green rajab
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 12,247
- 38,811
Mataifa makubwa hapa duniani mfano G7 hua na mifumo ya kimaslahi ya muda mrefu ili kujipatia utajiri wa kiuchumi, nguvu ya kisiasa na Kijeshi mfano usikute D.Trump na rais wa N Korea wanawasiliana vizuri tu na wanacheka safi kabisa ila ki nachowaunganisha maslahi Marekani ili iendelee kukaa South Korea, Japan na Philippine inabidi North Korea iendelee kua tishio Ili Marekani aendelee kuuza silaha kwa hizo nchi na pia Marekani lazima aifanye Iran kua tishio kwa mashariki ya kati ili aendelee kuuza silaha Saud arabia, Jordan, Kuwait, Pakstan na nk Upande wa Ulaya anaitangaza Russia kua adui ili a supply silaha nchi za NATO, Hali kadhalika China dhidi ya jirani zake India, Taiwani, Vietnam. Ukiangalia juzi USA amefanya jaribio la kudungua ICBM anajiandaa kufanya biashara na West Europe dhidi ya Russia Pia tumeona Russia inavyoanza kuuza silaha zake baada ya kuzifanyia Promo Sryia kwa hiyo haya yanayoendelea hapa duniani yanapangwa watu wachache wenye maslahi yao mfano kueneza magonjwa ili kuuza madawa na viwanda viendelee kuingiza faida pia