Mishahara ya watumishi wa umma iwe wazi

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Kwa kuwa rais ametangaza mshahara wake sasa mishahara ya watumishi wote wa umma iwekwe hadharani. Usiri uliowekwa na awamu ya pili ulikuwa kuficha Ubadhirifu.
 
Mshahara wangu 480000/= apo hujakata PAYE na makato mengine..Alafu eti mwingine anajitangaza kua analipwa 9.5M nauku kila kitu anapewa bure....
 
Tanzania yetu hii ni walimu peke yao ambao mishahara yao inafahamika. Watumishi wa kada zingine ni ngumu sana kufahamu mishahara yao.

Tunaomba muweke wazi kwa wote, kwani wanachokijua wananchi ni TGTSD1, C5, F1 etc.
 
Hivi Watumishi wa Umma ni kina nani, Je Rais, VP, PM na Ministers ni Watumishi wa umma (civil servants)? Msaada
 
Tanzania yetu hii ni walimu peke yao ambao mishahara yao inafahamika. Watumishi wa kada zingine ni ngumu sana kufahamu mishahara yao.

Tunaomba muweke wazi kwa wote, kwani wanachokijua wananchi ni TGTSD1, C5, F1 etc.
Mishahara na scales za mishahara vipo wazi mbona? Sumbua ubongo wako...
 
Hangaikeni na salary slip za watu ...msahau wana mishemishe nyingine mtaani.

Nimeona watu wengi wenye mishahara midogo na bidiii za kilimo ufugaji na biashara wenye maisha mazuri na mafanikio kuliko mabosi wao
 
Acha ujinga,mishahara ya watumishi mbona iko wazi...uwe unafuatilia mambo

Wakati wa awamu ya kwanza ngazi za mishahara (salary scales) zilikuwa zikichapishwa kwenye gazeti la Serikali na kwa kila fani na elimu. Kwa mashirika ya umma kulikuwa na tume ya mishahara na maslahi ya watumishi wa mashirika yote. Kwa sasa kuna usiri mkubwa kuhusu haya na ni fedha za umma zinatumika. Nia ya kuweka wazi ni kutuwezesha kuhoji matumizi mabaya ya madaraka kwa bodi ambayo husababisha ubadhirifu na kuikosesha serikali mapato ya kodi. Dunia nzima ni sisi tu tunafichaficha mishahara na tuna hofu kwa kuwa wahusika wanajua hata dhamira zao zinawasuta kwa kuwaibia wananchi maskini.
 
Back
Top Bottom