ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,785
- Thread starter
- #201
70% ya matatizo ya Tanzania ni ujamaa mentalityNilidhani utatetea hoja kwa kunipa link yenye mantiki kumbe unanipa porojo jlizoziandika mwenyewe. Kwani china ilivyoacha ujamaa imeacha kila kitu cha kijamaa? Au unadhani kumilikisha ardhi wageni ndio ufumbuzi wa tatizo la umaskini tanzania? Hata kenya wageni wana ardhi na bado wakenya ni maskini na wengine wanakufa njaa. Hata zambia wageni wana ardhi na umaskini upo mwingi sana.
Ingawa sipingi wageni kumiliki ardhi,lakini najua ujamaa si chanzo cha matatizo yote ya tanzania. Nilikupa mifano mingi ya uongozi mbovu na suluhisho lake,lakini kwa mtu kama wewe wa kusifia sifia huwezi ona hilo. Uduni wa fikra ni shida sana.Unadhani kumsifua samia ndio kutaondoa umaskin tanzania? Au mwenzetu hizi rushwa zilizoongezeka huoni ni kama tatizo kwa maendekeo ya nchi? Ina maana hata huoni aibu kuona mkuu wa mkoa au mbunge anayelipwa milioni kama 17 kila mwezi wakati wananchi wake hawana hata maji safi ya kunywa? Hapo utalaumu ujamaa?