Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 284
- 396
RightMnakuaga na akili hizo mkiwa nje, mkishika madaraka mnakengeuka full kuabudu ngozi nyeupe.
Mama Samia anataka tujitahidi kujijnga kwa hela zetu wenyewe ila watu hawataki
Africa inamalizwa na haya mambo( tawala mbovu, ubinafsi, ufisadi, migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na taasisi mbovu ndani ya nchi husika)
Izo sera aliziweza Hitler tu yaan aliforce ubunifu kwa lazima na akafaulu mengi sana ktk technologia, lakin kwa Africa rais akiwa na sera izo anauawa fasta sana..
Tatizo ni tawala mbovu na makutumizi makubwa ya serikali za Africa
Wazungu wajanja sana wakiona Unataka kujikwamua wanakupa msaada ili akili yako isifanye kazi uendelee kuwa tegemezi.
Tulipojikwamua na corona kwa nyungu na malimao haraka sana wakatuletea msaada wa dozi za chanjo milioni 1.
Nyie ambao mmeongoza nchi toka uhuru ndio ambao mmeshindwa kutumia bongo zenu vizuri hadi leo tunaonekana tunashindwa kusimamia mikopo sawasawa.tunahitaji sana mtu wa design hii ili baadhi ya watu akili zao zikae vizuri, ni aibu sana kuskia kikundi fllan wanalilia misaada, yaaani ni basi tu spo kwenye nafasi ya uongozi kuna watu wangehama hii nchi na wasirudi tena
Nyie ambao mmeongoza nchi toka uhuru ndio ambao mmeshindwa kutumia bongo zenu vizuri hadi leo tunaonekana tunashindwa kusimamia mikopo sawasawa.
Hapo umenena lakini tatizo kubwa si viongozi ni wananchi waliozoea vya bure. Ukimwambia toa Tozo tujenge nchi ni mayowe tupu, matokeo yake unakimbilia katika misaadaDunia imepita kwenye Mapinduzi mbalimbali ya viwanda karibia levels 4.
Ila Unajua Afrika has never succeeded neither of those industrial revolution levels.
Na ukichunguza na kusoma tafiti mbalimbali utagundua misaada na Mikopo ndio imetulemaza na kutuweka hapa tulipo leo.
Nadhani ufike wakati Afrika iachane na misaada na mikopo. Haki mfano mimi nikiwa mkuu wa nchi hii, sera yangu itakuwa ni kukataa na kuachana kabisa na misaada na mikopo ya aina yoyote ile kutoka nje.
Nitahimiza watu wafanye kazi kwa ubunifu, wagunduzi wa dawa nitawawezesha, wanaogundua teknolojia pia watawezeshea, hapo watu watafanya kazi kama punda, hata magari nitapiga marufuku ku-import, nitaruhusu vitu vichache sana ambavyo pengine vitasaidia kutengenezea mitambo tu.
Nitaacha viumane ili akili itukae sawa na hapo watumishi wa Umma watatakiwa kufanya kazi kwa Uzalendo yaani wakubali kufanya kazi kwa mishahara isiyo mikubwa ngazi zote hadi Wabunge, hapo ubunifu lazima uje.
Kama umesomea masuala ya IT...nawapeni pesa kuwawezesha kisha nawapa muda tengenezeni computerized programs, sasa mshindwe muone.
Wote wanaojiita wasomi nitawakusanya na kuwapa assignment kwa maendeleo ya Taifa Sasa mshindwe muone manina cha moto mtakiona.
Kama umesomea Agriculture ni lazima uwe na mashamba na uvune haswa, sasa uwe na Shamba ekari Moja halafu uvune gunia mbili hapo lazima chamoto ukione.
Kwa kiasi kikubwa nchi kama hizi zinahitaji aina fulani ya udikteta ili zisonge mbele yaani UDIKTETA wenye mantiki.