Mitandao ya Simu: Huwa mnarudisha vipi fedha zilizopo kwenye akaunti za simu za watu wanaofariki kwenye majanga kama ya moto au maji?

mbutamaseko

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
735
1,050
Fikiria tu mfano wa kilichotokea Morogoro jana. Watu waliungua wakiwa na simu zao mifukoni na lazima baadhi walikuwa na fedha kwenye Tigo pesa au Mpesa zao.

Je, hizi pesa mwisho wake huwa nini? Sijawahi kusikia mtandao wowote unatangaza kurudisha pesa kwa familia za ndugu ambao wanahofiwa kufa.

Kungekuwa na utamaduni wa kutangaza majina ya namba ambazo zimekuwa 'dormant' sana ili kama kuna ndugu wajitokeze watoe taarifa kuhusu wapendwa wao na kama kulikuwa na chochote kwenye simu zao basi ndugu wapewe.

Ni watu wengi walikufa nungwi kule, lakini pia Mv Nyerere iliuwa wengi sana. Unadhani fedha zao ziliishia wapi? kumbuka watanzania wengi wamefanya hizi simu kua Benki zao hivyo fikira ni pesa kiasi gani zinazopotea wakati warithi wapo.
 
Ikifika muda mrefu laini haitumiki huwa inafungwa na pesa huliwa/ hupelekwa kwa trustee ya serikali kwa ajili ya kutunzwa, itategemea na uadilifu wa wahusika
 
Miaka ya nyuma wakati mpesa inaanza nilipewa form ya kujaza ya kukubali terms of condition za mpesa,,
Nakumbuka kuna icho kipengele kinaeleza mzigo unapelekwa kwenye account maalum BOT,
 
Back
Top Bottom