Mitandao ya kijamii na maadili ya Tanzania

mwanahabari93

JF-Expert Member
May 20, 2015
263
169
Mitandao ya kijamii inazidi kuongezeka katika dunia ya leo na inazidi kuwa na misaada katika nchi zinazojitambua na kuleta madhara makubwa katika nchi zetu za dunia ya tatu mfano mzuri katika nchi yetu ilio na uongozi bora chini ya rais JPM lakini wingi wa mitandao ya kijamii inazidi kuangamiza nchi yetu ya Tanzania kwa kiwango kikubwa.

Kwasababu vijana wengi hususani wanafunzi washule za msingi na pia vijana wa sekondari wamekuwa wanasahau kabisa maendeleo katika nchi yao na wao wenyewe badala yake wamekuwa wakiwaza jinsi ya kupost picha Instagram, kubadilisha picha kwenye profile zao katika account zao wa Whatsaap wakitaka kujilinganisha na wenzetu wa nchi za kigeni tunazidi kuona maadili ya nchi yetu yakizidi kushuka kutokana na mitandao hii ya kijamii kwa watoto wetu.

Sitoshangaa na wala sishangai kuona ufaulu wa vijana wakitanzania katika ngazi mbalimbali za tanzania za elimu nzinazidi kushuka. Baya zaidi pia wafanya kazi wa makampuni mbalimbali wamekuwa wakijisahau katika kufanya kazi za makampuni yao na wamekuwa wakipoteza mda mwingi katika kuchati kupitia kompyuta za ofisi.

Mitandao ya kijamii ni mizuri sana endapo itatumiwa vizuri naiona Tanzania iliojaa wajinga, naiona Tanzania ilioharibika kimaadili naiona Tanzania ya wahuni naiona Tanzania ilioangukia kwenye dimwi la umaskini kutokana na mitandao endaapo watu watazidi kutumia hii mitandao vibaya.Endapo tutatumia vizuri tunaweza kufika mbali kiuchumi na kisiasa.

TANZANIA NAKUPENDA:):):)
 
Naiona Tz mpya yenye Neema,, Mabadiliko vijana kushika dola.. vijana kuongoza Africa.
Ni zamu yangu mimi na wewe kuchange Tz
 
Back
Top Bottom