilinganisha bei yake.

Mitsubishi outlander 2006 - 2015
1. Ni gari inakuja na charging system ya laptop, yaani unaweza kuchomeka switch sockate na ukaweka charger yako vizuri... Kwa kifupi gari hili linabadili umeme wa dc kwenda ac.

Kwa watu wanaopenda kutumia laptop wakiwa safari hii gari unaweza kutumia laptop toka Dar mpaka Mwanza, bila kuizima unafanya kazi tu au unaangalia series.

2. Gari hii inakuja na kifridge kidogo kuweka vivywaji uwapo safarini.

3. Gari hii ina option ya 4WD

4. Gari hii inakuambia muda wa kupumzika ukichoka safarini.

5. Gari hii inakuja na mziki mziti yaani subwoofer isiyojaza buti.

6. Gari inakuja na seat 7.

7. Gari hii ina option ya manual na automatic.

8. GARI hii ina gear 6, inaifanya itumie mafuta kidogo.

Hii gari bei yake ipo chini ya kina harrier, kulger na Vanguard. Kitu ambacho hivi vitu vyote vingekuwa kwenye hizo gari bei zake zisinge shikika.
Zitasikikaje kama hata kuonekana kwa picha tu hazionekani
 
Shukrani mkuu
Tawacheki mwishoni mwa Nov waniletee hiyo chuma
Good tena ingia kwenye web yao chagua ndinga unayoitaka, kwa kawaida ukishajiunga kwenye web yao ukawa member hapo hapo unapigiwa simu na sales manager aliyeko online mtazungumza kama ni mambo ya discount, rangi ya gari, unataka gari liweje nk.

Mwisho wa siku utafanya malipo kwenye account ya kampuni unamtumia TT au mnaita pay slip then mchakato wa kulisafirisha unaanza.

NB: Asitokee mtu akakwambia nipe hela nikakulipie, nenda bank mwenyewe lipa then sikilizia chuma ipakiwe kwenye meli mwisho kabisa muulize huyo sales manager auction grade ya gari, nakushauri grade iwe kuanzia namba nne 4. (Hii ni gari yenye hali nzuri kuanzia engine hadi body)

Autocom wanagrade gari zao kwa namba, ikiwa ndogo mfano #1 inakua worse 2 ina nafuu, kuanzia namba nne hadi tano ni almost brand new car.

Kila la kheri mkuu
 
Mkuu hao autocom wana office zao hapa tz au u a deal nao vip kuamini wanakuleta ndinga nq si janja janja.
Hakuna janja janja jamaa wako smart hakuna longolongo, nishaagiza gari kwao zaidi ya mara mbili. Mimi huwa naingia kwenye website yao sijawahi kutumia ofisi zao za Dar. Isitoshe nna account kwenye website yao

Hakuna ubabaishaji ni hayo tu.
 
Gari nzuri zisizoongelewa sana na wabongo

Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana, ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa watanzania.

Gari hizi zina vitu vingi sana ambapo gari nyingine kama Toyota huwezi pata hasa ukilinganisha bei yake.

Mitsubishi outlander 2006 - 2015
1. Ni gari inakuja na charging system ya laptop, yaani unaweza kuchomeka switch socket na ukaweka charger yako vizuri... Kwa kifupi gari hili linabadili umeme wa dc kwenda ac.

Kwa watu wanaopenda kutumia laptop wakiwa safari hii gari unaweza kutumia laptop toka Dar mpaka Mwanza, bila kuizima unafanya kazi tu au unaangalia series.

2. Gari hii inakuja na kifridge kidogo kuweka vivywaji uwapo safarini.

3. Gari hii ina option ya 4WD

4. Gari hii inakuambia muda wa kupumzika ukichoka safarini.

5. Gari hii inakuja na mziki mzito yaani subwoofer isiyojaza buti.

6. Gari inakuja na seat 7.

7. Gari hii ina option ya manual na automatic.

8. GARI hii ina gear 6, inaifanya itumie mafuta kidogo.

Hii gari bei yake ipo chini ya kina harrier, kulger na Vanguard. Kitu ambacho hivi vitu vyote vingekuwa kwenye hizo gari bei zake zisingeshikika.
Hii gari naifahamu sana hasa ya Diesel.
 
Mkuu acha zako niko na Mitsubishi Outlander ni gari imara na ngumu tena sio ngumu tu ngumu kwelikweli!! Acheni maneno ya vijiweni
Tatizo letu Watanzania tunajifanya tunajua kila kitu, hakuna gari iko comfortable kama hiyo! Achana na toyota zinazovibrate dashboard! Unaweza kuta mtu hapa anachangia kwamba sio gari nzuri wakati hakuwahi kumiliki hata boxer pikipiki!!
 
Hakuna janja janja jamaa wako smart hakuna longolongo, nishaagiza gari kwao zaidi ya mara mbili. Mimi huwa naingia kwenye website yao sijawahi kutumia ofisi zao za Dar. Isitoshe nna account kwenye website yao

Hakuna ubabaishaji ni hayo tu.

Hata mimi nishaagiza mara mbili moja kwa moja. Document ndo walituma kwenye office za Dar. Na walinipa discount kutoka kwenye bei ile unayoona mtandaoni
 
Tatizo letu Watanzania tunajifanya tunajua kila kitu, hakuna gari iko comfortable kama hiyo! Achana na toyota zinazovibrate dashboard! Unaweza kuta mtu hapa anachangia kwamba sio gari nzuri wakati hakuwahi kumiliki hata boxer pikipiki!!

Mkuu tupe mawili matatu kuhusu hii chuma Mitsubishi Outlander... yenye 2.0L cc: power & stability; comfortability; reliability (uimara kwa matumizi ya rough road mda mwingi); na fuel consumption ipoje.

-Kaveli-
 
Tatizo letu Watanzania tunajifanya tunajua kila kitu, hakuna gari iko comfortable kama hiyo! Achana na toyota zinazovibrate dashboard! Unaweza kuta mtu hapa anachangia kwamba sio gari nzuri wakati hakuwahi kumiliki hata boxer pikipiki!!
🤣🤣🤣🤣🤣 "Mtu anachangia kwamba sio gari nzuri wakati hakuwahi kumiliki hata boxer pikipiki" mwisho wa kunukuu!
 
Outlander hapa ili buniwa vilivyo,imekaa kibabe zaidi
BM220047_4f6187.jpg

Halafu Kuna wachawi Wachache
Wanaponda kutokea kusikojilikana
BM469460_fbda79.jpg
 
Back
Top Bottom