Tongo Elamu
JF-Expert Member
- Apr 26, 2020
- 2,904
- 4,404
Hawa voda ndiyo balaaa. Ukiweka 700mb sasa hivi, dakika kumi kuperuzi jf tu ni nyingi kabla hawajakupekekea ujumbe mb zako zimeisha.Ni dhahiri kwa sasa ukiweka bundle linaisha kwa haraka kwenye data, na sababu ni Makampuni ya simu kuibia wateja Mchezo huu umekithiri sana sasa kuelekea uchaguzi.
Ni kosa makampuni ya simu kifanya wizi wa kidola dhidi ya watumiaji
sina pesa ila nina tumia chini ya mb500 pekee kwa wiki nzima na haziishi gentleman,Nina ufahamu wa kutosha kuhusu speed za internet. Sibahatishi nisemacho. Hakuna ufahari wa kuibiwa na kusema hujali kisa utakuwa na fedha nyingi.
Hao ovyo sana.Yamenikuta haya juzi 1.4gb iliisha ndani ya dk 5 na sikuwa nadownload chochote. Yas endeleeni kutumixx.
Yote hayo nimefanya. Huwa sichezi clip zozote. Sina app yoyote ambayo sina ufahamu nayo boss wangu.Wakati mwingine tunailaumu mitandao ya simu kwamba wanaiba data kumbe tatizo ni sisi.
Kama unatumia mtandao wa simu kupata huduma za data, fanya yafuatayo ili data yako isiishe upesi:
- Zima data taustani (background data) kwa apps ambazo huzitumii mara kwa mara.
- Tumia toleo la "lite" la apps kama Facebook Lite, Instagram Lite, nk.
- Epuka kuangalia video za HD au kuzipakua bila sababu ya msingi.
- Tumia Wi-Fi unapopata nafasi badala ya kutumia data ya simu kila mara.
- Zima auto-update ya apps kupitia data; badili iwe Wi-Fi tu.
- Funga auto-play ya video kwenye mitandao ya kijamii kama TikTok, Instagram, na Facebook.
- Tumia Data Saver Mode ikiwa simu yako inayo.
- Fuatilia matumizi ya data kwa kutumia mipangilio ya simu au apps za mtandao wako.
Sawa mkuu. Changamoto kubwa inakuja pale unapotaka kupeleka malalamiko ya namna hii kwa mtoa huduma wako wa simu. Ni lazima uwe na ushahidi wa uhakika ili kuthibitisha madai yako kwamba kweli data unazopewa zinatumika kiwivi. Vinginevyo, unapaswa kujiridhisha kwa kufuatilia matumizi halisi ya data kwenye kila aplikesheni. Unaweza kupata ripoti kamili ya matumizi ya data kwenye simu yako itakayokuonyesha kama kweli aplikesheni zako hazitumii data hata kwa nyuma (background), lakini ukikabidhiwa kifurushi, data inaisha ghafla ndani ya muda mfupi.Yote hayo nimefanya. Huwa sichezi clip zozote. Sina app yoyote ambayo sina ufahamu nayo boss wangu.
Vodafone ni vinara wa huu wizi wakifuatwa na Yaas. Hii Wizara haijapata Waziri wa kueleweka wa kuisimamia. Wangemruhusu Musk aje na Starlink ili tuzike rasmi huu mitandao ya kipigaji.Ni dhahiri kwa sasa ukiweka bundle linaisha kwa haraka kwenye data, na sababu ni Makampuni ya simu kuibia wateja Mchezo huu umekithiri sana sasa kuelekea uchaguzi.
Ni kosa makampuni ya simu kifanya wizi wa kidola dhidi ya watumiaji
punguza mihemko bas gentleman unaedai kuibiwa mb wakati unatumia 5g halafu unaweka mb200🤣Usiwe mjinga ww.
mjanja unalamikia kuibiwa MB, mara umeibiwa kura n.kNarudia tena, usiwe mjinga.