Mitandao ya simu hili tatizo ni kero

Midekoo

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
43,293
233,235
Habari waungwana,
Muda mwingi napendelea kusoma mada za jamii,forum japo si mchangiaji kwa sana napenda kutoa hongera kwa mwanzilishi wa huu mtandao pamoja na wachangiji wote wa jamii forum.

Leo na mimi nimeamua kuwasilisha tatizo langu kwa hii mitandao ya simu hasahasa kwenye hizi huduma za kifedha.

Huduma za kifedha za kwenye simu zimeweza kunisaidia hasa kwenye shughuli zangu za biashara , lakini kuna tatizi moja ambalo kwakweli huwa linanikwaza na lipo karibia mitandao yote.

Mtu unatuma pesa , pesa hazimfikii mlengwa ukiwapigia simu Huduma kwa wateja unambiwa pesa iko hewani kuna matatizo ya kimtandao, kama mnajua kwa muda huo mna tatizo la kimtandao kwanini msitume ujumbe kwa wateja wenu wasifanye mihamala yoyote ya hela mpaka pale mtandao utakapokaa sawa .

Unarudishia pesa baada ya siku 3 hii si haki kwa kweli.,Huu ni uuwaji unajua hiyo pesa kwa muda huo nilitaka kuifanyia nini.
Nawasilisha hoja.
 
Hata hao mtandao wa simu kama kuna tatizo wawajui mpaka ww uwape taarifa mkuu....technology yetu iko chini sana katika hizo huduma....
 
Back
Top Bottom