Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

hata mbuyu ulianza kama mchicha
hata ukibadili kuni moto ni ule ule
pamba ya zamani
sikutumi mjin
 
Kuoga si kuwa safi, ingekuwa ni kuwa safi taulo zisingechafuka
 
Mie nliwahi kuiona misemo hii:

01. Mganga haagizii samaki
02. Ni kweli lakini hayakuhusu
03. Hata kwetu wapo
04. Jino moja
05. Kula tutakula ila tutachelewa
06. Kula ni kula mbaya kukomba mboga
07. Kumchinja kobe kwataka taiming
08. Ndio basi tena
09. Njaa haina baunsa
10. Hapo vipi??
11. Tatizo muda
12. Kaseme tena
13. Msafara wa mamba na kenge pia wamo
14. Gari bayaaaaaaaa, babako analo?
15. Tatizo mboga
16. Jogoo hafi kwa utitiri
17. Mbuzi yake kamba
18. Kunguru hafugiki
19. Midege isiyoliwa
20. Zimebaki stori

21. Kunya anye kuku akinya bata kaharisha


:welcome:
 
Mimi nilifurahishwa na hii (ingawa maana yake siifahamu):
1. Mutuka munene kange nzela!
2. Naacho cha Ruwa!
 
Bongo bila magumashi hutoki
Yule msiempenda sasa amefika
Bakuli halichagui mboga
Shinda uvizu uje nyemi
 
Siku moja nilikuwa najaribu kulipita Defender moja likawa linaninyima saiti na kunitimulia vumbi, kwa nyuma kwenye wheel cover limeandikwa "EAT MY DUST"
 
Back
Top Bottom