Misamaha ya kisiasa Utamaduni mpya uliojaa ghiliba, uongo na usanii

Mfalme Bugiri ni lazima ATUKUZWE NA KUSIFIWA.

 
Ni kweli kuwa jambo hili la Rais na akins Makamba,Kinana na Nape ni kama jipya kisiasa tena jipya sana....Rais kutoka hadharani na kuweka kipaza sauti pale mbele kwanza sio tamaduni zetu ,misamaha ni kama sadaka ukitoa sio lazima utangaze kwa SABABU aliykutukana hajaweka hadharani isipokuwa umetumia vyombo unavyojua kumweka hadharani ....hayo ya kumweka hadharan yawezekana n matusi madogo tu ulioyafanikisha kuyajua kuna mengine zaidi ya hayo ambayo hukuyajua

Sasa msamaha ni nini ?
Kwa sababu mm ni mkirsto nitakikita kwenye Biblia

Yesu alitumia ulinganisho huo alipowafundia wafuasi wake wasali hivi: “Utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi wenyewe pia humsamehe kila mtu aliye na deni letu.” (Luka 11:4) Vivyo hivyo, alipotoa mfano kuhusu yule mtumwa asiye na rehema, Yesu alilinganisha msamaha na kufuta deni.—Mathayo 18:23-35.

Tunawasamehe wengine tunapoepuka kuweka kinyongo na kutodai malipo kwa sababu ya uchungu au hasara tuliyopata. Biblia inafundisha kwamba upendo usio na ubinafsi ndio msingi wa msamaha wa kweli, kwa kuwa upendo, “hauweki hesabu ya ubaya.”—1 Wakorintho 13:4, 5.

Kusamehe hakumaanishi
Kupuuza kosa. Biblia inawashutumu wale wanaosema kuwa matendo yasiyofaa hayana madhara au yanakubalika.—Isaya 5:20.

Kutenda kana kwamba kosa halijafanywa. Mungu alimsamehe Mfalme Daudi dhambi nzito, lakini hakumlinda Daudi kutokana na madhara ya matendo yake. Mungu alimwongoza Daudi aandike kuhusu dhambi zake hivi kwamba zinakumbukwa hadi leo.—2 Samweli 12:9-13.

Kuwaruhusu wengine wakutumie vibaya. Kwa mfano, tuseme umemkopesha mtu pesa, naye anazitumia vibaya halafu anashindwa kukulipa kama alivyoahidi. Anasikitika sana na kuomba msamaha. Unaweza kumsamehe kwa kutoweka kinyongo, kutomkumbusha-kumbusha jambo hilo, na labda hata kufuta deni hilo. Hata hivyo, unaweza kuamua kutomkopesha pesa tena.—Zaburi 37:21; Methali 14:15; 22:3; Wagalatia 6:7.

Kusamehe bila msingi halali. Mungu hawasamehi watu wanaotenda dhambi kimakusudi na kwa ukatili na ambao hukataa kukubali makosa yao, kubadilika, na kuwaomba msamaha wale ambao wameumizwa. (Methali 28:13; Matendo 26:20; Waebrania 10:26) Watu hao wasiotubu huwa maadui wa Mungu, naye hatazamii tuwasamehe watu ambao yeye hawasamehi.—Zaburi 139:21, 22.

Namna gani ikiwa umetendewa kwa ukatili na mtu anayekataa kukuomba msamaha au hata kukubali kuwa amekosa? Biblia inatushauri hivi: “Acha hasira na uache ghadhabu.” (Zaburi 37:8) Ingawa hutapuuza kosa lake, unaweza kukataa kuendelea kukasirika. Uwe na hakika kwamba Mungu atamtoza hesabu mtu huyo. (Waebrania 10:30, 31) Unaweza pia kufarijika kujua kwamba Mungu ataleta wakati ambapo hatutahisi tena maumivu au uchungu kwa sababu ya mambo yanayotulemea sasa.—Isaya 65:17; Ufunuo 21:4.

“Kusamehe” makosa ya kudhaniwa. Nyakati nyingine, huenda tukahitaji kukubali kuwa hatukuwa na sababu ya kukasirika. Biblia inasema: “Usiwe na haraka kuudhika katika roho yako, kwa maana kuudhika hukaa katika kifua cha wajinga.”—Mhubiri 7:9.

Jinsi ya kusamehe
Kumbuka msamaha unahusisha nini. Si kupuuza kosa au kutenda kana kwamba hakuna kosa lililotendeka—ni kuliachilia tu.

Tambua manufaa ya kusamehe. Kuondoa hasira na kutoweka kinyongo kunakusaidia kuwa mtulivu, kunaboresha afya yako, na kufanya uwe na furaha zaidi. (Methali 14:30; Mathayo 5:9) Jambo muhimu zaidi ni kwamba kuwasamehe wengine ndio msingi wa kusamehewa na Mungu makosa yetu wenyewe.—Mathayo 6:14, 15.

Uwe mwenye hisia mwenzi. Sisi sote si wakamilifu. (Yakobo 3:2) Kwa kuwa tunathamini sana tunaposamehewa, tunapaswa kuwasamehe wengine makosa yao.—Mathayo 7:12.

Uwe na usawaziko. Tunapokuwa na sababu ndogo ya kulalamika, tunaweza kufuata shauri hili la Biblia: “Endeleeni kuvumiliana.”—Wakolosai 3:13.

Tenda upesi. Jitahidi kusamehe haraka iwezekanavyo badala ya kuacha hasira yako iendelee.—Waefeso 4:26, 27.

Kati ya hao wawili (mtoa msamaha ) na muomba msamaha mmoja wapo ,hajaomba msamaha na mmoja wapo hajatoa msamaha ila wana maslah.
 
Kwa hizi aina za siasa zilizopo hapa nchini hivi sasa, zinayapa nguvu maneno ya Trump, ya kuwa Afrka bado inahitaji kutawaliwa tena kwa karne moja zaidi, ili iendane na ustaarabu wa kidunia. Hata kama tunacheza na " matrix" ya "order out chaos" hesabu zake zinaendeshwa hovyo kabisa.
 
Kati ya hao wawili (mtoa msamaha ) na muomba msamaha mmoja wapo ,hajaomba msamaha na mmoja wapo hajatoa msamaha ila wana maslah.
 
Mwehu tu yule
 
nilikuwa naamini JK ni mwanasiasa ila huyu kazidi
 
Kama ingekua ndiyo mimi, nisingeomba huo msamaha wa kinafiki wala nini! Kama mbwai naiwe mbwai tu. Bahati mbaya asilimia kubwa ya wanasiasa wetu nchini, ni wachumia tumbo tu, wabinafsi na wanafiki wakubwa.

Yaani ukiwaona wanavyolilia kubakia kwenye siasa/madaraka, unaweza ukahisi hawana uwezo wa kufanya shughuli nyingine yoyote ile ya ziada wakiwa nje ya siasa!
Nitashangaa sana kama hao Makatibu wakuu na makamanda wastaafu, watakubali kupiga magoti kirahisi tu mbele ya huyo mtaalamu wa koro show! Watakuwa wamejidhalilisha sana! Bora wakaamua tu kufa na tai zao shingoni.
 
Hivi mtu unaweza kuomba msamaha ukiwa umesema ukweli unaouamini ndani ya nafsi yako?!siungi mkono uombaji wao wa msamaha labda kama waliyoyasema ulikuwa uzushi...na kama ulikuwa ni uzushi basi watuombe msamaha watanzania
 
Chadema wepesi kusahau
Alianza kubenea na Komu kuomba msamaha kwa mbowe kwa kumteta na wakasamehewa ila wakisameheana ccm inakua nongwa
 
Chadema wepesi kusahau
Alianza kubenea na Komu kuomba msamaha kwa mbowe kwa kumteta na wakasamehewa ila wakisameheana ccm inakua nongwa
Hebu weka ushahidi hapa... Between kwenye mada yangu kuna mahali popote nimeitaja ccm? Au mnajistukia?
 
Ni siasa za kishamba ambazo zinadhalilisha Taifa
 
Hakuna mwanasiasa mwenye uwezo wa kuyashinda matokeo ya kumnunia boss.

Boss hanuniwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…