Kulingana na ratiba iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano, na Mipangilio ya Kuelekea Dijitali kabla ya Ukomo Wa Analojia tarehe 17 June 2015, hakuna mpango wowote wa kuwasha mitambo ya analojia kwani gharama za kuendesha mifumo yote miwili ni kubwa na hakuna wa kuzigharamia kwenye maeneo ambayo yana dijitali.