kichuminyi
JF-Expert Member
- Mar 4, 2014
- 234
- 173
Nazungumzia hizi mita zinazotumia remote.
Sina shida na lengo kuu la kudhibiti mianya ya wizi wa umeme, shida yangu ni kwenye ubora wa hizi mita na remote zake na hasara inayo patikana kutokana na ubovu wa mita hizo na usumbufu kwa wateja.
Mimi binafsi nilifungiwa mita hii mwezi July 2015, lakini ilifanya kazi kwa siku 4 tu ikawa haiingizi umeme, baada ya kutoa taarifa nikapewa clear temper namba niingize, kweli umeme uliwaka lakini kesho ukazima. Nikarudi tena Tanesco nikapewa number nyingine hali ikawa hivyo hivyo baada ya siku nne ukakata tena.
Mafundi wakaja kucheki wakadai mita mbovu, kinachofuata ni kuandikiwa maombi ya mita nyingine.
Nikaenda ofisini kwao nikauliza sasa mnakuja lini kunifungia hiyo mita? Wakadai kuwa maombi kama yako ni mengi kwa hiyo itachukua kama miezi miwili hivi. Niliumwa kichwa ghafla maana hapo nimekaa miezi 5 baada ya kulipia ndipo nikafungiwa, sasa hivi naambiwa tena nisubirie miezi 2 ili hali hata zile unit 50 za kwanza sijazimaliza na kosa si langu lkn nilivumilia baada ya miezi 3 ya kuvutana kila siku Tanesco ndipo nikafungiwa. Bahati mbaya mimi si mtoaji wa chochote kwenye haki yangu.
Wiki tatu zilizopita mita ya shangazi yangu aina hihi wakati ule wa ile mvua kubwa ya siku moja hapa Dar na radi zake nayo ikazima. Amepewa number za ku clear mara mbili lkn hamna kitu, baadaye wanasema imeharibika wakati hata miezi 6 bado??
Hao hao mafundi wa Tanesco wanadai mita hizi zipo chini ya kiwango. Maana malalamiko ya mita hizi kuharibika ni mengi mno kuliko yale matoleo ya kwanza. Binafsi kwa wazazi wana ile luku ya zamani ni miaka zaidi ya 15 lkn haijawahi kuwa na tatizo.
Najiuliza kama ni kweli zipo chini ya kiwango kwa nini ziliingizwa?
Je ni bei nafuu ndio ilifanya ziingizwe? Kama ni unafuu wa bei, mbona wateja tunalipishwa bei za juu?
Zile remote nazo ni majanga maana button zinatoka mojamoja zenyewe.
Naomba wahusika habari ziwafikie popote pale walipo, kama ni jipu basi litumbuliwe tu, maana hamna namna