Misaada ya China Afrika inavyotesa mataifa ya Ulaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misaada ya China Afrika inavyotesa mataifa ya Ulaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Feb 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]06 FEBRUARY 2012[/h][h=3][/h]

  [​IMG]
  *Yajenga jengo la AU Ethiopia

  Na Danny Matiko

  UMOJA wa Afrika (UA) hivi karibuni umepata jengo jipya la Makao Makuu yake yaliyopo
  mjini Addis Ababa, Ethiopia ambalo limejengwa na China kwa gharama zote.

  Jengo hilo la kisasa lenye ghorofa 20, na ambalo ndio refu kuliko yote nchini
  Ethiopia, limejengwa kwa vyuma vizito na vioo.

  China inasema, jengo hilo ni zawadi yake kwa watu wa Afrika katika kuenzi uhusiano
  mwema uliopo kati yake na bara hili.

  Jengo hilo lenye urefu wa mita 100 kwenda juu, lina kumbi tatu za mikutano, ukiwemo mkubwa wa kukaa watu 2,500, ofisi zenye uwezo wa kuhudumia watu 700, hadhi
  ya kutumiwa na marais wa nchi na mandhari ya kuvutia.

  Jengo hilo limejengwa kwenye eneo ambalo kulikuwa na gereza lililotumika kama
  kizuizini kwa watu "wote", ambao walikamatwa na utawala wa kijeshi kutokana na kuangushwa kwa Mfalme Haile Selassie wa nchi hiyo mwaka 1974.

  Inaelezwa kuwa, wengi wa watu hao waliuawa kikatili wakati wa kampeni iliyojulikana
  kama "Red Terror" (ukatili mwekundu), ambayo ililenga kuwaondoa wale wote walionekana kama wapinzani wa mageuzi ya kutoka himaya ya kifalme kwenda mfumo wa Kikomnisti.

  Ethiopia ni nchi ambayo haikuwahi kutawaliwa na wakoloni kutokana na imani kwamba, ina mizizi ya ukoo wa Mfalme Sulemani wa Israeli, na hivyo basi wakoloni wa Ulaya
  waliiona kama nembo ya Mfalme Daudi wa Israeli ambaye alikuwa Baba yake Mfalme
  Sulemani.

  Kuna wakati Italia iliivamia kwa lengo la kutaka kuitawala, lakini ilishindikana kwa kuwa majeshi yake yalitimuliwa kwa hasara kubwa kufuatia yale ya Ethiopia kusaidiwa na baadhi ya nchi za Ulaya.

  Wakati wa uvamizi huo wa kuanzia mwaka 1936 mpaka 1941, Mfalme Selassie alikimbilia nchini Uingereza ambako alipewa makazi maalumu wakati juhudi za kumrejesha zikifanyika.

  Hivyo, hatua ya utawala wa kijeshi kutaka kuibadili nchi hiyo kutoka Ufalme kwenda
  kwenye Ukomnisti, zilikumbana na kisiki cha upinzani wa raia na ndipo nguvu kubwa
  ikatumika na kupelekea mauaji ya kutisha. Wengi wa waliolengwa ni wasomi, pamoja na
  maofisa waliokuwa katika nyanja mbalimbali.

  Taasisi za jumuiya kimataifa, ikiwemo ya 'Human Rights Watch', Amnesty
  International zimekuwa zikidai kuwa, watu 500,000 waliuawa kikatili, ingawa
  Waethiopia wenyewe huamini kuwa idadi hiyo ni ndogo mno, na kueleza kuwa watu
  waliouawa ni Milioni moja.

  Aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo wakati wa kampeni hiyo ya "Red Terror", Kanali
  Mengistu Haile Mariam, ambaye alitawa kuanzia mwaka 1977 mpaka 1987, kwa sasa
  anaishi nchini Zimbabwe kama mgeni rasmi wa kitaifa.

  Hifadhi hiyo ni fadhila kutokana na kujitolea kwake kuwapatia misaada wapigania
  uhuru wa nchi hiyo, wakati wa harakati za ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

  Rasi Robert Mugabe wa Zimbabwe amekuwa akikaririwa akisema "kamwe", Wazimbabwe
  hawawezi kumtoa mgeni wao huyo kwa maadui zake.

  Kwa upande wa msaada wa China kwa Afrika, zawadi hiyo ya jengo imekuja wakati
  mataifa ya Ulaya yanailalamikia kwa kutaka kuhodhi shughuli zote Afrika ikiwemo biashara za kawaida na miradi mbalimbali.

  Nchi hizo zinasema kitendo cha China kutoa misaada yake, mikopo nafuu, na zawadi
  nyinginezo, bila kuambatanisha na mashariti yoyote kinachangia kwa serikali za Afrika kukiuka haki za binadamu.

  Ingawa taifa hilo la Kikomnisti halijawahi jibu madai hayo, yaani "kuchangia
  ukiukaji wa haki za binadamu", viongozi wake wamekuwa wakieleza kuwa Afrika ipo
  nyuma katika nyanja zote za kimaendeleo na hivyo kuhitaji misaada ya aina mbalimbali ili kujikomboa.

  Akifungua jengo hilo la Afrika siku moja kabla ya kuanza kwa kikao cha 18 cha kila
  mwaka cha wakuu wa mataifa ya Afrika, Mshauri wa Siasa wa Serikali ya China, Jia
  Qinglin anasema zawadi hiyo ya jengo lenye hadhi litabaki kuwa alama ya ushirikiano kati ya Afrika na nchi yake.

  Bw. Jia anasema Afrika ndio mshirika mkubwa wa kibiashara wa China, ambapo kwa sasa
  mtaji ambao nchi yake imewekeza barani humu ni Dola za Marekani Bilioni 130 (sh.
  trilioni 210).

  Bila kutaja viwango, kiongozi huyo alifafanua kuwa China itazidisha misaada yake
  kwa nchi mbalimbali za Afrika katika kiwango cha kurithisha.

  Akipokea jengo hilo jipya, Mwenyekiti wa UA aliyemaliza muda wake, Rais Teodoro
  Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta, alisema jengo hilo linaashiria mwanzo mpya wa
  Umoja wa Afrika, ambao ulianzishwa Julai 9, 2002, na kuurithi Umoja wa Nchi Huru
  za Afrika (OAU) ulioanzishwa Mei 25, 1963.

  Jengo hilo lilijengwa kwa miaka mitatu kuanzia 2009, ambapo kulikuwa na jumla ya
  wafanyakazi 1,200 wa Ethiopia na China.

  Baadhi ya majukumu makuu ya umoja huo ni kuhamasisha umoja na ushirikiano miongoni
  mwa Nchi za Afrika ili Bara hili liweze kuwa na sauti moja ya "hapana ua ndiyo"
  katika jumuiya ya kimataifa; kuratibu na kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi za
  Afrika; kulinda uhuru na kutetea hadhi na heshima ya nchi za Afrika na watu wake;
  na kutokomeza aina zote za ukoloni popote katika Afrika.

  Ingawa inafurahisha na kutia moyo kwamba ukoloni upo ukingoni kutokomezwa, Bara
  linatishiwa na aina mpya ukoloni wa kupora rasilimali za nchi, ambapo washirika wa
  ukoloni huo ni wananchi wenyewe wa Afrika wenye uroho wa mali na ambao
  wanashirikiana na mataifa ya kigeni.

  Ni aina mbaya kabisa ya hujuma, kama ilivyowahi kutokea huko nyuma, ambapo baadhi
  ya viongozi waliojulikana kama Watemi walishirikiana na wageni kuwapeleka Waafrika
  utumwani huko ughaibuni.

  Muungano huo pia una taasisi nyingi ambazo zinajishughulisha na masuala mbalimbali
  ya kisiasa, kiuchumi, kiulinzi.

  Mojawapo ya taasisi hizo ni pamoja na Benki ya Afrika (ADB), yenye makao makuu yake mjini Abdjan nchini Ivory Coast, Afrika ya Magharibi.

  Benki hiyo ni mojawapo ya taasisi muhimu za Afrika, zinazodhamini na kufadhili miradi ya maendeleo katika nchi wanachama wa Muungano huo wa Afrika.

  Chombo kingine ni Bunge la Afrika ambalo lilianzishwa mwaka 2004. Rais wake wa
  kwanza alikuwa Mama Getrude Mongela wa Tanzania, ambaye anasifika kutokana na kazi
  nzuri katika kipindi alichotumiakia.

  Bunge hilo ambalo wabunge wake huchaguliwa kutoka mabunge ya nchi wanachama wa
  Muungano huo, linajumuisha wabunge wa jinsia zote ambao idadi yao ni 265. Makao
  yake makuu yapo Midrand nchini Afrika Kusini.

  Rais wa sasa ni Idriss Moussa wa Chadi, ambaye alipokea kazi hiyo kutoka kwa Mama
  Mongela mwaka 2009.

  Mama Mongela ni muhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika taaluma ya Ualimu,
  na Dkt. idriss ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ndjamena, Chadi, katika taaluma ya Udaktari.

  Kazi ya Bunge hilo ni kuangalia kama taratibu na utendaji wa kazi za Umoja wa
  Afrika zinafuatwa na kutoa ushauri kwa vyombo vya UA.

  Chombo kingine cha Umoja wa Afrika ni Taasisi ya kukuza Ushirikiano wa Kibiashara
  baina ya Nchi za Afrika (NEPAD) ili kuharakisha maendeleo ya bara hili lote.

  Kuna taasisi nyingi za kikanda ambazo zimepewa majukumu yake kulingana makusudio
  ya kuanzishwa kwake.

  Hata hivyo, ingawa umoja huo umepiga hatua katika kusimamia masuala ya amani katika Afrika, bado kuna changamoto za uhaba wa fedha katika kusimamia mambo ya kiulinzi katika nchi wanachama zenye migogoro.

  Mfano ni nchini Somalia, ambapo jeshi la kulinda amani la umoja huo si imara kama
  ilivyotarajiwa, ambapo kutokana na udhaifu wa jeshi hilo katika kudhibita upande
  unaovunja matakwa ya chombo hicho nchini humo, ni baadhi ya mambao yanayosababisha
  amani katika Somalia kuwa kama kitendawili.

  Kabla ya kuundwa UA, OAU ndio lilikuwa jina maarufu la umoja wa Bara hili, ambapo watendaji wake wakuu walijulikana kama Makatibu Wakuu wa OAU.

  Wengi wa viongozi hao ambao walikuwa wanadiplomasia mahiri, walifanya kazi nzuri
  ya kuratibu ushirikiano baina ya nchi zote za Afrika na kuiweka Afrika katika
  hadhi yake.

  Hao ni Katibu Mkuu muasisi, Bw Kifle Wodaji wa Ethiopia aliyetumikia kuanzia mwaka
  1963 mpaka 1964.

  Wengine ni Diallo Telli wa Guinea-Konakry (1964-72); Nzo Ekangaki (1972-74) na
  William Eteki (1974-78), wote wa Kameruni.

  Edem Kodjo, Togo (1978-83); Peter Onu, Nigeria (1983-85); Ide Oumarou, Niger
  (1985-89); Salim Ahmed Salim, Tanzania (1989-2001); na Amara Essy, Ivory Coast
  (2001-2002).

  Dkt. Salim ndiye anashikilia rekodi ya kuutumikia Umoja huo kwa muda mrefu wa miaka
  12 mfululizo, na pia ndiye alisimamia maandalizi ya kuanzishwa UA.

  Miongoni wa viongozi wa Afrika waliosimama kidete kuhakikisha umoja huo wa OAU
  unabaki kuwa imara, ni pamoja na Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia mwaka 1984
  alikuwa Mwenyekiti wake.

  Rais Jakaya Kikwete alikuwa Mwenyekiti wa UA mwaka 2008 mpaka 2009.

  Katika mkutano wa 18 wa viongozi wakuu hao wa Afrika uliofanyika mjini Addis
  Ababa wiki iliyopita, ulishindwa kumchagua Kamishina Mkuu wa Umoja huo, baada ya
  aliyekuwepo, Jean Ping wa Gabon, kutaka kuchaguliwa tena kuendelea katika nafasi
  hiyo.

  Mvutano ulikuwa kati ya Dkt Ping (69), ambaye ni raia wa Gaboni mwenye asili ya
  China, na Bi Nkosazana Dlamini-Zuma (63), ambaye ni mke wa zamani wa Rais Zuma wa
  Afrika ya Kusini.

  Katika upigaji kura za siri, viongozi hao hawakumchagua yeyote kati ya wawili hao,
  ambao kutokana na kanuni za UA, wote sasa wamepoteza nafasi ya kuwania tena
  kuchaguliwa.

  Umoja huo sasa unaongozwa kwa muda na Bw Erastus Mwecha wa Kenya mpaka mwakani
  2013 atakapochaguliwa Kamishina mpya katika mkutano wa 19 wa wakuu hao
  utakaofanyika nchini Malawi.

  Bw. Ping, ambaye alisomea uchumi katika Chuo Kikuu cha Paris, nchini Ufaransa, baba
  yake ni mfanyabiashara wa China liyehamia Gaboni miaka ya 1930 na kumuoa Mgaboni.

  Mwaka jana 2011 alilalamikiwa sana na baadhi ya nchi za Afrika kwa kushindwa
  kuchukuwa hatua za haraka na zilizofaa dhidi ya uvamizi wa Mataifa ya Magharibi
  kule Libya, ambapo kiongozi wa nchi niyo Kanali Muammer Gaddafi aliuawa.

  Kanali Gaddafi alikuwa mfadhili mkuu wa UA katika masuala mbalimbali ya dharula,
  yaliyohitaji kujitolea katika kuchangia fedha za baadhi ya mahitaji ya Umoja huo.   
Loading...