Mitandao ya simu ya Tanzania na siri zao, jionee mwenyewe

kirusi cha ukimwi

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
799
644
MITANDAO NA MAZURI NA MABAYA YAO (KASORO) AMBAZO ZINATUPA STRESS WATUMIAJI NA KUAMUA KUKAA NA MALAINI 1000 KIDOGO


THIGO TZ
KUPIGA SIMU- unampigia simu mtu hapa na hapa unaambiwa hapatikani ni shida tupu kama una mgonjwa na unatakiwa uite gari la kumbeba anaweza akafia nyumbani .
INTERNT - Yaani ni mwendo wa spidi ya kobe japo wanasema wa 4G LTE hakuna lolote labda iko DAR tu basi ni shida tupu ukitumiwa picha whatsapp ina 59Kb ita load mpaka kesho mh patamu hapo

KUTUMA SMS - kwanza niseme kabisa ukituma sms zinanasa sana yaa ukituma inakuwa delivered after some minutes au hours na kama bahati yako mbaya sana ukituma asubuhi inafika jioni , niseme tu ukweli nilishawahi kugombana na demu mmoja nikajua ananifanyia maksudi namtumia sms hanijibu kumbe ni limtandao basi kwa hasira nikamchenjia demu.

HUDUMA KWA WATEJA - Hapa napo pana kajipu inabidi katumbuliwe huduma kwa wateja inasumbua balaa mara uambiwe unalipia dah

VIFURUSHI - Havieleweki halafu vingiii mh

MATANGAZO - matangazo hayaendani na wanachokitoa na wanajitangaza sana kuliko kazi au huduma utasikia 4G na wakati ni G au E

UKIKWANGUA VIBAYA VOCHA - mtandao kama hawa jamaa na wengine isipokuwa foda peke yao ndo wanaweza wakakusaidi moja kwa moja kwa huduma kwa wateja kupewa vocha yako wengine noooo mpaka uende ofisini kwao sasa jero ndo nipige safari mh hivyo hilo nalo tatizo

TUINGIE SASA KWA HEWATEL

HEWATEL AU EATEL
KUPIGA SIMU- ukipiga simu inakata mpaka urudierudie na kama una shida ya haraka itakula kwako hivyo hawa na wale wa mwanzo hawana tofauti kwa hili labda kale ka sauti ka mdada wa karibu ........ simu ya mteja unayempigia haipatikani
INTERNET - Hawa nao ni shida tu hawana tofauti na wale wa thigo tofauti rangi ya mabango tu na majina mh internet spidi ya kobe ni mwendo wa G na E
KUTUMA SMS - hawa jamaa wako vizuri katika suala la sms yaani ukigusa tu kitu delivered mpaka raha yaani unaweza kuzani uko hapa na hapa na unayechat naye hivyo nawapa 100% kwa hili

HUDUMA KWA WATEJA- Wako vizuri pia kwenye hili nawapa 100 %

VIFURUSHI - vifurushi havina shida

MATANGAZO - hawa walau hawana mbwembwe sana

SASA NGOJA TUINGIE KWA WAZEE WA KAZI NI KWETU YAANI FODACOM TZ

KUPIGA SIMU- wao hawana shida unampigia mtu na kumpata

INTERNET - hawa ni wababe wa internet wamedumu kwa muda mrefu sana toka miaka ile ya tanzania leading cellular network mpaka leo kazi ni kwetu na 3G yao HSDPA nawapa heko japo sasa hivi wanapata ushindani mkubwa kwa mtandao ambao hata hawajitangazi bali wao wanapiga kazi tu na si wengine ni HALOOTEL

KUTUMA SMS - hawa hawana shida sana japo mara moja moja huwa wanazingua

HUDUMA KWA WATEJA- wako vizuri sana na wana wahudumu ambao wako vizuri kwenye mambo mbalimbali nawapa heko

VIFURUSHI - Vifurushi viko poa havina tatizo

MATANGAZO - wanachokitangaza kinaendana na uhalisia wa kile wakifanyacho hivyo ni wakweli

UKIKWANGUA VOCHA VIBAYA -hawa wanakupatia ufumbuzi kwa kupiga simu huduma kwa wateja tu mambo yanakuwa poa tofauti na wengine mpaka ufike ofisini kwetu

TUJE KWA WA VIETNAM SASA WAZEE WA SPIDI KALI

KUPIGA SIMU- wako vizuri hawana shida ila siku kukiwa na mawingu ujue mtandao hakuna

INTERNET - spidi kali ya internet na haikwami hata ukiwa you tube na ndo wababe wa internet kwa sasa wakifuatiwa na wakongwe fodacom tz

KUTUMA SMS - hamna shida kabisa

HUDUMA KWA WATEJA -hawana shida unawapata haraka

VIFURUSHI- Havina shida

MATANGAZO - hawajitangazi kwa mbwembwe wanajitangaza kwa kazi yao nzuri HSDPA

UKIKWANGUA VOCHA VIBAYA - msaada mpaka uende ofisini

KWA VIGEZO HIVYO MIMI NINGEPENDA KUIPA MITANDAO HII NAMBA KUTOKA ULIO BORA ZAIDI KUJA WA MWISHO KAMA IFUATAVYO

1. FODACOM TZ

2. HALOOTEL TZ

3. EATEL TZ

4. THIGO TZ

JE WEWE UNAONAJE?

NAWASILISHA .
 
hayo matatizo labda ni hayo maeneo yako. tigo, vodacom, halotel na airtel hii mitandao mimi eneo nililopo zote ziko poa na spidi ya maana hasa airtel na halotel. tigo huku nilipo 4G yao haina tofauti na 3G ya airtel lakini kiujumla swala la internet nalidhika na mitandao yote niliyotaja. kutokana na ghalama kuongezeka na kupunguza mb nimeamua kustiki na halotel pamoja airtel maana ndo penye unafuu. sikuwahi kukumbwa na hayo matatizo uliyoyataja mimi binafsi namiliki laini nyingi kwa sababu ya internet na nimeachana na vodacom kwenye internet naitumia voda kwa kupiga na kupokea simu tu.
 
Mi hiyo namba moko nilianza kuitumia tangu 2000 ilipoingia nchini, sijawahi kubadili, ingawa kuna wakati wananikera hadi nishawahi tukana sana wahudumu wao.
 
Mkuu nadhani spidi ya mtandao inaendana na eneo utakalokuwa lakin by my experience vodagooo wako poa Sana kwa mwanza labda na maeneo mengine
 
hayo matatizo labda ni hayo maeneo yako. tigo, vodacom, halotel na airtel hii mitandao mimi eneo nililopo zote ziko poa na spidi ya maana hasa airtel na halotel. tigo huku nilipo 4G yao haina tofauti na 3G ya airtel lakini kiujumla swala la internet nalidhika na mitandao yote niliyotaja. kutokana na ghalama kuongezeka na kupunguza mb nimeamua kustiki na halotel pamoja airtel maana ndo penye unafuu. sikuwahi kukumbwa na hayo matatizo uliyoyataja mimi binafsi namiliki laini nyingi kwa sababu ya internet na nimeachana na vodacom kwenye internet naitumia voda kwa kupiga na kupokea simu tu.


Halotel hamna kitu.....airtel ni bure mm nipo kimara ila speed yao ni mbovu kinyama....ukitaka huduma kwa wateja ni kero tupu ili lipo Airtel na halotel niliwai piga huduma hii tangu magomeni mpaka kimara hawajapokea ni nyimbo tupu.....vocha halotel mpaka ufunge safari.....voda wezi watupu m.pesa.....tigo nao tigo pesa ugoro mtupu salio likibaki kama haupo makini wanakwangua kiujanja.....Tcra haya majipu mnayasubiri yakaukie hama mana tangu mwaka jana kero ndo kama hizi.....
 
Mimi niko Dar naishi Boko,tigo sipat 3G,kuna mda inakuja H au H+ na si mara zote me ni mzee wa E nimepiga kelele weeee tiGO ila hadi sasa hawajaboresha
 
Halotel bado network haijaanza kuchemka.... Switch yao haibebi hata call 50,000.... So nendeni mkijaa mtarudi.... Ila nawasifu kwa kuingia na kusambaza mtandao maeneo mengi
 
Vyodakom ni wezi wa salio na M-Pesa balaa. Ukijiunga na kifurushi kiki-isha utakoma, salio lililobaki litalambwa lote kwa sekunde chache tu utajikuta hamna kitu. Ukiwa mteja wa huu mtandao inabidi uwe na timing kama mchinja kobe.
 
mi natumia tigo jombaa, na hata nikitumia ki-itel net inakamata fresh, labda kama upo inamankusweke
 
Halotel wako vizuri sana! Hata sisi wa vijijini tunajihisi kama tuko mjini vile. Sema vifurushi vyao ni ghali sana.
 
Mahali nilipo tigo heko kwangu.

1gb kwa 1000 mwezi mzima
500mb kwa 500 siku 7
whatsapp siku 30 kwa 500

internet ya kasi sina budi kuwapa heko ni namba moja kwangu halafu wanafuata Halotel
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom