GalileiGalileo
Senior Member
- Nov 19, 2011
- 165
- 225
Nikiwa mmoja wa Wadau na Watumiaji wa huduma za Mitandao ya Simu za Mikononi haswa upande wa DATA, ninasikitishwa na HUDUMA MBAYA au zilizo CHINI YA KIWANGO nnazopata kwa sasa nikilinganisha na miaka iliyopita. Inasikitisha kuona tunapiga hatua kurudi nyuma badala ya kwenda mbele!
Mimi ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Vodacom zaidi ya miaka 9 sasa, nimekuwa nikitumia internet ya kampuni hii kujifunza, kuhudhuria madarasa ya mitandaoni (online learning), kupata taarifa mbalimbali, kutafuta ujuzi katika kuboresha ufanisi ofisini, kufanya mawasiliano mbalimbali Duniani kwa mahitaji mbalimbali, nk. Nilifika wakati ambapo nilikuwa na-refresh mind kwa kuangalia SERIES mbalimbali mitandaoni moja kwa moja (live) kama vile naangalia TV! Bila kumung'unya maneno, hapa ndipo Dunia ilipo kwa sasa.
Cha kusikitisha, kwa siku za hivi karibuni, nimeshuhudia huduma hii muhimu kwa Dunia ya sasa ikiporomoka kwa mwendokasi ambao haulezeki na hivyo kutuacha sisi Wabongo katika Dunia tofauti na hii walio wenzetu. What's going on here?!!!!
Mwanzo nilidhani ni Voda tu, ila kwa UTAFITI mdogo niliofanya nimegundua kuwa ni MAKAMPUNI YOTE ya simu za mkononi (Mobile Phone Companies), kwani wakati nalalama kuwa sipati huduma niliyozoea toka Vodacom, kwa mshangao nilisikia toka kwa watumiaji wa mitandao mingine kuwa hali ni hiyo hiyo, hata Halotel ambayo imezaliwa hivi karibuni! No way! There must be some common problem somewhere!
Nasubiri kwa hamu toka kwa Wamiliki wa Makampuni haya kujua kama kuna some tangible issues why these services have gone down to this extent!
Ahsanteni na nasubiri majibu, kama na ninyi mmetekwa mseme! Otherwise wajitokeze watumiaji wa mitandao mingine wanipinge kwa evidence kuwa tatizo ni kwa Voda tu au ni kwenye line yangu tu!
NB:
Sijawahi kutumia mtandao wa TTCL kwa kuwa naishi eneo ambalo hawana hiyo huduma ya "mobile", be it voice or data.