Mitandao ya simu kuweka sauti za miito kwa watumiaji bila ridhaa yao

Nyabutoro

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
1,340
1,595
Habari wana jamvi.
Leo nineona ni vema kuwashirikisha katika jambo hili ambalo limekuwa likifanywa na mitandao ya simu bila ridhaa ya mtumiaji.Jambo lenyewe ni kuwekewa mwito unaosikilizwa na anayekupigia bila wewe kuuridhia.Mfano unawekewa wimbo wa mapenzi/kutongozana alafu ukipigiwa na mama mkwe anajisikia vibaya au kukuona kama muhuni vile, au wewe ni mchungaji/shehe unawekewa wimbo unaoenda tofauti na maadili ya dini yako.
Kwa mawazo yangu nafikiri jambo hili si sawa.Ifike mahali mitandao isilazimishe biashara.
Nawasilisha.
 
Mkuu siyo nyimbo tu hata huduma nyingine mfano sijui hadithi,ujumbe wa mapenzi N.K wanakera sana unakuta unakatwa pesa bila ridhaa yako na ukiwapigia unaambiwa ulijiunga na huduma fulani wakati katika kumbukumbu zako hujawahi fanya hivyo
 
Halafu baadaye wanakwambia Mteja unayempigia hapatikani.
 
Back
Top Bottom